Msikiti wa Majini (Masjid al-Jinn) ni moja ya sehemu za kipekee mjini Makkah

Msikiti wa Majini (Masjid al-Jinn) ni moja ya sehemu za kipekee mjini Makkah

Ngoja nikuchanganye akili tu:Uisilamu ulikuwepo tangu enzi za Nabii Abraham ila uisilamu ulianzishwa karne ya saba.
Unaweza kunipa ushahidi wowote hata wakuokoteza unaoonesha paliwahi kuwepo uislamu kabla ya Muhammad?

Karibu
 
Nimekupa Isaya 14:13-

Nimekupa ya agano jipya pia

Au ndugu yangu unadhani biblia inasomwa robo robo ?
Hiyo isaya inazungumzia mfalme wa babeli sio malaika hiyo ya malaika umeyatoa wapi, na wenye kitabu chao wayahudi wanasema na toka enzi hizo ilikua inazungumzia mfalme wa babeli
 
Mungu haangalii karne ngapi zimepita ili kuleta elimu fulani. Yeye ndiye hufanya atakalo kwa muda atakao.

Elimu yako imeishia kukuaminisha kuwa kila jini ni pepo chafu basi ishia kuamini hivyo, ila sisi wengine tumepewa elimu ktk Quran tukufu kuwa wapo majini waasi na wapo wachamungu.
Kuna swali aliuliza Lwiva

Umewahi kusikia lini Mungu kamtuma Jinni kuleta UJUMBE kwa mwanadamu?
 
Hiyo isaya inazungumzia mfalme wa babeli sio malaika hiyo ya malaika umeyatoa wapi, na wenye kitabu chao wayahudi wanasema na toka enzi hizo ilikua inazungumzia mfalme wa babeli
Sisi ni wakristo ,

Nikuukize ,maswali, lini mfalme wa babeli aliishi juu?

Biblia Kuna Aya au nabii zinaandikwa kwa mafumbo

Soma vzr hizo Sifa hapo ,mfalme wa babel hajawahi kuwa nazo

Agano jipya mitume ndio wamefafanua vzr ,malaika waliasi
 
Lisome vizuri ,linamuhusu Lucifer ,Kuna NITA zipo 5 hapo ,anajiinua kutaka kuwa Mungu

Kwasisi tunaochimba zaidi maandiko, hizo NITA (5) ndio zinazaa kitu kinaitwa SATANIC LAW OF FIVE ,hili ni somo jingine
Acha siasa hilo andiko limetafsiriwa miaka na miaka hata kabla ukristo haupo duniani hayo mambo ya satanic law of five umeyatolea wapi?
 
Acha siasa hilo andiko limetafsiriwa miaka na miaka hata kabla ukristo haupo duniani hayo mambo ya satanic law of five umeyatolea wapi?
Ametafsiri nani?

Mimi nimekupa Aya za mitume ,kwamba nikuamini wewe na sio mitume ?kwamba Hawa nisiwaamini ?

2 Petro 2:4 – “Kwa maana Mungu hakuwaacha malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije siku ya hukumu.”

Yuda 1:6 – “Na malaika wasioilinda milki yao ya kwanza, bali waliliacha makao yao wenyewe, amewaweka katika vifungo vya milele, chini ya giza, hata ije siku ya hukumu kuu
.”

Hapo ndio ilivyo biblia haipingani Agano jipya na kale ni tafsiri sawa
 
Ndugu zangu wakristo hakuna andiko katika agano la kale linalosema kuna malaika kaasi Kawa shetani, malaika ni viumbe watakatifu na watiifu kwa Mungu hawatakuja kuasi kamwe.

Kama Kuna mwenye andiko hilo alete hapa tujadili mambo ya kudanganya yamepitwa na wakati


Mwanzo 6:1–4 (SUV)

1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi, na wana wa kike walizaliwa kwao,
2 wana wa Mungu wakawaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wowote waliowachagua.
3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni mwenye mwili; siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baadaye, baada ya wana wa Mungu kuingia kwa binti za wanadamu, wakazalia wana; hao ndio waliokuwa hodari, watu wenye sifa zamani.

Wana wa Mungu
hapa wanaeleweka na wengi kuwa ni malaika waliokuja duniani, wakaingia kwa wanawake wa kibinadamu, wakazaa watoto waliokuja kujulikana kama Wanefili (Nephilim)
watu warefu na hodari.

Hili ndilo tukio lililosababisha kuharibika kwa kizazi cha wanadamu na hatimaye Mungu kuleta gharika enzi za Nuhu

Walifanya uasi
 
Msikiti wa Majini (Masjid al-Jinn) ni moja ya sehemu za kipekee mjini Makkah.

Mzee wangu alienda mwaka Jana kufanya hijja , nilimuuliza akasema huo MSIKITI ni kweli una matukio na VITUKO vya majini , kila siku Namuombea Mzee wangu kabla hajalala mauti atoke huko .
View attachment 3465077Nimeona Leo niwajuze kuhusu huu MSIKITI ambao unaitwa Masjid Al jinn, Ingawa si miongoni mwa misikiti mikubwa, ila unatambulika sana kwa sababu ya tukio la kihistoria lililotokea hapo, ambapo Muhammad alikutana na kundi la majini waliomsikiliza akisoma Qur’ani, kisha wakaamini akawasilimisha.
Tukio hili limeelezwa ndani ya Qur’ani, katika Sura ya Al-Jinn (72).
View attachment 3465064

Qur’ani inasema wazi kuhusu majini walimsikiliza Muhammad wakaikubali Quran na kundi hilo la majini likasilimu.

(Qur’ani 46:29).

Hadith pia zinasimulia kuwa Mtume alisoma Qur’ani na majini wakakubali Uislamu.

Tukio hili ndilo lililoufanya msikiti huu kuwa maarufu sana,

Msikiti huu ulijulikana tangu karne ya 7 kutokana na tukio hilo la muhamad kuyasilimisha majini, lakini ujenzi wake rasmi ulifanywa karne nyingi baadaye chini ya utawala wa Waislamu wa Hijaz.

Baadaye Serikali ya Saudi Arabia iliuendeleza ili kuhifadhi kumbukumbu hii ya kihistoria.


📌 Kwa nini Unaitwa Msikiti wa Majini?

Unaitwa hivyo kwa sababu ya tukio la kihistoria ambapo majini walimsikiliza Muhammad akihutubu na kusoma Qur’ani usiku.

Baada ya kuisikia, waliamini na wakaahidi kuwaonya majini wenzao.

Tukio hili liliweka wazi kwamba Qur’ani si kwa waislamu pekee bali pia ni ujumbe kwa majini yaliyofukuzwa mbinguni .

📌 Visa vya Watu Wanaoingia Msikitini

Kuna simulizi nyingi kutoka kwa mahujaji na wageni

Wengi wanasema walisikia sauti za Qur’ani bila kuona mtu.

Wengine walihisi kama wako katikati ya kundi kubwa la watu, kumbe msikiti uko mtupu.

Wengine waliona mwanga wa ajabu usiku, kana kwamba ibada inaendelea.
View attachment 3465066


📌 Visa vya Sheikh Hashim Rusaganya

Sheikh Hashim Rusaganya, miongoni mwa masheikh maarufu Tanzania, aliwahi kusimulia visa kadhaa kuhusu Msikiti wa Majini:

Kisa cha Kijana Hujaji
Kuna kijana aliyekwenda kuswali Msikiti wa Majini usiku baada ya kutoka Haram. Alipoingia, alihisi kama msikiti umejaa watu wakiswali pamoja naye. Alisikia sauti nzuri za Qur’ani zikisomwa kwa Sauti ya madaha, Lakini baada ya kuswali na kugeuka nyuma, aliona kuwa yuko peke yake msikitini.
View attachment 3465067

Kisa cha Mahujaji Wawili
Mahujaji wawili vijana kutoka Afrika waliingia msikitini usiku. Walihisi kama msikiti umejaa, na waliposwali, waliposoma Qur’ani wakasikia yakijibu “Amin.” Walipomaliza swala na kugeuka nyuma, waligundua kuwa walikuwa peke yao.
View attachment 3465069

Kisa cha Mwanamke Hujaji
Mwanamke mmoja alipotea njiani usiku karibu na msikiti. Alionekana kuongozwa na mwanamke mwenzake hadi karibu na mlango wa msikiti. Alipogeuka kumshukuru hakuwepo tena.

Sheikh Rusaganya alifundisha kwamba alikuwa ni jini kwa ruhusa ya Allah.

Kisa cha Sauti ya Qur’ani
Mtu mmoja aliyelala karibu na msikiti alisikiliza Qur’ani ikisomwa kwa sauti kubwa kana kwamba msikiti umejaa. Lakini alipoamka na kuangalia, aliona kimya kabisa. Sheikh alisema, “Haya ndiyo mambo yanayothibitisha kuwa Msikiti huu bado unatumiwa na majini hadi leo.”
View attachment 3465075


📌 Visa Vingine vya Masheikh wa Tanzania

1. Sheikh Yahya Hussein (Dar es Salaam)
Aliwahi kueleza kuwa Msikiti wa Majini ni ushuhuda wa kwamba ibada haikuwekewa mipaka kwa binadamu pekee. Aliwahi kutaja simulizi za mahujaji waliopata “msaidizi wa ghafla” karibu na msikiti – mtu asiyejulikana aliwaongoza njia au kuwasomea du‘a, kisha akatoweka.


2. Sheikh Othman Maalim (Tanga)
Alisimulia kuwa mahujaji kutoka Tanzania walimwambia walipoingia kuswali Msikiti wa Majini, walihisi kama wameswali kwa “umati mkubwa” hata kama walikuwa wachache.


3. Sheikh Salum Barahiyan (Zanzibar)
Katika mawaidha yake kuhusu masuala ya majini, alitaja Msikiti wa Majini kama alama ya ushahidi wa Qur’ani kuwa majini wapo. Alisema simulizi za watu kusikia sauti za Qur’ani ndani ya msikiti huo si jambo la ajabu, kwa kuwa Qur’ani inasema wazi kuwa majini waliisikia na kuamini.


View attachment 3465076

Swali linakuja ,Kwanini Majini yaliposikia Quran yakaikubali na yakasilimu na kuwa waislamu?

Nimewahi kukutana na Binti mmoja ambaye ni dada wa kazi wa jirani yangu, siku moja wakampeleka kanisani kama mgeni tu ,siunajua wengi Huwa wanawapeleka kanisani wadada wa Kazi,

Mziki ulianza aliporudi ,bint akapagawa na hilo Jini ,lilikuwa linadai halitaki kabisa lipelekwe huko kanisani Tena ,Bali linataka kwenda msikitini tu, yule bint alikuwa anaitwa mariamu, katika kulihoji Jini lililo ndani yake likawa linasema linaitwa Rahma ,

Nikashauri TUFANYE maombi ,bahati mbaya yule dada ambaye ndiye bosi wake ,akaharakisha kumrudisha yule Binti kwao mkoani ,

SWALI NINALOJIULIZA MPAKA KESHO KWANINI MAJINI YALIONA QURAN NA UISLAMU NDIO SAHIHI KWAO ?

Bado nasoma kujua rank za mapepo ,majini kwa UPANDE Wa shetani ,

Yesu aliwahi kuwaambia wanafunzi wake waliposhindwa kumtoa Pepo ,alisema kwa aina hii halitoki labda ufunge au maombi , it means kwamba Kuna Pepo au Jini unalifukuza kwa kukemea tu, ila Kuna aina (kinds) inahitaji njia zaidi, ...ukisoma Mathayo 17:21

Matthew 17:21 KJV
[21] Howbeit this kind goeth not out but by prayer and fasting.
Wewe jamaa bure kabisa
 
Ametafsiri nani?

Mimi nimekupa Aya za mitume ,kwamba nikuamini wewe na sio mitume ?kwamba Hawa nisiwaamini ?

2 Petro 2:4 – “Kwa maana Mungu hakuwaacha malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije siku ya hukumu.”

Yuda 1:6 – “Na malaika wasioilinda milki yao ya kwanza, bali waliliacha makao yao wenyewe, amewaweka katika vifungo vya milele, chini ya giza, hata ije siku ya hukumu kuu
.”

Hapo ndio ilivyo biblia haipingani Agano jipya na kale ni tafsiri sawa
MKuu agano la kale tafsiri ya Aya ya isaya inazungumzia mfalme wa babeli sasa haya unayoleta ww nikulazmisha vitu.

Mm nakuuliza hiyo tafsiri ya malaika kuasi kwenye isaya ni kwamujibu wa nani wayahudi wenye maandiko yao au wakristo?

Ukiwa Kwa mujibu wa wayahudi basi ntakubaliana naww na ikiwa kwa mujibu wa wakristo ntakubaliana naww pia.

Kua tu specific acha kukwepa hoja
 
"Mathayo 25:41
[41]Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake"
Mm agano jipya sijawah tumia kama reference Hasa katika maneno ambayo sio ya YESU mwenyw tuishie hapa.

Kama unaandiko linalosapot hoja Yako kutoka kwenye agano la kale weka hapa kama huna kwaher
 
Hiyo isaya inazungumzia mfalme wa babeli sio malaika hiyo ya malaika umeyatoa wapi, na wenye kitabu chao wayahudi wanasema na toka enzi hizo ilikua inazungumzia mfalme wa babeli
Lini Mfalme wa Babeli “alikuwa juu” kama andiko linavyosema, na ni wapi maandiko yanathibitisha kwamba alianguka mbinguni?

Je, Mfalme wa Babeli anaweza kweli “kupanda mbinguni” au kuishi katika kiti cha enzi cha mbinguni, au hili ni maneno ya kifalme/kishairi?

Andiko linaposema “nyota ya asubuhi, mwana wa alfajiri”, je, hili ni jina la kifalme la kibinadamu au jina la kiumbe wa kiroho?

Ni kwa nini maandiko yanatumia maneno ya kifalme kama kupanda, kushuka, kiti cha enzi, ambayo kwa ufahamu wa kifalme ni metaphor, si
literal?
 
Mm agano jipya sijawah tumia kama reference Hasa katika maneno ambayo sio ya YESU mwenyw tuishie hapa.

Kama unaandiko linalosapot hoja Yako kutoka kwenye agano la kale weka hapa kama huna kwaher
Kumbe upo hapa unachagua maandiko ?
 
MKuu agano la kale tafsiri ya Aya ya isaya inazungumzia mfalme wa babeli sasa haya unayoleta ww nikulazmisha vitu.

Mm nakuuliza hiyo tafsiri ya malaika kuasi kwenye isaya ni kwamujibu wa nani wayahudi wenye maandiko yao au wakristo?

Ukiwa Kwa mujibu wa wayahudi basi ntakubaliana naww na ikiwa kwa mujibu wa wakristo ntakubaliana naww pia.

Kua tu specific acha kukwepa hoja
Mbona nimekupa Aya ya Petro na Yuda hao ni wayahudi pia

Ndio maana nikauliza haya maswali ,labda utaelewa hapo ni lugha ya fumbo tu ,

Lini Mfalme wa Babeli “alikuwa juu” kama andiko linavyosema, na ni wapi maandiko yanathibitisha kwamba alianguka mbinguni?

Je, Mfalme wa Babeli anaweza kweli “kupanda mbinguni” au kuishi katika kiti cha enzi cha mbinguni, au hili ni maneno ya kifalme/kishairi?

Andiko linaposema “nyota ya asubuhi, mwana wa alfajiri”, je, hili ni jina la kifalme la kibinadamu au jina la kiumbe wa kiroho?

Ni kwa nini maandiko yanatumia maneno ya kifalme kama kupanda, kushuka, kiti cha enzi, ambayo kwa ufahamu wa kifalme ni metaphor, siliteral?
 
Back
Top Bottom