Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Nitazungumzia moja tuu kwenye hoja zako paschal Mayalla
Kuombewa msamaha kwa Mbowe na Zitto hadharani kwenye ule mkutano una harufu zote za stage managed .
Ili kupata kukubaliwa na jumuia ya kimataifa ilibidi Mbowe atolewe kwenye kesi ya kubambikiziwa ikawa si Mbowe wala CDM walikuwa tayari kuomba msamaha ikabidi itumike plan B, enter Zuberi Kabwe Zito.
Ikawa convenient face saving formula na matunda yake tumeona ya mikopo,misaada,na mialiko nchi mbalimbali kitu hakikuwepo kwa hayati Mwendakuzimu.
 
UNA CHUKI ZA KUZALIWA NA cHADEMA, LKN HUIWEZI. HAJASEMA cHADEMA, ANASEMA WANANCHI WOTE HATUNA AKILI KAMA TUNAPEWA WABUNGE WA KUCHAGULIWA NA RAIS HATA KAMA WANAPEWA WAO HAO WABUNGE (MARK HAYA MANENO).
 
Ukiwauliza waliofanya naye kazi za siasa na taaluma watakuambia haya:-

-Mh.Tundu Lissu ni "mgobo"....
-Mh.Tundu Lissu ni "pwagazapwagaza"....
-Mh.Tundu Lissu ni "mjuaji mno"....
-Mh.Tundu Lissu ,HOJA ZAKE ,MAWAZO YAKE ,MISIMAMO YAKE ndiyo iliyo JUU na BORA kushinda ya wengine.......

Nachelea kusema kuwa "grandeur delusion" ni tatizo.......

Eeeee Mwenyezi Mungu tupe HEKIMA kwani ELIMU umeshatupatia ,aaaamin aaaamin[emoji120]

"Never give wisdom to unworthy because it's unfair to the knowledgeable".

#SiempreJMT[emoji120]

#TanzaniaIdumuDahari[emoji120]
 
Sema Lissu usiogope sema,yapotezee mazombie ya CCM
Alitokea mtu mmoja mwerevu sana....haogopi kusema CHOCHOTE ,LOLOTE,MBELE YA YEYOTE....kwa elimu yake kubwa aliyokuwa nayo hatukujua kuwa kumbe alikuwa ni CHIZI........wa kutibiwa kabisa na dawa za wataalamu wa "PSYCHIATRY AND ABNORMAL PSYCHOLOGY".....

#SiempreJMT[emoji120]
 
Pamoja na kukubaliana nawe kuwepo kwa 'moderation' katika uwasilishaji wa habari/taarifa ili kutoonekana kubomoa zaidi kuliko kujenga kwa pamoja, nchi hii sasa imefikia mahali pa hovyo sana kutokana na kurembaremba na kupeana sifa zisizostahili mara nyingi, hasa kwa viongozi. 'Bruntness' na lugha ngumu, hata kama haipendezi kuisema, lakini ikiwa ndio ukweli ni sahihi kabisa sasa kusemwa hivyohivyo.

Kiongozi anaposhindwa kusema ukweli kwa kutumia lugha anayofikiri itawaudhi hao wanaosemwa, na badala yake analembalemba tu, kwa mfano :"kwani watazikwa na hizo mali wakifa"?; badala ya kuwa 'direct' kwamba wote watashughulikiwa kwa mjibu wa sheria; namna hii ya uwasilishaji ndiyo inayozidi kulemaza nchi.
 
Ninapoona watu kama huyu aliyeweka mada hapa ndio wakiwa mbele zaidi kulalama juu ya anayosema Lissu, ninaanza kuamini Lissu yupo sahihi kabisa..

Ukitazama mada nyingi zilizoanzishwa zikilalama juu yake, utaona karibu wote ni watu wa huko huko CCM. Wanachohofia ni kuwa Lissu anakata kamba iliyomfunga Mbowe wakati wa maridhiano.
 
Lisu anakataa kukata miuno Kwa sababu DJ kashazima muziki.
 
Rais Mama Samia alivyo mtu wa hiyana,

Hivi pascal unajua maana ya neno "hiyana"-- au umeandika tu bila kujua??

na mhafidhina Mkuu ni Tundu Lissu! Mama akafuata hadi Ubelgiji

Unayo hakika kwamba Mama alimfuata Lissu Ubelgiji au mama alikuwa na mambo mengine ya kiserikali huko ndipo akaona/akaombwa akutane na Lissu??

je Lissu ni asset kwa Chadema, or kwa sasa, Tundu Lissu is liability?

Kumbuka Pascal Lissu ni Universal man, ni universal public figure, watu wa caliber yake huwa ni watu kwa ajili ya maslahi wa binadamu wenzao, yeye, nawezasema ni kama Martin luther, Nyerere, Nkrumah,Mandela nk, ambao roho zao zimeumbwa kupigania wengine, kama angaliishi katika zama za kupigania uhuru basi tungemuita mpigania uhuru.

Leo katika nchi yetu Uhuru wetu ni katiba mpya, tumekosa katiba mpya hivyo Lissu mara zote anajaribu kuhamasisha umma juu ya faida za kupata katiba mpya na huku akitoa mifano hai na madhara ya kutokuwa na katiba mpya akioanisha na katiba hii tuliyonayo.

Ninachoweza kusema Lissu ni universal asset si tu kwa nchi yetu bali kwa Africa na dunia yote Muangalie Lissu in that big picture and not through a pin hole camera.

Na kwa mtazamo wangu wa kibinadamu naona anatosha kuwa kiongozi, japo Mungu ndiye ajuaye zaidi.
 
Lissu hajawahi kuwa mwanasiasa
Siku zote ni mwanaharakati...

Nna wasiwasi soon Lissu na Dk Slaa watakuwa kitu kimoja...
 
Lissu hajawahi kuwa mwanasiasa
Siku zote ni mwanaharakati...

Nna wasiwasi soon Lissu na Dk Slaa watakuwa kitu kimoja...


Acha kabisaaaa!!!, unawezaje kumfanisha Lissu na ile takataka "Mwanaharakati" huru 😏😏
 
Mazuri kama aliyoanisha CAG mijitu myeusi mmekuwa HASARA ya DUNIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…