Msimamo wa chama cha ACT-Tanzania na katiba mpya

Mchambuzi,

Asante sana.Na Kitila Mkumbo, alikua ndani ya kamati kuu ya CHADEMA maoni yaliyopelekwa Tume anayajua na pia ndio yalikua msingi wa maandiko yake kwenye makala.

Hata maoni ya mkwamo wa bunge la katiba Lissu alizungumzia na Dr.Slaa alishawi kutoa msimamo kuwa hakuna haja ya haraka ya katiba mpya na kama haiwezekani iliyopo ifanyiwe marekebisho.

Mara kadhaa ndugu Zitto amekua akikebehi msimamo huu kwenye page yake ya Facebook.

Sasa leo wanakuja na summary zile zile kama vile ni maoni mapya tena yanayopingana na misimamo yao kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Mbona hata nyie mtindo wa kujilipua mnacopy kwenye mataifa mengine?

Hivi ule uongo wa Lissu na wale madiwani ni mpya?

Kuna tatizo gani mtu akiona jambo zuri akalisema tena? Acha chuki kijana hakuna jipya chini ya jua!
 
Mwl,''kudhaa'' ndio kufanyaje?
Mchakato utadhaa......... !
 
Wamechukua Maoni ya CHADEMA kwa tume ya Katiba na pia maoni juu ya mchakato wa Bunge Maalumu la Katiba.

Huu ushabiki wa Simba na Yanga kwa vyama vya siasa ndio unaofanya hivi vyama kuwa tatizo badala ya solution....

Hivi kuna ubaya gani wa Chama au Taasisi nyingine kuwa na Maoni au msimamo sawa na chama fulani (in this case chadema)
 
Mbona hata nyie mtindo wa kujilipua mnacopy kwenye mataifa mengine?

Hivi ule uongo wa Lissu na wale madiwani ni mpya?

Kuna tatizo gani mtu akiona jambo zuri akalisema tena? Acha chuki kijana hakuna jipya chini ya jua!

Sasa mkuu huoni ni utapeli kwa jinsi headline/title ya thread ilivyokaa?Watasemaje ni maoni ya ACT -Tanzania ?

Headline ilipaswa kuwa ACT-Tanzania yaunga Mkono msimamo na maoni ya CHADEMA
 
Maridhiano ni pamoja na kukubali kupoteza sasa nyie mnataka ushindi na hamtaki kusiikiliza wengine Mnataka nyie ndio msikilizwe tuu!

Sasa Act wameshauri mwende kwenye Maridhiano lakini wewe uoni Kama ni jipya maana umekariri Kuwa maridhiano ni kukubaliwa Hoja zako kumbe hata kukubali hoja za wengine!
 
Last edited by a moderator:
Huu ushabiki wa Simba na Yanga kwa vyama vya siasa ndio unaofanya hivi vyama kuwa tatizo badala ya solution....

Hivi kuna ubaya gani wa Chama au Taasisi nyingine kuwa na Maoni au msimamo sawa na chama fulani (in this case chadema)

Jaribio la kutaka kuaminisha watu kuwa huo ni msimamo wao huku wakipingana kivitendo na waliotoa msimamo huo ni utapeli wa kisiasa na kijamii.Tena unaweka signature chini kuwa umetolewa na katibu mkuu wa ACT wakati hayo ni maoni ambayo yalishatolewa huoni kuwa kuna athari juu ya matumizi ya raslimali muda na fedha kwa jamii?
 
Umeshawahi kuona ccm ikawa na wazo jipya? Sana sana ni kuteka hoja za CDM na kuzifanya zakwao na ndiyo maana wanaishia kuumbuka kwa kukosa ufahamu juu ya agenda wanazoziteka. Mfano agenda ya Katiba mpya sasa inawaumbua!.

Wameumba ACT kama kitengo cha kutafuta nguvu machoni pa wananchi kwa kutoa matamko yanayofunika aibu zao, kuhamasisha watu kukubaliana na misimamo ya ccm, na kuhujumu upinzani. It is known. Angalia na utaona kuanzia sasa, kila watakapochemka, ACT itakuja na aina fulani ya kurekebisha lakini kwa kuiba ideas za CDM.

Lakini, Democrasia Makini (kama sikosei) ilianzishwa ccm Zanzibar ili kupunguza nguvu ya CUF. Na viongozi walichukuliwa kutoka vyama mbali mbali chini ya ufadhili wa serikali ya ccm lakini mwisho wake uko wapi?

CCM haina namna namna kwa CDM.

Copy and Paste..! Hakuna kitu hapo
 
Viongozi wetu walikua kwenye vikao.Kunahitaji maridhiano gani zaidi ya kujadili Maoni ya Rasimu ya Tume yaliyotolewa na Wananchi?Maridhiano ya kukubali kupunguza People's Sovereignity katika utungaji wa katiba ni hujuma kwa Taifa na watu wake
 
Sasa mkuu huoni ni utapeli kwa jinsi headline/title ya thread ilivyokaa?Watasemaje ni maoni ya ACT -Tanzania ?

Headline ilipaswa kuwa ACT-Tanzania yaunga Mkono msimamo na maoni ya CHADEMA
hawajaunga mkono kila jambo na hoja zenu wasome utaona!

Nyie hamtaki Maridhiano bali mnahitaji ushindi wao wana washauri mwende kwenye maridhiano na maana yake muwe tayari kupoteza na kupata. Tatizo la chadema ni ujuaji mwingi!
 
Wamechukua Maoni ya CHADEMA kwa tume ya Katiba na pia maoni juu ya mchakato wa Bunge Maalumu la Katiba.

Mbona haya haya ndiyo aliyoyaandika Zitto kwenye wall yake ya FB? Hiki chama kina uhusiano gani na MM2?
 
ACT ni kati ya wale Prof. Kabudi anawaita walioshupaa

Hamna mpya zaidi ya kuripoti na kuwa centre,chagueni upande
 
Viongozi wetu walikua kwenye vikao.Kunahitaji maridhiano gani zaidi ya kujadili Maoni ya Rasimu ya Tume yaliyotolewa na Wananchi?Maridhiano ya kukubali kupunguza People's Sovereignity katika utungaji wa katiba ni hujuma kwa Taifa na watu wake
Kinacho jadiliwa ni maoni ya wananchi kutoka kwenye Rasimu na hata kabla ya nyie kususa wote mlikuwa mnajadili hayo hayo maoni na hata leo ndio yanayo jadiliwa na kuchambuliwa! Au kabla ya nyie kutoka mlikuwa mnajadili nini bungeni na kwenye kamati!

Umeona Rasimu mpya pale!
 
hawajaunga mkono kila jambo na hoja zenu wasome utaona!

Nyie hamtaki Maridhiano bali mnahitaji ushindi wao wana washauri mwende kwenye maridhiano na maana yake muwe tayari kupoteza na kupata. Tatizo la chadema ni ujuaji mwingi!

Kwamba tukubali rasimu nyingine ijadiliwe bungeni?Kama hayo ndio maridhiano basi maridhiano ni adui wa haki ,demokrasia na ni adui wa katiba ya wananchi
 
ACT Wanatafuta Kiki tu. Kijiwe cha wasaliti hufuata upepo tu wa kusaka umaarufu.
Ova.
 
Tumia akili yako kujenga hoja sio ubishi usio na msingi.
 
Hizi ni sera na misimamo ya zito ubinafsi, eti kushusha umri wa mgombea urais na na mgombea binafsi ili zito agombee urais. Tumewashutukia. Hamna pakutokea hapo mmekwisha
 
Sasa mkuu huoni ni utapeli kwa jinsi headline/title ya thread ilivyokaa?Watasemaje ni maoni ya ACT -Tanzania ?

Headline ilipaswa kuwa ACT-Tanzania yaunga Mkono msimamo na maoni ya CHADEMA

Taratibu kidogo...

Ni wapi Chadema wameshauri kama hatua ya dharura wakati huu baada ya kuharishwa mchakato wa katiba basi

1. Umri wa mgombea urais ushushwe?

2. Chadema wameshauri wapi mshindi wa urais awe na 50%?hiyo 52% ya Dr Slaa sijui kaiona nchi gani, unless hajui maana ya kuvuka nusu.

3. Chadema wameshauri wapi suala la mafuta na gesi litolewe kwenye masuala ya muungano?

4. Chadema wameshauri wapi mgombea Ubunge aweze kuhama chama bila kupoteza ubunge??

5. Je Chadema na Dr Slaa hapo ameshauri kipengele cha mgombea binafsi kiwekwe SASA??

Kama haya hayapo kwenye taarifa ya Chadema basi hiyo sio copy na kupaste, unless hujui maana ya kucopy na kupaste.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…