Msimamo wa chama cha ACT-Tanzania na katiba mpya

Mbowe anaitwa Mr. Zero kwa sababu alitaga mtihani wa form six. Au wewe hujui? Zitto hawezi kuwa Mr. Zero kwa sababu mwenzio ni msomi na anamalizia PhD.

Huyo ni msomi njaa kama alivyo Mkumbo aliyekuwa akihongwa laki 2 kupitia mpesa kwa mujibu wa ripoti ya mwenendo wa MM.Wasomi wengi wa tz ni wachumia tumbo na wanafiki wakubwa ambao hata usomi wao hauwasaidii kitu.njaa mbaya sana!
 
kwani tatizo lako ni nini hapa hasa. wao kutoa maoni yao? kwani lazima yatofautiane na yenu? unaonekana u-mweupe kichwani.

 
Masikini Imebidi .........Nimepitia maandishi yake ni aibu tupu ana matusi ambayo ni aibu sana ,,,,,,,kweli Imebidi Dr.Kitila Mtumbo .........ona sasa aibu hizi ........usaliti ni dhambi mbaya na lazima utaumbuka .....huyu Imebidi alianza usaliti tangu zama za akina Gervas Mkili .......
 
Masikini Imebidi.........chama cha uwazi hiki .........aibu Dr.Kitila Mtumbo hii.......utajiri cha wapi ?
 
You are just too short sighted. Yaani badala kuangalia hoja unaangalia mtu. Huyu Zitto kwa nini anawatesa hivi? Tunajadili umri wa kugombea tukilenga kukomesha ubaguzi wa umri, wewe unaongelea personality ya Zitto. Mtafute mkanywe naye chai!
Masikini ulidhani umejificha kumbe uko peupe .......aibu sana hii........
 
v) Kuweka msingi wa kikatiba kwamba wagombea Urais lazima wawe na angalau midahalo mitatu katika kipindi cha kampeni.
Yaani katiba it aje idadi ya midahalo ya wagombea Urais kweli ?
 
v) Kuweka msingi wa kikatiba kwamba wagombea Urais lazima wawe na angalau midahalo mitatu katika kipindi cha kampeni.
Yaani katiba it aje idadi ya midahalo ya wagombea Urais kweli ?

Midahalo angalao ingetajwa katika Sheria au kanuni za uchaguzi.
 

Hadi sasa sijui nimjibu nani kati ya hizo ID mbili.
 

Daah...kumbe Imebidi ni Dr Kitila Mkumbo? Mama yangu weeee mtu mzima umejiumbuwa mwenyewe.
 
Matola,njoo umuone IMebidi. Nasubiria comment yako
 
Last edited by a moderator:

Onesha Hati miliki ya Mawazo hayo kiasi cha kujiaminisha ni Haramu mtu mwingine kuwa na Maoni sawa na ya Genge lako.
Kwa hiyo Chadema ikiamini kuwa ni busara Bunge la Katiba kusitishwa basi iwe Haramu mtu au Taasisi nyingine msiyoikubali kuwa na Mawazo hayo?
 
Viongozi wetu walikua kwenye vikao.Kunahitaji maridhiano gani zaidi ya kujadili Maoni ya Rasimu ya Tume yaliyotolewa na Wananchi?Maridhiano ya kukubali kupunguza People's Sovereignity katika utungaji wa katiba ni hujuma kwa Taifa na watu wake

Inamaana hiyo rasimu ya katiba haitakiwi kubadilisha kipengere chochote?

Au kunavipengere unaruhusiwa kuvirekebisha na vingine uruhusiwi?

Je wananchi wakiambiwa waamuwe muundo wa muungano uwe wanamna ipi,kisha wananchi wakapitisha muundo wa serikali mbili mtaikubali hiyo katiba?

Tunaona cdm mnavyo chukizwa na wanachama mnaotofautiana mawazo.mnawaita wasariti.je huoni kuwa nyinyi cdm niwazaifu wakukubali mawazo ya wenzenu wenye mawazo tofauti nanyi.
 
Yaan fikra hizi ndio una exponsure ya kuishi nje ya Tenende....sijui ungekuwa bado kijijini Tenende ungekuwaje?

Nakusamehe bure...

Sikutegemea kama kuna "mjinga mjinga" kama wewe mwenye mawazo kama haya
 
Mbowe anaitwa Mr. Zero kwa sababu alitaga mtihani wa form six. Au wewe hujui? Zitto hawezi kuwa Mr. Zero kwa sababu mwenzio ni msomi na anamalizia PhD.

Imebidi nikuache ujibiwe na muasisi wa ACT:
Inasound vizuri sana "Mr Zero a.k.a Zitto". Mkurugenzi wa SACCOS ya ACT ambayo pia ni nyumba ndogo ya CCM.

 
Kwani kujiunga na ukawa ni lazima??

Wapu imeandikwa kwamba ili uonekane muadilifu ni lazima ujiunge na ukawa.

Watu hawawez kusimamia haki hadi wajiunge na ukawa?

Hoja Hapa sio Kujiunga na ukawa Bali kuunga Mkono msimamo wa ukawa. Ni busara kuacha duplicate resources and efforts Katika suala Zima la kudai katiba itokanayo na wananchi. Tayari vyama vya upinzani vina msimamo wa pamoja juu ya Hilo, sasa ukawa ni upinzani wa wapi, je ni mpinzani wa vyama vya upinzani? Mnachanganya sana wananchi, Kaeni vijiweni msikie mnavyokoroga wananchi.

Msimamo wa ACT sasa unatafsiriwa na wengi Kwamba ni sawa na kuunga Mkono UKAWA. Kinachochanganya na pia kushangaza wananchi Wengi ni je, kwanini ACT wanaendelea kuhangaika kujitofautisha na chadema Katika suala husika Wakati kimsingi Madai ya ukawa (chadema) ni Yale Yale Kama ya ukawa - katiba itokanayo na wananchi hasa Mfumo wa muungano?

Hizi hoja na juhudi za Kitila Mkumbo kutofautisha msimamo wa ACT vis a vis Chadema kwa hoja Kwamba chadema wanapendekeza serikali Tatu Zenye muungano legelege Wakati ACT wanapendekeza serikali Tatu Zenye muungano imara ni hoja ya kitoto sana. Msingi wa hoja Hapa ni muungano wa serikali Tatu, period. Hayo Ndio wamesema wananchi, Hayo mengine juu ya uimara na ulegelege wa muungano wa serikali Tatu ni masuala ya kujadiliwa bungeni, na hiyo Ndio kazi ya BLK - kuboresha rasimu itokanayo na wananchi.

Cc Nguruvi3, Mag3, JokaKuu, Jasusi



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Kitila mkumbo ameclarify hoja yake vizuri kabisa pale juu kuelezea tofauti baina ya muundo..missions...na visions za chadema na act bila shaka kaeleweka.

Hizo spinnings kama mnaamua kuzifanya basi ni juu yenu.

Hata kama unasema hoja ni kuwaunga mkono ukawa ndio nakuuliza kwamba wapi ambapo act ameenda kinyume na ukawa??na kama unasema kwamba chadema is a part of ukawa na huoni kwanin act na chadema watofautiane ili hali woote wanaunga mkono hoja za ukawa ndipo nikuulize sasa...kwani sera za cuf na chadema
..au nccr na cuf...au nccr na chadema zinalandana kwa fact tu kwamba wooote wanaunganishwa na ukawa??

Hao si wameumgamishwa na ukawa kupitia mzozo wa katiba ??

Sasa iweje baadhi waonekane hawana uzalendo eti kisa tu hawajaonekana moja kwa moja kuungana na ukawa.

Wewe unajua fika kwamba chadema wana chuki za waz waz na act...hata kama act inataka kujiunga na ukawa watajiunga vip ili hali tokea kimeanzishwa kinaitwa kibaraka wa ccm??

Tena hawa hawa chadema waliokawa wanaiita cuf ni ccm b ndio hawa hawa leo wameungana nao cuf kusha bila ushahid wowote wanawaita act ni kibaraka wa ccm.

Unawaamini vipi vihiyo kama hao.
 
Last edited by a moderator:
Nimelisoma tamko nakubaki kujiuliza maswali mengi, kama kuna umakini wa aina yoyote.

1. Tamko hili ni mwendelezo wa matamko waliyotoa UKAWA, CCM(Lembeli, Miwgulu) na wazee (Mark Boman), waandishi wa habari na wanajamii.
Hakuna walichokiongelea ACT kigeni zaidi ya kunukuu watu bila acknowledgement.

2. ACT wameorodhesha matatizo ya BMK. ACT hawajaweka wazi tatizo ni nini.
Wame epuka kusema rasimu ya kujadiliwa ni ya Warioba.
Wamekwepa kusema maoni ya tume ili kutowaudhi CCM kwa kujificha.
Hilo ni kuwachanganya watu na wala si kuonyesha njia.

3. Suala la umri si agenda ya ACT. Tumejadiliana jamvini na akina Ben Saanane, MWANAKIjiji, JokaKuu, Jasusi, Mchambuzi , Bongolander, Mag3 n.k. muda mrefu

Tumepingana na akina Ben, leo tunaaminishwa ni jambo geni kabisa eti lina umakini. Mnachokifanya ni kujificha nyuma ya kundi la January na Zitto na agenda yao.

Hatutengenezi katiba ya watu wawili, tunatengeneza katiba ya nchi.


4. Mchambuzi anauliza, iwapo CUF, CDM, NCCR kila mmoja atakuja na madai yanayofanana kuna ulazima wa kufanya hivyo? Nami nauliza, kama ACT wana madai yanayofanana na UKAWA kuna ulazima wa kuja na kitu kile kile.


5. Hoja ya Kitila Mkumbo kuhusu S3 ni mfu.
Kinachojadiliwa ni muundo wa muungano kwanza, ndilo tatizo la kukwama BMK.

Namna gani serikali 3 zitakuwa imara au dhaifu hilo ndilo lipo mbele ya BMK.


Hoja ya msingi ni S3 kwanza. Hayo ya lege lege na imara ni mambo baada ya hoja kuu.Kusema ACT ina hoja imara tusizozijua na tusizozifahamu ni ad hominem

6.
Tamko la ACT lilikusudia kueleza msimamo kuhusu BMK na mtafaruku unaoendelea.
Ukiliangalia ni tamko la jumla na hilo halina tatizo hata kama wanadurusu ya wenzao.


Tatizo ni pale Kitila anapoingia katika mkumbo usiolingana naye.

Kitila, katika tamko la jumla ni aibu kuongelea vipengele visivyohusika
Hili tamko, Dr, ni la kiwango kisicholingana na hadhi yako, nakuthibitishia hapa chini.

Soma kifungu hiki
ACT: ACT-Tanzania: 7. Kutokana na mazingira ya mchakato wa Katiba tuliyoeleza hapo juu, ACT-Tanzania inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe mapema iwezekanavyo ili kunusuru mchakato wa Katiba
Hadi hapa Kitila na ACT, wanatoa mapenekezo haya
v) Kuweka sharti kwamba ili mgombea atangazwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano lazima apate angalau asilimia 50 ya kura zilizo halali.
Anachronism! Tatizo ni kukwama kwa mchakato si vipengele husika. Mumedai mnapendekeza kukwamua mchakato.
Hili lina uhusiano gani na tatizo lililopo?
v) Kuweka msingi wa kikatiba kwamba wagombea Urais lazima wawe na angalau midahalo mitatu katika kipindi cha kampeni.
Irrelevant, tumekwama mchakato hili linahusiana vipi na sehemu ya 7 ya mapedekezo yenu!
vi) Kuondoa suala la Mafuta na Gesi katika mambo ya Muungano ili kuruhusu Zanzibar kuendelea na utafutaji wa Mafuta na Gesi asilia kwa uhuru na bila kuingiliwa na Tanzania bara
Here we go! BMK limejadili kanuni, na muundo ndipo lilipokwama.

Halijajadili kipengele hata kimoja kinachohusu mambo ya muungano.

Wapi mnaona suala la gesi na mafuta ni sehemu ya tatizo tulilo nalo?Hii haina maana yoyote kufuatana na kipengele namba 7 cha tamko lenu. Tamko ni kukwamua mchakato si mafuta na gesi

Lakini pia mumeshindwa kuelewa.
Tume imeorodhesha matatizo mengi kuhusu muungano kwa pande zote.

Katiba tunayotaka kutengeneza si ya mafuta na gesi, na wala si katiba ya zanzibar.
Kuna matatizo ya Tanganyika.

Mnapochagua kipengele na kukifanya sehemu ya kukwamua mchakato, inasikitisha Kitila.

Zaidi ya hapo, gesi na mafuta si mambo ya muungano tena. Zanzibar walishaondoa.

Ningaliwaelewa kama mngeongelea uvunjwaji wa katiba, na si ku-appease wznz kwa cheap politics za kitoto namna hii.
vii) Kuruhusu Zanzibar kuwa na mahusiano na ushirikiano wa kimataifa (International Cooperation) kwa faida za maendeleo yake.
Hakuna uhusiano na kukwama kwa BMK.

Mnachomeka vipengele kufurahisha watu, Kitila anasema ni tamko makini. Real ! This one!

Na mwisho, Kitila, ukiangalia lugha tu inatia shaka kama unapitia na kuhakiki matamko makubwa 'makini'.
Chama cha ACT-Tanzania kinasikitika .......... Bila kujali sababu za kundi la UKAWA....haiamini kwamba mchakato huu utadhaa Katiba bora
Kitila usijeniambia ni typo error!

Ndio maana nakusihi uangalie matamko kama haya, hayalingani na hadhi yako.

Ahsante

 

Ahsante Mkuu Nguruvi3…niko hapa na familia yangu tunakusoma kwa makini sana huku tunapata breakfast.

Haya bwana Kitila Mkumbo njoo ujibu hizi hoja za bwana Nguruvi3…sisi wengine tumebaki kuwa wafuatiliaji wa mtanange huu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…