Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Inabidi wampuize kwa kuwa wanaelewa tu uchungu alio nao kwa majeraha aliyopata hawezi kuwa sawa, ni watu wa aina ya Mdude Nyangali, Suzan Kiwanga ndio wafuasi wa sera za Lissu. Wana vitu vinawauma
Mawazo ya mlemavu wa akili haya
 
Naona umechagua upande wa wanaa Tena wenye njaa ya kufa mtu! Kusoma na mtu Haina maana unamjua Sana kiundani kwani chuo kikuu alikoenda kujiongeza na huenda ndiko kulikombadili kifkra na kimtazamo hukuwa naye!
Na hata huko mtaani na kwenye majukumu yake ya uwakili huenda kilimfundisha zaidi jinsi ya kureason na kuargue kulingana na mazingira anayokuwepo hivyo Inakunyima alama za kusema unamfahamu!
Ni kwanini umsemee Jambo ambalo naye amejiinclude na kumchomesha kwa jamii kuwa anaropoka?
Tabia nyingine Zina umri wa kizimudu na kuzifurahia lakini kwa umri wako na taaluma yako hukutakiwa kuchonganisha watu na kumsagia kunguni Lissu.
Nakushauri tu kiutuuzima kuwa kabla hujaandika humu, angalia mvi zako kwenye kioo na Kisha ujiambie mwenyewe kuwa, " Mimi ni mtu mzima mwenye kutakiwa kuwa na busara na hekima"!
 
MKuu umemuua mwenzio balaa.
Kila mara Pascal akisema mada yake ni ya kizalendo na maslahi mapana ya taifa ujue kumkandia mtu na kumharibia.
Kwa hali hii hawezi kufika anakolenga
 

Ndugu yangu, idadi ya vilaza nchini wanaomilki vyeti ndio tishio kuu kwa hatma ya taifa letu. Bahati mbaya zaidi ni vilaza hawa kupewa hifadhi ndani ya chama kikongwe kilichozeeka!

Sijui safari hii wana mpango gani na shujaa Mh. Lissu baada ya jaribio lao la awali kutofanikiwa. Kuwa na akili katika kambi ya vilaza, ni jambo la hatari kweli kweli!

Kwa mtu kama mtoa mada, aliyoandika humu hayanishangazi zaidi ya kunikumbusha yalowapata wengi huko nyuma…give a dog a bad name and hang him!

Mtu kama Pascal Mayalla hana uwezo wa kuelewa anachosema Lissu.

Je hizo kampeni zimeanza tena?
 
Lisu ni mgonjwa wa akili siku nyingi, bahati mbaya sana nyumbu wanachelewa kulijua hili.
Wenyewe wanamsifia kuwa ni mwanasheria msomi na msema kweli ila wengine tulishaona Lissu hayupo sawa, sasa wao ndio wanagundua leo kuwa Lissu ni mropokaji na ana mihemuko.
 
Hata kwenye hayo mengine, kama ameongea na viongozi wenzake chamani akapata baraka ya kuropoka nje, kwangu haina shida, lakini kama ndio ameamua kujiropokea tu tofauti na msimamo wa chama chake, hapo shida ipo..
Hii lugha unayotumia hapa inaonyesha una jambo na huyo bwana. Hilo ni lako na yeye.

Lakini kiujumla, acha Lissu atumie lugha anayodhani anaeleweka nayo, hata kama itaonekana ni "kuropoka" kwa baadhi ya watu.
 
Kweli nimeanini Paskali umebadilika sana. Umekuwa mwoga kuliko Kunguru. Paskali wa 'Kiti Moto' angekula sahani moja na Shujaa Tundu Antipas Lissu. Ukombozi wa Taifa hili unamhitaji sana Tundu Lissu. Na Paschal Mayala wa 'Kiti Moto'. Bwana Paskali, kwa kuwa ulitishwa ukatishika sana, jizuie kutangaza na kueneza woga wako. Haulipi wala hauwezi kukupa uDC. Hizo zama zilishapita.
 
Lissu yupo makini sana. Ni Punguani pekee anayeweza amini maridhiano uchwara. Mwenyekiti wa saccos asali aliyoilamba itamtokea puani.
 
Wenyewe wanamsifia kuwa ni mwanasheria msomi na msema kweli ila wengine tulishaona Lissu hayupo sawa, sasa wao ndio wanagundua leo kuwa Lissu ni mropokaji na ana mihemuko.
Tatizo sukuma Gang mna chuki binafsi na Lissu kama alivyokuwa bwana wenu dikteta uchwara lililopo motoni.
 
Mkuu Lissu ni project za mataifa za magharibi ambao hawataki kuona stability ya nchi hii. Sasa maridhiano yakipatikana Lissu atakuwa amekosa kazi. Tanzania ni nchi pekee kwenye ukanda huu yenye amani tumeona siasa za majirani zetu Kenya zinavyozidi kuigawa nchi hiyo. Ni vizuri kwa Chadema kumthibiti Lissu kwa haraka sana kama anataka akaanzishe chama chake cha siasa kali. Kama unakumbukumbu huyu Lissu alijaribu kwa kiasi kikubwa kujaribu kivunja Muungano na hata kutoa lugha za kejeli dhidi ya waasisi wa taifa hili.
 
Niko uswahilini huku, hakuna yeyote anayenifahamu ndani ya Chadema, hayupo, tatizo lenu hamuwezi kuambizana ukweli.

Mkiwekewa hoja muwe mnaijibu kama ilivyo, kukimbilia vijisababu vya kitoto kama fulani ni CCM, au sijui kutaka jimbo, ni dalili ya kuzidiwa na kukosa majibu ya hoja husika.

Unaposema CCM wanataka kuwarubuni Chadema unakuwa umetumia kipimo gani kuthibitisha hilo? vipi lugha anayotumia Lissu kwa wenzie chamani, sio tatizo?

Kama ana "concern" kuhusu maridhiano kwanini asiwaambie wenzake mezani, anakimbilia barabarani kutafuta nini kama sio uchizi? punguzeni mahaba yaliyopitiliza kwa huyo jamaa, mnazidi kumuharibu mmekuwa kama walevi wake.

I know how I play my cards, Lissu ni mtovu wa nidhamu kwa wenzake, na chama chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…