Msimamo wa chama cha ACT-Tanzania na katiba mpya

Msimamo wa chama cha ACT-Tanzania na katiba mpya

Sasa A-Ct wameshauri mwende kwenye Maridhiano lakini wewe uoni Kama ni jipya maana umekariri Kuwa maridhiano ni kukubaliwa Hoja zako kumbe hata kukubali hoja za wengine!

Nashangaa na Mchambuzi hajaliona hili.Kutokubaliana na CCM juu ya kuendeleza mchakato wa katiba bila kuridhiana na pande zingine zinazohusika, haimaanishi kuwa unakubaliana na msimamo wa UKAWA.

So far ACT imesimama vizuri, naiangalia kwa karibu.
 
Sijaelewa hapo anaposema anavilaumu vyama vinavyounda ukawa na ccm kwa kushindwa kufikia muafaka.nilitegemea kwamba angewapongeza ukawa kwa kushikilia msimamo wa kutetea maoni ya wananchi.

2. Pia sijamwelewa anaposema vyama vimeacha kujadili maoni yaliyopo mezani na kushikilia misimamo ya kujadili misimamo ya vyama vyao.nilitegemea akitaje chama cha CCM waziwazi kua hakitaki kujadili maoni yaliyopo mezani na kulazimisha yajadiliwe matakwa yao. Sijui kwa nini ameogopa kuilamu CCM waziwazi au ni sababu ya uswahiba uliopo baina ya ACT NA CCM.
 
Taratibu kidogo...

Ni wapi Chadema wameshauri kama hatua ya dharura wakati huu baada ya kuharishwa mchakato wa katiba basi

1. Umri wa mgombea urais ushushwe?

2. Chadema wameshauri wapi mshindi wa urais awe na 50%?hiyo 52% ya Dr Slaa sijui kaiona nchi gani, unless hajui maana ya kuvuka nusu.

3. Chadema wameshauri wapi suala la mafuta na gesi litolewe kwenye masuala ya muungano?

4. Chadema wameshauri wapi mgombea Ubunge aweze kuhama chama bila kupoteza ubunge??

5. Je Chadema na Dr Slaa hapo ameshauri kipengele cha mgombea binafsi kiwekwe SASA??


Kama haya hayapo kwenye taarifa ya Chadema basi hiyo sio copy na kupaste, unless hujui maana ya kucopy na kupaste.

Hayo ni mapendekezo ya CHADEMA kwenda kwenye tume ya katiba na akina Kitila Mkumbo walikua wajumbe wa kamati kuu na hili wanalijua isipokua hapo namba 4. Kitila Mkumbo na Mwigamba waje hapa wakanushe
 
Last edited by a moderator:
Sijaelewa hapo anapo sema anavilaumu vyama vinavyounda ukawa na ccm kwa kushindwa kufikia muafaka.nilitegemea kwamba angewapongeza ukawa kwa kushikilia msimamo wa kutetea maoni ya wananchi.
2.pia sijamwelewa anaposema vyama vimeacha kujadili maoni yaliyopo mezani na kushikilia misimamo ya kujadili misimamo ya vyama vyao.nilitegemea akitaje chama cha ccm waziwazi kua hakitaki kujadili maoni yaliyopo mezani na kulazimisha yajadiliwe matakwa yao.sijui kwa nini ameogopa kuilamu ccm waziwazi au ni sababu ya uswahiba uliopo baina ya ACT NA CCM.

Hiyo ni project ya CCM wanaitekeleza mkuu. Hawawezi kuipongeza CHADEMA. Wanachotaka ni Chadema ikubaliane na masharti ya bunge la katiba kuifumua fumua na kubadili maoni ya wananchi kwenye rasimu. Hawa jamaa sijui wana malengo gani na wananchi
 
Alliance for Change and Transparency-Tanzania Maoni ya ACT-Tanzania kuhusu namna ya kutoka katika mkwamo uliopo katika mchakato wa Katiba Mpya.

1. Nchi yetu iliingia katika mchakato wa Katiba kwa kushirikisha wananchi wote ili kupata Katiba bora yenye kuakisi matakwa ya nchi kwa sasa na baadaye. Ili kupata Katiba bora na inayokubalika na wananchi wengi iwezekanavyo, ni lazima mchakato wa kutunga Katiba uwe wazi, shirikishi na wenye kuzaa mwafaka na maridhiano miongoni mwa makundi mbalimbali ya wananchi

2. Chama cha ACT-Tanzania kinaipongeza sana Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyofanya kazi yake kwa bidii, umakini na weledi mkubwa kwa kuwashirikisha wananchi kwa upana wake na kwa kuzingatia maoni ya wananchi na matakwa ya nchi ya sasa na baadaye katika kuandika Rasimu ya Katiba.

3. Chama cha ACT-Tanzania kilitarajia kwamba Bunge Maalumu la Katiba lingeiga na kuendeleza utamaduni wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kuhakikisha kwamba mwafaka na maridhiano yanapewa nafasi katika kila hatua ya mjadala badala ya kuzingatia misimano ya vyama vya siasa na wingi wa wajumbe wanaounga mkono hoja fulani katika mijadala. Bahati mbaya Bunge Maalumu la Katiba limeshindwa kuzingatia utamaduni wa maridhiano uliojengwa na wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

4. Chama cha ACT-Tanzania kimesikitishwa sana na viongozi wa vyama vya siasa wa CCM na vile vinavyounda kundi la UKAWA kwa kushindwa kwao kupata mwafaka na maridhiano kuhusu muundo wa muungano wa nchi yetu na hata kusababisha kuvurugika kwa mchakato wa Katiba. Ni aibu kwamba mchakato mzima wa Katiba katika Bunge Maalumu umetekwa na sera za vyama vya siasa kuhusu muundo wa serikali ya Muungano badala ya kutafakari na kujadaili Rasimu ya Katiba kwa upana wake na kwa maslahi ya nchi na wananchi kwa ujumla.

5. Chama cha ACT-Tanzania kinasikitika kwamba Bunge Maalumu la Katiba linaendelea na ratiba yake ilihali kundi kubwa la wajumbe likiwa nje ya mchakato. Bila kujali sababu za kundi la UKAWA kuwa nje ya Bunge Maalumu la Katiba, ACT- Tanzania haiamini kwamba mchakato huu utadhaa Katiba bora na yenye kukubalika kwa upana bila makundi yote muhimu kushiriki katika mchakato huu kwa ukamilifu wake mwanzo hadi mwisho. Ni maoni ya ACT-Tanzania kuwa tukiendelea na mchakato kama ulivyo sasa inawezekana tukapata katiba mpya yenye uhalali kisheria. Lakini itakuwa ni katiba isiyo na uhalali wa kisiasa wala kijamii, na kwa maana hiyo itakuwa haina tofauti ya maana na katiba ya sasa na hivyo kuifanya nchi kuingia kwenye hasara kubwa ya fedha za umma.

6. ACT-Tanzania haioni uwezekano wa kupatikana katiba mpya iliyo bora katika kipindi hiki, hasa kwa kuzingatia mkwamo uliomo baada ya wajumbe kujikita katika misimamo ya vyama vyao badala kujadili rasimu ya katiba mpya kwa uhuru, umakini na weledi.

7. Kutokana na mazingira ya mchakato wa Katiba tuliyoeleza hapo juu, ACT-Tanzania inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe mapema iwezekanavyo ili kunusuru mchakato wa Katiba na kurudisha hali ya kuelewana katika jamii yetu:

a. Bunge Maalumu la Katiba lisimamishwe ili kuendelea kutoa fursa ya mazungumzo ya kutafuta mwafaka na maridhiano.

b. Mchakato wa kuandika katiba mpya uahirishwe hadi baada ya uchaguzi mkuu.

c. Katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu, Bunge la Jamhuri ya Muungano lifanye marekebisho katika katiba ya sasa ili kutengeneza mazingira ya uchaguzi ulio huru na haki.

Tunapendekeza marekebisho ya katiba ya sasa katika maeneo kumi (10) yafuatayo:

i) Tume ya Uchaguzi iwe huru na ionekane kuwa huru,

ii) Kuruhusu mgombea binafsi na wabunge ‘kukatisha kapeti’ bila kupoteza ubunge wao ili kudhibiti ubabe wa vyama vya siasa

iii) Kushusha umri wa mgombea urais ili kuwapa vijana haki na fursa ya kugombea katika nafasi hii muhimu, hasa ukizingatia kwamba karibu theluthi mbili (65%) ya wapiga kura wote Tanzania wapo chini wa umri wa miaka 40, na ukweli kwamba takwimu za Tume ya Marekebisho ya Katiba zinaonyesha kuwa wananchi walio wengi (53.7%) waliotoa maoni kuhusu umri wa mgombea urais walitaka umri huo ushushwe.

iv) Kuweka sharti kwamba ili mgombea atangazwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano lazima apate angalau asilimia 50 ya kura zilizo halali.

v) Kuweka msingi wa kikatiba kwamba wagombea Urais lazima wawe na angalau midahalo mitatu katika kipindi cha kampeni.

vi) Kuondoa suala la Mafuta na Gesi katika mambo ya Muungano ili kuruhusu Zanzibar kuendelea na utafutaji wa Mafuta na Gesi asilia kwa uhuru na bila kuingiliwa na Tanzania bara

vii) Kuruhusu Zanzibar kuwa na mahusiano na ushirikiano wa kimataifa (International Cooperation) kwa faida za maendeleo yake.

viii) Kuweka mipaka ya Mashtaka ya Kesi za Rushwa ili kuruhusu TAKUKURU kufanya uchunguzi na kuendesha kesi hususani kwa kesi ufisadi wa mali umma bila kupita kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.

ix) Kuweka msingi wa kisheria wa Tangazo la Mali na Madeni ya Viongozi kuwa wazi kwa Umma na uthibitisho wa uhalali wa mali ambazo mtu anamiliki uwe upande wa mtuhumiwa (reverse of burden of proof).

x) Kuweka msingi wa Kikatiba wa Uhuru wa kupata habari kwa wananchi (Freedom to access information) na kupiga marufuku vyombo vya habari kufungiwa isipokuwa kwa amri ya mahakama.

8 Chama cha ACT-Tanzania kinatoa wito kwa wadau wote wa Katiba kuungana katika kushinikiza mchakato wa Katiba unaoendelea kusimamishwa na kuruhusu mabadiliko hayo machache ya Katiba ya sasa ili kupisha uchaguzi na kuhakikisha Taifa linapata muda wa kutosha wa kuandika Katiba bila shinikizo na katika hali ya utulivu.

8 ACT-Tanzania inawataka mahasimu katika mchakato wa Katiba kutoa fursa kwa majadiliano na kujenga mwafaka na maridhiano ya nchi katika maeneo hayo. Tunasisitiza kwamba tusichoke kuzungumza katika masuala ya nchi yetu kwani mbadala wa mazungumzo ni fujo na upotevu wa amani.

Asanteni kwa kunisikiliza
Ndugu Samson Mwigamba
Katibu Mkuu, ACT-Tanzania.

Kikao hiki mlikaa wapi kama si uzushi! Mwigamba wewe UTADHAA lini?
 
Hayo ni mapendekezo ya CHADEMA kwenda kwenye tume ya katiba na akina Kitila Mkumbo walikua wajumbe wa kamati kuu na hili wanalijua isipokua hapo namba 4. Kitila Mkumbo na Mwigamba waje hapa wakanushe

Kumbuka...mapendekezo haya sio ya katiba mpya...bali ni hatua ya dharura ya kuboresha katiba ya mwaka 1977 wakati mchakato wa katiba mpya ukisimama.

Kama Dr Slaa alivyosema (kwenye hiyo link) kuwa kwa CHADEMA ya dharura kwa sasa ni tume ya uchaguzi na mshindi wa urais kupata 52%...

Ndio maana nimekuuliza kama hiyo ya ACT ni copy na kupaste, je yapo wapi hayo mapendekezo mengine ya ACT ambayo kwa Chadema (kwenye ile link) sio ya dharura kwa sasa?? Kama hayapo basi hiyo haiwezi kuwa kucopy na kupaste.
 
Last edited by a moderator:
Taratibu kidogo...

Ni wapi Chadema wameshauri kama hatua ya dharura wakati huu baada ya kuharishwa mchakato wa katiba basi

1. Umri wa mgombea urais ushushwe?

2. Chadema wameshauri wapi mshindi wa urais awe na 50%?hiyo 52% ya Dr Slaa sijui kaiona nchi gani, unless hajui maana ya kuvuka nusu.

3. Chadema wameshauri wapi suala la mafuta na gesi litolewe kwenye masuala ya muungano?

4. Chadema wameshauri wapi mgombea Ubunge aweze kuhama chama bila kupoteza ubunge??

5. Je Chadema na Dr Slaa hapo ameshauri kipengele cha mgombea binafsi kiwekwe SASA??


Kama haya hayapo kwenye taarifa ya Chadema basi hiyo sio copy na kupaste, unless hujui maana ya kucopy na kupaste.

Msukule wa Zitto kazini. Suala la gesi alitoa pendekezo wakati tunaanzisha CHAUMA.
 
Tumia akili yako kujenga hoja sio ubishi usio na msingi.
 
Atleast Makene angekuwa anaandika vitu vya msingi na kwa mpangilio kama huu angeonekana yupo timamu.

Hongereni ACT.

Mmeonesha tofauti na wale wachaga.
 
ACT ni kile chama chenye watu ambao Prof. Mpalamagamba amewaita Wa.pu.mbavu.
 
Sikubaliani na uhuru wa kukatisha kabeti,ukiwa ubunge wako umedhaminiwa na chama cha siasa basi ubunge wako utakoma pale ambako chama hicho kitakuchanganya uanachama.Hii itasaidia sana kuleta discipline kwenye vyama na kuzuia kuzalisha watu kana zito

Hayo mapendeezo yako ya katiba kongwe ksasa tunataka mawazo mapya kaka. Munge huwa buneni awakishi cam bali uwa anawakilisha wananchi kwahiyo hiyo ridhaa ya kumsimamisha iwekwe kwa wananchi na sio chama.
 
Hayo ni mapendekezo ya CHADEMA kwenda kwenye tume ya katiba na akina Kitila Mkumbo walikua wajumbe wa kamati kuu na hili wanalijua isipokua hapo namba 4. Kitila Mkumbo na Mwigamba waje hapa wakanushe
Watu na akili zao timamu watakuja vip kuzungumza na kichaa mwenye ufukara wa akili na kipato kama wewe??

Eti waje hapa wakanushe...wakanushe nin na ili iweje.

We mchumia tumbo tu na muoshaji wa nepi za junior wa slaa na josephine umsumbue nani.

Pimbi kweli wewe.

Huna kazi tu hadi leo unaendelea kulipiwa pango hapo kinondoni.

Angalia sana vya rahisi hivyo unavyopenda penda.

Mwisho wake ni kutoa huduma.
 
Last edited by a moderator:
Taratibu kidogo...

Ni wapi Chadema wameshauri kama hatua ya dharura wakati huu baada ya kuharishwa mchakato wa katiba basi

1. Umri wa mgombea urais ushushwe?

2. Chadema wameshauri wapi mshindi wa urais awe na 50%?hiyo 52% ya Dr Slaa sijui kaiona nchi gani, unless hajui maana ya kuvuka nusu.

3. Chadema wameshauri wapi suala la mafuta na gesi litolewe kwenye masuala ya muungano?

4. Chadema wameshauri wapi mgombea Ubunge aweze kuhama chama bila kupoteza ubunge??

5. Je Chadema na Dr Slaa hapo ameshauri kipengele cha mgombea binafsi kiwekwe SASA??


Kama haya hayapo kwenye taarifa ya Chadema basi hiyo sio copy na kupaste, unless hujui maana ya kucopy na kupaste.

Huyo mrembo namba 8 ni mwendawazimu tu.

Hawez kushughulisha akili za watu attention seeker na mganga njaa tu.

Zitamuua njaa zake na sio kitu kingine.
 
Huko nyuma Kitila Mkumbo aliandika sana juu ya jinsi gani taifa linahitaji mbadala wa chama kikuu cha upinzani - yani mbadala wa chadema. Katika suala nyeti Kama hili la mchakato wa katiba mpya, ACT kuja na msimamo Kama wa chadema, hasa juu ya kuwa upande wa wananchi, halafu hapo hapo kutounga mkono UKAWA ni kitendo ambacho kinaacha maswali mengi kuliko majibu huku mitaani. Nazungumza Nikiwa kijiweni nikisikiliza mijadala Hapa. Wanasema mengi lakini in a nutshell, ni hayo hapo juu.


Sent from my iPhone using JamiiForums

Kwani kujiunga na ukawa ni lazima??

Wapi imeandikwa kwamba ili uonekane muadilifu ni lazima ujiunge na ukawa.

Watu hawawezi kusimamia haki hadi wajiunge na ukawa?
 
Last edited by a moderator:
Atleast makene angekuwa anaandika vitu vya msingi na kwa mpangilio kama huu angeonekana yupo timamu.

Hongereni ACT.

Mmeonesha tofauti na wale wachaga.

Haya ni mahaba yaliyopitiliza sasa lipi andishi linaloweza kufikia angalau asilimia 10 ya mabandiko ya Makene ktk uzi huu we jamaa..... basi tu

Makene anataaluma ya Uandishi na huyo Mwigamba anataaluma ya Ualimu hivi kwa taaluma zao tu ni nani unaweza kujua kwa haraka anahusika na upangaji wa au uandishi wa hivyo unavyoviita vitu vya msingi?

Halafu huo unaodai utofauti na Uchaga umetokea wapi ktk bandiko hili hivi Makene ni Mchaga kiasi aonyeshe utofauti na Mwigamba ambaye sijui ni Mnyakyusa/Msafwa? Sometimes uwe unaziweka akiri zako mahala sahihi si kila mara kuongea upumbavu umri ushaenda huo hutarudi tena kuwa mtoto ili urekebishe makosa uliyotenda ukiwa kijana

Grow up dude!!!!!!

BACK TANGANYIKA
 
Hiyo ni project ya CCM wanaitekeleza mkuu.Hawawezi kuipongeza CHADEMA.Wanachotaka ni Chadema ikubaliane na masharti ya bunge la katiba kuifumua fumua na kubadili maoni ya wananchi kwenye rasimu.Gawa jamaa sijui wana malengo gani na wananchi

Ben jifunze kuumeza ukweli unapokufikia asiwe kama maccm wanapopewa hoja zilizoenda shule hubaki kuzomea.
chadema kwa sasa mayumbayumb . mwazoni cuf mliwaita mai rukuki na kuwasma ni ccm B na mliahi kuwaita waliberaili lakin leo nimaswahiba wa nguvu.

ACT-Tanzania imetoa hoja za ukweli zimeze tu
 
Back
Top Bottom