Msikiti wa Majini (Masjid al-Jinn) ni moja ya sehemu za kipekee mjini Makkah

Ngoja nikuchanganye akili tu:Uisilamu ulikuwepo tangu enzi za Nabii Abraham ila uisilamu ulianzishwa karne ya saba.
Unaweza kunipa ushahidi wowote hata wakuokoteza unaoonesha paliwahi kuwepo uislamu kabla ya Muhammad?

Karibu
 
Nimekupa Isaya 14:13-

Nimekupa ya agano jipya pia

Au ndugu yangu unadhani biblia inasomwa robo robo ?
Hiyo isaya inazungumzia mfalme wa babeli sio malaika hiyo ya malaika umeyatoa wapi, na wenye kitabu chao wayahudi wanasema na toka enzi hizo ilikua inazungumzia mfalme wa babeli
 
Kuna swali aliuliza Lwiva

Umewahi kusikia lini Mungu kamtuma Jinni kuleta UJUMBE kwa mwanadamu?
 
Hiyo isaya inazungumzia mfalme wa babeli sio malaika hiyo ya malaika umeyatoa wapi, na wenye kitabu chao wayahudi wanasema na toka enzi hizo ilikua inazungumzia mfalme wa babeli
Sisi ni wakristo ,

Nikuukize ,maswali, lini mfalme wa babeli aliishi juu?

Biblia Kuna Aya au nabii zinaandikwa kwa mafumbo

Soma vzr hizo Sifa hapo ,mfalme wa babel hajawahi kuwa nazo

Agano jipya mitume ndio wamefafanua vzr ,malaika waliasi
 
Lisome vizuri ,linamuhusu Lucifer ,Kuna NITA zipo 5 hapo ,anajiinua kutaka kuwa Mungu

Kwasisi tunaochimba zaidi maandiko, hizo NITA (5) ndio zinazaa kitu kinaitwa SATANIC LAW OF FIVE ,hili ni somo jingine
Acha siasa hilo andiko limetafsiriwa miaka na miaka hata kabla ukristo haupo duniani hayo mambo ya satanic law of five umeyatolea wapi?
 
Acha siasa hilo andiko limetafsiriwa miaka na miaka hata kabla ukristo haupo duniani hayo mambo ya satanic law of five umeyatolea wapi?
Ametafsiri nani?

Mimi nimekupa Aya za mitume ,kwamba nikuamini wewe na sio mitume ?kwamba Hawa nisiwaamini ?

2 Petro 2:4 – “Kwa maana Mungu hakuwaacha malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije siku ya hukumu.”

Yuda 1:6 – “Na malaika wasioilinda milki yao ya kwanza, bali waliliacha makao yao wenyewe, amewaweka katika vifungo vya milele, chini ya giza, hata ije siku ya hukumu kuu
.”

Hapo ndio ilivyo biblia haipingani Agano jipya na kale ni tafsiri sawa
 


Mwanzo 6:1–4 (SUV)


Wana wa Mungu
hapa wanaeleweka na wengi kuwa ni malaika waliokuja duniani, wakaingia kwa wanawake wa kibinadamu, wakazaa watoto waliokuja kujulikana kama Wanefili (Nephilim)
watu warefu na hodari.

Hili ndilo tukio lililosababisha kuharibika kwa kizazi cha wanadamu na hatimaye Mungu kuleta gharika enzi za Nuhu

Walifanya uasi
 
Wewe jamaa bure kabisa
 
MKuu agano la kale tafsiri ya Aya ya isaya inazungumzia mfalme wa babeli sasa haya unayoleta ww nikulazmisha vitu.

Mm nakuuliza hiyo tafsiri ya malaika kuasi kwenye isaya ni kwamujibu wa nani wayahudi wenye maandiko yao au wakristo?

Ukiwa Kwa mujibu wa wayahudi basi ntakubaliana naww na ikiwa kwa mujibu wa wakristo ntakubaliana naww pia.

Kua tu specific acha kukwepa hoja
 
"Mathayo 25:41
[41]Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake"
Mm agano jipya sijawah tumia kama reference Hasa katika maneno ambayo sio ya YESU mwenyw tuishie hapa.

Kama unaandiko linalosapot hoja Yako kutoka kwenye agano la kale weka hapa kama huna kwaher
 
Hiyo isaya inazungumzia mfalme wa babeli sio malaika hiyo ya malaika umeyatoa wapi, na wenye kitabu chao wayahudi wanasema na toka enzi hizo ilikua inazungumzia mfalme wa babeli
Lini Mfalme wa Babeli “alikuwa juu” kama andiko linavyosema, na ni wapi maandiko yanathibitisha kwamba alianguka mbinguni?

Je, Mfalme wa Babeli anaweza kweli “kupanda mbinguni” au kuishi katika kiti cha enzi cha mbinguni, au hili ni maneno ya kifalme/kishairi?

Andiko linaposema “nyota ya asubuhi, mwana wa alfajiri”, je, hili ni jina la kifalme la kibinadamu au jina la kiumbe wa kiroho?

Ni kwa nini maandiko yanatumia maneno ya kifalme kama kupanda, kushuka, kiti cha enzi, ambayo kwa ufahamu wa kifalme ni metaphor, si
literal?
 
Mm agano jipya sijawah tumia kama reference Hasa katika maneno ambayo sio ya YESU mwenyw tuishie hapa.

Kama unaandiko linalosapot hoja Yako kutoka kwenye agano la kale weka hapa kama huna kwaher
Kumbe upo hapa unachagua maandiko ?
 
Mbona nimekupa Aya ya Petro na Yuda hao ni wayahudi pia

Ndio maana nikauliza haya maswali ,labda utaelewa hapo ni lugha ya fumbo tu ,

Lini Mfalme wa Babeli “alikuwa juu” kama andiko linavyosema, na ni wapi maandiko yanathibitisha kwamba alianguka mbinguni?

Je, Mfalme wa Babeli anaweza kweli “kupanda mbinguni” au kuishi katika kiti cha enzi cha mbinguni, au hili ni maneno ya kifalme/kishairi?

Andiko linaposema “nyota ya asubuhi, mwana wa alfajiri”, je, hili ni jina la kifalme la kibinadamu au jina la kiumbe wa kiroho?

Ni kwa nini maandiko yanatumia maneno ya kifalme kama kupanda, kushuka, kiti cha enzi, ambayo kwa ufahamu wa kifalme ni metaphor, siliteral?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…