Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Serikali ya Tanzania imethibitisha kupokea tamko kutoka kwa Jumuiya ya Madola linaloitaka kumwachia huru Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ndani ya siku 30. Akijibu swali la mwandishi wa habari, Msemaji wa Serikali alieleza kuwa serikali imeliona tamko hilo na kwa sasa inafanya tathmini ya kina ya maeneo yote yaliyobainishwa kwenye barua hiyo ili kuona namna ya kulitolea maamuzi na majibu rasmi.
Soma: Jumuiya ya Madola yaipa Tanzania siku 30 Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria
"Tamko ni kweli limetolewa. Serikali tumeliona, tunafanya tathmini tuone namna ya kulitekeleza. Lakini, nataka nikwambie Tanzania ni nchi huru, ni nchi inayojiamulia mambo yake yenyewe, lakini ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya kikiba na kisheria."
"Tutafanya tathmini, tutayangalia maeneo yote ambayo Jumuia ya Madola wametuandikia na tutawasiliana nao, tutawapa majibu ya Serikali. Nimemaliza kujibu."
Soma: Wasira: Jumuiya ya Madola haiwezi kutuamrisha, sisi ni Sovereign state