Pre GE2025 Msigwa na Sugu wamekuwa mahasimu kitu ambacho hakipendezi kwa afya ya chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu anatelekezwa kwa sababu ya hela unaona hata Msigwa mtandaoni ametengwa wameenda kwa Sugu mwenye hela.

Siasa za nchi yetu zimeshapoteza mwelekeo watu wanaingia kwenye siasa kwa sababu ya njaa zao siyo kwa lengo la kusimamia wanachokiamini ?
 
Tatizo la Mbowe haijifunzi. CCM hainaga urafiki wa kweli. Shauri zake, na ndio maana amehairisha kustaafu kisa makubaliano na Samiah.
Kwan hayo makualiano kaingia kama Mbowe au kama mwenyekiti wa CDM? Ni kipi ambacho mwenyekiti mwingine hataweza simamia katika hayo makubaliano? Mwenyekiti ni taasisi si mtu ajue hilo.t
 
Lissu anatelekezwa kwa sababu ya hela unaona hata Msigwa mtandaoni ametengwa wameenda kwa Sugu mwenye hela.

Siasa za nchi yetu zimeshapoteza mwelekeo watu wanaingia kwenye siasa kwa sababu ya njaa zao siyo kwa lengo la kusimamia wanachokiamini ?
Hali hii itakomeshwa na wananchi wenyewe watakapopata uelewa wa kutosha kuhusu maslahi yao na nchi yao na kuanza kuwakataa hawa wachumia tumbo.
Wanatakiwa kupatikana viongozi wachache tu wanaoweza kuisimamia kazi hii ya kuwaelimisha wananchi. Tundu Lissu ni mmoja kati ya hao wengine ambao hadi sasa hawajipambanui na kujitokeza mbele. Hata huko ndani ya CCM wapo, lakini wamizibwa midomo.
 
Kupambana kwa maneno wakati wa kampeni za uchaguzi sio vibaya. Vibaya ni kuyabebaba ya kwenye kampeni za uchaguzi hadi kwenye masuala mengine. Binafsi sitegemei Msigwa na Sugu wapande gari moja kama enzi za CCM Moja! Na pia sioni kama ni afya wagombea wagombea kura kwa kusifiana. Kama mwenzako ni mzuri kiasi unamsifia kwenye kampeni unagombea nae Ili iweje?
 

Wanashindana sio kulumbana. Utamaduni wa kushindana ni mzuri. Na wanashindana wazi hii ndiyo demokrasia msije kufikiri demokrasia ni watu kwenda kunywa chai pamoja. Hayo ni mambo ya baadae wacheni ushani uwe ushindani hakuna matusi ya nguoni wala nini sasa tatizo ni nini?
 

..Lissu na Msigwa ndio walitofautiana.

..ikafika mahali vijana wakawa wanamshambulia Msigwa.

..lakini leo tunasikia Lissu na Msigwa wako " timu " moja.

..Watanzania tujifunze kushindana na kutofautiana.

..mambo ya kulindana'lindana, kudekezana, na kupanda kuabudiwa, ni tabia za Ccm. Tuzikatae ktk vyama mbadala.
 

..sio lazima viongozi wote wa Cdm waende kwenye mkutano mmoja wa Lissu.

..Cdm ni chama kikubwa. Ni lazima wawe na uwezo wa kutawanyika kufanya mikutano ktk maeneo mbalimbali.
 
HUJAIPATA HOJA YANGU. SIKATAI USHINDANI, ushindani ni mzuri sana BUT PEOPLE ARE TURNING INTO ENEMIES.
 
kuna mpaka matusi yanatamkwa na rapper yuko serious kabisa,
Correct, ninaona na bahati nzuri nimeattend hivyo vitu na sikurudi tena! matusi ambayo mashabiki wanayapenda, matusi ya ngono, and all filthy language! after all mashabiki wote wanakuwa wamevuta bangi and other drugs of the same outcome to brain functioning! hao sio watu , ni wehu, wanayama.......
 
Mbowe, Lisu and all concerned, take care of this.

Msigwa na Sugu wanaonekana kujenga "uadui" nawatahadhalisha mbegu hii itaenea pote at the advantage of CCM
Sugu alishamstukia Msigwa kuwa kafika bei, ndiyo maana alikuwa anamjibu shit hata kwenye mdahalo
 
Niliandika hii post May 29, 2024 na mwezi mmoja baadaye inatimia kwa Msigwa kuwa mwanachama wa chama kingine, sio Chadema.

Msigwa ameishi muda mrefu kwenye upinzani kwa maana ya product ya upinzani, lakini sasa hivi yuko CCM. Jiwe moja la upinzani limeanguka.

Ova
 
Kwani kuna 'mchoro' wako ambao haujawahi kutimia? Kuna watu kisha kuna wewe Mdakuzi
Kiumbe mmoja mwenye akili kuliko wote ninaowafahamu, mi nakukubali sana.
 
Kwani kuna 'mchoro' wako ambao haujawahi kutimia? Kuna watu kisha kuna wewe Mdakuzi
Kiumbe mmoja mwenye akili kuliko wote ninaowafahamu, mi nakukubali sana.
Asante sana b..., ujue na mimi nakuaminia hivyohivyo. Kwanza ni mzuri, na una akili na upeo wa juu.

Ova
 
Hili la Msigwa lilianza tangu kipindi kile cha kupinga Wamasai kuhamishwa Ngorongoro, haina shida kuwa na mawazo tofauti lakini namna ambavyo Msigwa alikuwa akli critisize haikuwa na afya kwao, ingawa mimi pia hata sasa bado naunga mkoni Wanadai kuhamishwa Ngorongoro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…