Uchaguzi 2020 Msimamizi wa Uchaguzi awanyima fomu CHADEMA Jimbo la Kibamba, adai fomu yao imeshachukuliwa

Hapo ukisema Chadema wasubiri mpaka arudishe form watakuwa wanajidanganya kamwe hatorudisha na hapo ndio lengo la Msimamizi na Mgembea wa CCM litakuwa limefanikiwa,Yaani msimamizi wa uchaguzi yeye akipelekewa barua tu anakubali pasipo hata kujiridhisha kama aliyekuja ni mtu sahihi au lah.

Hizi issue aambiwe Tundu lissu tu ndio dawa yake atatoa ufafanuzi kitu gani kifanyike.
 
Video imesambaa lazima sana Lazima ataiona tu
 
Yale yale ya uchaguzi wa serekali za mitaa....
 

Huu ni uzembe wa hali ya juu wa tume ya uchaguzi unaopelekea unyanyasai wa kisiasa.

Inakuwaje wewe unadai umetoa form kwa mtu asiyejulikana halafu unadai watu ambao hawakumwona wala kushuhudia tukio hilo wakamtafute badala ya wewe uliyefanya naye hiyo transaction?

Na kwa nini anakataa kuwapa hata barua ya utambulisho aliiyotumia kumtambua huyo mgushi?

Ina maana sheria imeegemea upande mmoja tu kwamba makosa yote yanayotokea katika mchakato ni ya mlalamikaji na kwamba wafanyakazi wa tume ni malaika ambao hawawezi kufanya makosa?

Kutoa form ya pili kwa malalamiko kama haya kunagharama gani na kwa nani?

Hapa kuna tatizo.

Hawa watendaji wawe na uwezo wa kutumia akili na utashi wa uaminifu kwa Watanzania.

Ninaomba mamlaka iingilie hili ili CHADEMA wapewe form. Iiwekwe sharti kwamba form zirejeshwe kwa wakati mmoja ili suala limalizike na atakyebainika kughushi ashitakiwe kwa forgery na waliomsaidia washitakiwe kwa conspiracy.

Kwanza inakuwaje tume na kutumia fedha zetu zote zile wanatengeneza forms ambazo hazina hata simu za mawasiliano?

Hivi ni nini hiki?

Hakuna utukufu katika kumtumikia shetani. Maisha haya yanaishia hapa na baada ya kifo ni hukumu.

CCM jiangalieni.
 
Fomu imetolewa kabla ya majina ya wagombea wa Chadema kutangazwa na halmashauri kuu.

Fomu hawajakabidhiwa mkononi iweje kosa liwe la makamanda wa Chadema.
 
Fomu imetolewa kabla ya majina ya wagombea wa Chadema kutangazwa na halmashauri kuu.

Fomu hawajakabidhiwa mkononi iweje kosa liwe la makamanda wa Chadema.

Huu ni upuuzi na ujinga mkubwa ambao hauwezi kukubalika katika utendaji kazi wa ofisi yoyote ya umma. Na hii ndiyo rangi ya ofisi za Serikali zilizonyingi pasipo Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…