Mimi ni wa Kijijini na ninatolea mfano kwa mazingira ya huku kwetu Idukilo-Kishapu-Shinyanga. Watu wanafadhaiiiiikaaa eti sijui nani karudi au kaenda kwenye LiChama Tawala na upinzani unazidi kuchoka ! Walaaaaa! Sio hivyo kabisa! Upinzani utakuwa kwa asilimia kubwa sana Mwaka huu - subiri kipenga cha Uchaguzi kilie. Mwaka huu wengi watashangaa nawaambia na sikieni maneno haya. Msifikiri Mbowe, Zito, Maalimu Seif na wengineo wamechoka. Hamna aliyechoka hata!
Maisha ya wanasiasa yanategemea siasa. Kwa yanayoendelea huko CCM kuna wengi watatoka - tena wengi sana. Wanasiasa hawana pensheni ya kila mwezi (acha mawaziri wakuu na Rais labda) kama wastaafu wengine. Wanasiasa mpaka wanakufa wanategemea domo - yaani kupiga siasa. Unafikiri kama Makamba Senior, Membe, Kinana (ingawa huyu nafuu), Wasira, sijui nani yule wangekuwa na pensheni km Majaji waliostaafu na kula pensheni nono kungekuwa na kelele?
Ndiyo maana wanasheria wakaitwa wasomi - wajanja sana. Majaji wanakula tu pensheni na mawakili wanaendelea tu na kesi zenu hata kama wana miaka zaidi ya 80. Wanasisasa wakibanwa hapa au wakikosa maslahi hapa wanaenda kule. Tanzania inakuwa kama Kenya soon, mtu kuhama Chama inaelekea kuwa kawaida tu. Demokrasia inakuwa. Sasa usitegemee sisi wanaCCM tunafurahia kuja kupokwa nafasi zetu huku. Ninaona hapa Idukilo ilivyo.
Juzi juzi mtoto wa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa toka huku Kishapu ameingizwa kwenye ajira ya ualimu kinyemela kwa sababu ana kadi ya CCM. Watoto wa WanaCCM wengine na wale wengi ambao hawana kadi za CCM wameshuhudia hilo na wapo mtaani. Kilichotokea wamejenga chuki kwa mwenzao kwa sababu ameshindwa kuwajuza kapataje hiyo nafasi. Na hata kama angewajuza kwani kuna nafasi za kuwaajiri? - kwa maana hiyo CCM imepata kura ya huyo mmoja kwa kukosa kura za mamia ambao ni rafiki zake huyo. CCM inafanya bla bla - INAONWA!
Mtu anahamia CCM kwenda kuwapoka wenzake nafasi - na kweli akipitishwa basi atawafanya wengi warudi opposition kwa sababu hata CCM yenyewe haiwezi kuwapa wote. Mfano Mwaka 2015 zaidi ya wanachama 12 waligombea ubunge na kwa mchujo wa ndani tu alibaki mmoja na hawa wengine waliobaki ni wawili tu ambao nawaona angalau walikuwa na kazi zao na wanendelea na maisha, wengine walihamia upinzani kama 3 hivi na waligombea ingawa hawakushinda lkn angalau walionesha kuchukizwa na mchakato.
Usifikirie kuwa machukizo ya namna hii hayatakuwepo mwaka huu, tena yatakuwa mengi sana. Watu wanaotegemea siasa hawana ujanja mwingine, hata kama wamesoma vipi hurudi huko huko kwenye siasa, tofauti na watu wachache ambao waliwahi kubadilika baada ya upepo kuwachenjia - Marehemu Spika S. Sita na Dr. William Shija ambapo kuna wakati siasa ziliwakataa wakaenda kwenye utendaji. Au mfano mwingine ni Dr Mwale Malechela ambaye akijitoa ufahamu na akija na akajaribu kugombea Mwaka huu huu watu watakaomuunga mkono watakuwa wengi sana. Si ajabu hata Membe naye anaweza akamuunga mkono.
Huku Idukilo hakika wengi tupo CCM lkn kwa uongozi huu ama wengi hatutapiga kura ama akija Mpinzani Mjasiri atatupata tu kiurahisi. CCM kuamua kudeal na upinzani kwa namna hii mnasikitisha sana sana. Mnasabisha chuki dhidi ya watu na hata CCM yenyewe inachukiwa. Watu wanavaa tu nguo zenu kwa shinikizo na kwa woga ili waonekane ni watawala, eti tumeshika hatamu, hatamu gani ya kibabe!?
Uchaguzi huu tutashangazwa sana ninawaambia watu wana hali ngumu (hata posts nyingi zinaelezea hali ilivyo) na watapochukua maamuzi magumu hawatakuwa na cha kupoteza. Hawatapoteza na watapata kupitia upinzani. Hata huku wapinzani wetu wamejipanga kulinda kura zao na wana haki na mkituletea wagombea wa hovyo mjue tutawasaidia wapinzani kulinda kura zao ili watushinde. Mnafanya mambo ya hovyo sana kuchukia upinzani.
Kumbukeni wapinzani ni ndugu zetu, na jirani zetu. Dadangu ana mwanae ambaye ni Mbunge wa upinzani lkn anamsomesha mtoto wa mdogo wetu ambaye yeye ni CCM damu damu. Hapo kuna ubaya au faida?
Acheni hizo CCM, tunasubiri tu kipenga, mchakato wa kibabe this time kama wa Serikali za Mtaa hautakwepo na ukifanyika madhara yake yatawarudi na nyie. Na hii post yangu tutaijadili na wanaIdukilo wenzangu jioni pale kijiweni.