love life live life
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 2,584
- 3,051
Huyo ni lecture;
Anasema sub saharan Africa ni row material producers hiyo ni role yake katika uchumi wa dunia.
Sub saharan countries ni muhimu kwa nchi zilizoendelea katika uchumi wake, Na hawataruhusu Sub saharan
ku-escape katika role yake kama row material producers.
Pia ameongelea kuwa uchumi wote na ideology zake ziko designed kuiweka Africa maskin specifically Sub-saharan iwe
Marakani, Ulaya au china hayo ndio malengo makuu.
Na hiyo haimaanishi kuwa africa haina cha kufanya lakini huo ni ukinzani wanaotakiwa kupambana nao.
Amesema Africa iwapo itafanya tofauti na mipango hiyo then uchumi wa mataifa makubwa lazima uanguke, USA haitakubali kitu kama hicho bila mapambano makali.
Kazi kubwa ya wasomi wa mataifa makubwa na taasiis za elimu zao ni kutengeneza ideology ambazo zina washiwishi Waafrica kuendelea kufanya wanayofanya ili waendelee kuwa mikononi mwao na kuwaonyesha kuwa umasikini ni matokeo ya uzembe wao.
Hiyo misaada tunayopewa ni kwa ajiri ya kuzisaidi serikali ziendelee kusafirisha row material bila tatizo.
Hiyo ni short summary unawez kufungua video kwa mengine mengi.