Pre GE2025 Msigwa: Mbowe aliacha tuliyomtuma Ikulu akaenda kushughulikia Billicanas. CHADEMA hakuna Sera ni kudandia mambo ya CCM tu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sidhani kama Chadema kitakuja kudhoofu kiasi cha kupotea kabisa.Naona Tanzania vyama vya siasa vya kudumu vitakavyokuwa vinabadilishana madaraka ni CCM na Chadema.Kama ilivyo Marekani Democrat na Republican au Uingereza ilivyo Labour na Conservative.
Upo sahihi kabisa
 
Kiukweli nmemuelewa sana msigwa. Kwanza ni mtu smart sana kichwani,
Anaongea point tupu,
Mdomo wake unatoa hoja ukizifatilia ni hoja za msingi.
Naomba mnifahamishe sera kuu ya chadema kwa sasa ni ipi?
Msigwa kaanza kwa kumuita Mbowe ni kiongozi wake. Jiulize kwanini bado anamtambua Mbowe kama kiongozi wake.
 
Msigwa unatia aibu wanao, mtoto wako wa kike anajionea aibu.
Msigwa unatia aibu washirika wako, wanasema huna roho mtakatifu na umejiunga na masadukayo.
Msigwa una shida sana!
 
Mchungaji,Samehe 70*7.
 
Rais yupi?. Huyu aliyesema Kilimo tumpe msomali?. Hapana.
 
Weka namba ya Simu ewe chawa.
 
Juzi makala kamsema Mbowe na Jana Msigwa kamsema Mbowe. CCM inatia huruma.
 
Me nadhani kama CCM wana akili timamu
Watakuwa makini na mtu wa namna hii

OVER

Na niwaombe kabla hawajampa teuzi wawafikirie chawa wao waaminifu WASHAMBA wasio hama hama
 

Nataka niwaambie hata hao wazee wa Ccm hapo hawamwelewi
 
Kwa hiyo alikaaa kwenye chama zaidi ya miaka 20 ila leo ndio anajua hakina sera? Msigwa ni spent item, hata akizunguka nchi nzima hana impact yoyote. Yeye asubiri apewe ukuu wa Mkoa au Wilaya astaafu siasa kwa utulivu
Jiulize

Dk Slaa , Zitto, Kitila, Mwigamba , nk

Ni spent item sio?

Msichotaka kusikia ni mbowe kukosolewa na jamaa alivyowafanya mazuuzu mnawamini bila yeye chama kitakufa

Je Leo Mbowe katwaliwa na Mungu je ndio mnasema chama kitakufa?

Mbowe na akina Nkuruzinza Wana Tofauti gan Sasa? Mtu asietaka kupingwa Wala kushindana na wengine?

Wekeni mizani wazi asubuh tu Mbowe anashindwa mapaka na Mtu wa kawaida kama Heche

Nyalandu aliondoka huko Baada ya kujua nyie ni matapeli na hata mkienda kokote Huko Marekani alishawaambia hamna dira Wala sio chama Cha kisiasa zaidi ni chama Cha harakati na mali ya mtu binafsi

Mwenyekiti wa Kanda Ya Kati alisepa
Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani alisepa
Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini alisepa
Mwenyekiti wa Kanda ya Nyanda za juu kasepa

Jiulize maswali mnapoteza brigedi 4 za chama tena hao walichaguliwa na wafuasi wenu Leo mnasema hawana impact yeyote maanake awakuchaguliwa Bali waliteuliwa na mbowe kwa maslahi yake na Mali yake ?

Jiulizeni sana

Mmepoteza Makatibu wakuu wawili , makamu Mwenyekiti Bara , mmepoteza mshaurii , Wenyeviti wa Jumuiya zenu ikiwepo Bavicha

Kama kweli hao ni bidhaa au walikua pandikizi la CCM basi hata mliobakia huko Mtakua pandikizi la Siri la CCM

Ova.
 
Sidhani kama kuna haja ya kupiga kura.Serikali za Afrika zibadilishe mifumo ya utawala ama kwa kuajili wasomi katika nafasi wanazoteuliwa wanasiasa au kufuta kabisa mifumo ya uchaguzi.
Kwanini?
Uongo na unafiki wa wanasiasa unaopekelea Nchi kuingia katika gharama kubwa za chaguzi ambazo pengine zingelitumika kutatua matatizo ya wenyeNchi.
 
Msigwa ni afadhali angejiuzulu siasa, au angekwenda chama kingine cha upinzani. Lakini huu utaratibu wa kupanda majukwaani, na kuponda mambo yote aliyowaaminisha wananchi kwa miaka zaidi ya 20, ni kujidhalilisha, na kuwadharau Watanzania
Ana Uhuru kama aliokua nao sativa na wengine wanaotukana uongozi wa Tanzania .yaani nyie chadema mnataka kuiponda ccm tuh nyie kuambiwa ukweli hamtaki
 
Uhuru wa kusifu na kukosoa ni wa kikatiba.
Msigwa kama alivyokuwa Chadema na sasa CCM anandelea kukosoa.
Siasa ni vijembe.
Kama huwezi kuhimili vijembe vya siasa kaa pembeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…