Msimamo wa chama cha ACT-Tanzania na katiba mpya


Nguruvi3,

Asante sana sana .Yale niliyotarajia kuandika umeniwahi kabisa.

Nakumbuka tulipingana sana kwenye suala la umri na thread zipo na msimamo wangu ukaendelea kubakia ule ule hadi leo

Nimeshangazwa sana idadi ya midahalo eti itajwe kwenye katiba badala ya kuwa suala la kutungiwa sheria au kanuni zitakazoeelekeza tume huru ya uchaguzi iandae midahalo
 
Last edited by a moderator:

Mchambuzi,



Nakubaliana na hoja zako hapo juu
 
Last edited by a moderator:
THE BIG SHOW,
Huko nyuma Katika Bandiko lake la "ACT, mpini wa CCM kumaliza upinzani, Nguruvi3 alijadili Kwamba Zitto na wenzake ambao ni wapinzani wa vyama vya upinzani, mkakati wao ulikuwa ni kuhakikisha Kwamba zitto anaingia ndani ya bunge la katiba Kabla ya kuondoka chadema. Nimeanza kuelewa hoja ya nguruvi3.

Kwa wale waliofuatilia BMK session Ile ya awali, nadhani ilikuwa bayana jinsi gani zitto alikuwa anakwepa kuweka msimamo huku akisoma upepo. Wenzake ambao sasa Wanaunda ukawa, wakaamua to risk kwa Imani Kwamba wanasimama na wananchi. Kina zitto, kitila, na mwigamba walikuwa wapi Katika hatua zile? Kwanini ACT ije na msimamo, tena ule ule miezi Sitta baadae? Jibu ni Kwamba siasa za ACT ni za kusoma upepo, sio siasa za kuwa pre-emptive. Matokeo yake, badala ya kuwa chama mbadala cha upinzani Kama kitila alivyodai Huko nyuma Kwamba taifa linahitaji mbadala wa upinzani, ACT sasa Nina pro - active party, running pro- active strategies.

ACT wanajaribu sana kuwa mbadala wa chadema kwa kuja na vision, mission na strategies tofauti, lakini chama Hiki ambacho kitila alikitabiri Kwamba kitakuja na mikakati ya kisayansi na kuwa UNIQUE, sasa kimeishia kuwa ni HYBRID. Ndani ya BMLK, zitto amefeli Katika kusaidia ACT kuteka agenda ya Katiba mpya, na nje ya bunge, kina kitila wanaendesha mikakati ambayo Kama alivyojadili Nguruvi3 kwa kina, haiendani na hadhi Yake.

Ni muhimu kina kitila waelewe Kwamba huku vijiweni, wananchi wanasema Kwamba "hatimaye zitto aungana na ukawa kudai katiba mpya", ni vizuri kina kitila wakaelewa hoja ya msingi sasa ni utanganyika wao Kama alivyojadili nguruvi3 hapo juu, na suala Hilo ukawa has already covered enough mileage. Mengine raised na ACT, mengi yake mahala pake ni ndani ya bunge la katiba Kama sio Katika Sheria mbalimbali Kama alivyojadili Ben Saanane.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:


Tatizo ni ACT.

Kila napojaribu kuwasoma kwa undani kabisa nakuja kubaini tatizo ni ACT as a political party.

Hamjapenda kuasisiwa kwake....hampendi uwepo wake...pia hamuwapendi waanzilishaji na wanaokisapoti chama hiko.

Ushahid upo wazi kwani hao hao wanaotokea huku kukikosoa na kukikejeli chama hiko ndio hao hao siku zoote wanaojipambanua ktk kuwapinga waasis wa chama hiko kabla ya kuasisiwa kwake na hata mpaka hivi sasa.

Kutofautiana kifikra na misimamo ndiyo demokrasia ilivyo.

Siyo lazima wayawazayo hawa woote yawe ni masuala yanayofanana.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu mpaka sasa naona kwa ujumla tatizo kubwa ni kuwa we are not thinking as Tanzanians. Not yet. Bado naona kuwa tunaeleezwa kujadili mambo tusisyotakiwa kujadili. ACT is just a distraction, the issue ni katiba, na kwanza kabisa ni Muungano na sura ya muungano ambao utakuwa na manufaa kwa wanaounda muungano, sio wenye manufaa kwa CCM.

Kwenye suala la Katiba naona maoni ya watanzania yako wazi. Lakini tatizo ni kuwa uwaze wake unaweza kukosolewa kwa sababu za kisiasa.

Kimsingi naona kama ACT ni kama inarukia jambo ambalo hailiwezi. Kwa maoni yangu ACT imeanzishwa kwa ajili ya njaa tu, na baadhi ya watu ndani ya CCM wanatamuia njaa ya ACT kuibomoa CCM. Lakini inawezekana kabisa kuwa hata njaa yao, haijawafanya wawe vipofu kabisa, hala kwenye kipengele cha muungano.
 
Wakuu inawezekana haya mambo huko nyuma tumejadili kiasi, lakini hili la kuibuka kwa ACT na kuanza kukosoa vyama vyote na kujiona chenyewe ndio chama sahihi zaidi, linanishangaza kiasi.

ACT, imenifanya nianze kujiuliza kuhusu mfumo wetu wa kusajili vyama ulivyo. Hii ni suala la kuwa na saini za watu tu, na idadi ya watu na ofisi tu ndio tunaanzisha chama? au kuna ya muhimu zaidi ya hapo?

Sijasoma katiba ya ACT, ningependa kujua kama kweli ACT iko tofauti kisera na kiitikadi na vyama vya siasa vilivyopo Tanzania. Na kama kweli ni chama ambacho kinatuletea mbadala wa sera na itikadi mbazo zitakuwa plus kwenye siasa za Tanzania, au ni chama ambacho kimeanzishwa kama njia moja ya ulaji kama vilivyo vyama vingi hapa Tanzania.

Memba mmoja hapa Acha Ushamba ameweka point moja nzuri sana. Point yake kutokana na hilo bandiko la Mwl.Kaijage ni kuwa ACT inaonekana ni chama cha kuangalia upepo, na kutoa maoni kutokana na upepo unavyokwenda sasa, na si chama ambacho kina jambo ambalo kinasimamia bila kujali upepo unavuma kuelekea wapi. Hii inanipa picha kuwa it is opportunistic party. I wonder how and why it got registered.

Tukiangalia wanachama wake, tunaweza kuona kama kweli hiki chama ni chama ambacho kinaweza kuwa chama cha siasa au ndio kundi la losers waliokataliwa kutoka kwenye vyama vingine kutokana na utovu wa nidhamu, na kutaka kuwavuruga wale waliowavuruga.

Tukiangalia baadhi ya mapendekezo 10 walioyotaja naona kama it is more of a collection of people who can be labelled as civil society na hata sio NGO, ambayo kazi yake ni kukusanya maoni na kuyaandika kwenye karatasi baada ya kufuatilia vyombo vya habari.

Mchambuzi, Nguruvi3, Ben saanane, Mwanakijiji, Pasco, The Big Show, Gor, Theroom, invisible, Hot lady ningeomba tujadili kidogo kama ACT ni zao za ubovu wa mfumo wetu wa kusajili vyama, au ni upungufu wa kisera na kiitikadi kwenye jamii yetu.
 
Muungano haupo tangu kufa kwa karume na Baadaye jumbe kukosa urais wa Tanzania mbona mnasumbua akili za Watu
 

Inasemekana kuwa hii ni nchi ya kidemokrasia.

Na ni haki yako kikatiba kuwa na uhuru wa kuunganika na wenzako na kuanzisha chama cha siasa ili mradi tu uweze kukidhi vigezo vinavyotakiwa.

Sasa kuna dhambi gani kikatiba na kisheria ya nchi hii kama ACT wameona wao ni mbadala wa vyama vingine hivyo katika kupigania haki za watanzania kisiasa kijamii na kiuchumi kwa ujumla?

Huwez kusema kuibuka kwa ACT ni uzao wa mfumo mbovu wa msajili wa vyama vya siasa n.k.n.k...

Hiko ukisemacho hakina uhalisia.

Pambananen na ACT kwa hoja na sio viroja.

At the end of all this wananchi pekee ndio wataamua.

Kila watu wazinadi sera zao.

Kama wengine sera zao ni uchaga waache wawe huru kuzinadi.

Kama wengine sera zao no udini waache wawe huru kuzinadi.

Kama wengine sera zao ni ukabila waache wawe huru kuzinadi.

Kama wengine sera zao ni ufisadi waache wawe huru kuzinadi.

Kama wengine sera zao ni ukombozi na demokrasia waache wawe huru kuzinadi.

Thats what we call Democracy.
 
Nilichokiona...watu wanahofu sana na ACT...wanajaribu kuwapuuza lakini hofu zinawafanya warudi kuwapinga ata pasipopaswa kupingwa.

Mchambuzi umezungumzia kijiweni....mie kijiweni nilipo Chadema imefifia sana..watu wameanza kutafuta mbadala...ACT ina nafasi ya kucover hilo gap pindi itakapoanza kufanya mikutano ya kisiasa kwa nguvu ili watu waijue inasimamia kwenye nini na italeta nini ambacho vyama vingine vya upinzani vineshindwa na kufanya uwezekano wa CCM kuwa chama cha upinzani uzidi kushuka siku ata siku.

Kuna watu wanazungumzia habari ya mjini sasa kuwa ni Tanganyika tu ata kama Tanzania itakufa, ni kweli lakini ACT hapa inajipambanua kuwa Tanzania Kwanza kisha Tanganyika, means tumlinde Tanzania aendelee kuexist pamoja na uwepo wa Tanganyika.

Hiki ni kitu ambazo Ukawa sio msisitizo kwao na CCM ndio hofu yao.ACT hapa wanatoa suluhisho la mkwamo huo, kwa kujenga serikali tatu ambazo zinabebwa na serikali kuu ya Tanzania, kwa hili wanaotaka serikali tatu watazipata na wasiotaka muungano ufe watapata wanachotaka.

Tusijifanye wapiga ramli hapa, lakini ni wazi kuwa wakati wa Chadema unakwisha na pindi Ukawa itakapokufa ndio mwisho wa Chadema.Hivyo tusiwalazimishe watu wawe na mawazo sawa.ACT ni muhimu kwake kujitofautisha na vyama vingine ili kuwapa Watanzania utofauti wake.
 
Nguruvi3, Mag3, Pasco, Mzee Mwanakijiji, EMT, JokaKuu, Jasusi, Kobello, Kitila Mkumbo, Zitto, Mtanganyika.










Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Bongolander,

Thank you !

Ningependa tujadili sana hilo suala la kisera na kiitikadi.Kuna mahali niliona wakijiita kuwa ni Social Democrats ambao kimsingi ideologically ni leftists.Sasa kwenye Ombwe la kiitikadi na kisera walete mezani ni kitu gani kilikosekana CCM(Wanaijiita Leftists ingawa wamechanganyikiwa) au CHADEMA(Centrists ambao wanaweza ku-swing Left kwenye social issues na Right kwenye Economic issues na hata haki za binadamu na za kiraia).,NCCR-Mageuzi na CUF(The Libs)

Niliona hata background figures wa chama wakiji-associate na Nyerereism wakati walikua wapinzani wakubwa wa Gradualism especially kwenye Pan-Africanism Tujadiliane sasa hapo na kama hapa sio sehemu muafaka basi tuanzishe open debate nyingine .
 
Last edited by a moderator:
Kitila Mkumbo,

..mimi nadhani kitu cha msingi ni kwamba CDM na ACT nyote mnaunga mkono serikali 3.

..hayo masuala ya hizo serikali 3 zitakuwa na muundo na mamlaka gani nadhani ni masuala ambayo yanajadilika.

..actually huu muundo wa serikali 3 ambao ACT mmeupendekeza mimi nakumbuka mara ya kwanza niliusikia kutoka kwa CUF.

NB:

..otherwise it will be interesting to know kama wewe ulikuwa unapinga mapendekezo ya CDM waliyoyatoa ktk tume ya Warioba.

cc Mchambuzi, THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Kitila Mkumbo..Nina maswali Matatu tu kwako..

1. Umesema dhana inaweza kufanana.. sawa..Je CDM ni lini na wapi walitamka wanataka Serikali 3 Legelege? ,Sambamba na hilo la kupinga Umri wa kugombea Urais...

2.Mmekua mkijinadi kuwa Bora na tofauti na vyama vyote hapa Nchini kwa kuwa karibu na jamii
Swali ..Je kwa yule Mtu wa kijijini ambaye hata kiswahili kinampa shida kuongea anaweza kujua maana ya ACT ??

3.
CCM-Chama Cha Mapinduzi

CHADEMA=Chama cha Demokrasia na Maendeleo

ACT = ??

Kukwepa Lugha yetu pendwa ya Kiswahili Katika utambulisho wa Chama/vyama ni Uzalendo au Usasa zaidi?
 
Last edited by a moderator:

Mkuu nafurahia mtazamo wako wa kuzingatia hoja na si kuleta vioja.

Kimsingi sipingi hicho chma kinachoitwa ACT, kama ulivyosema kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria. Lakini tunatakiwa tujiangalie kama ni kweli tunademokrasia tunayotaka itupatie vyama tunavyohitaji....or we have a systmen where democracy is demonstration of of craziness.

Nilichokuwa najaribu kukiongelea naona umegusia vizuri. NI kwamba (kwa mujibu wa sheria) tunaanzisha vyama kutokana na upepo tu au kutokana na kile wanachosimamia wanachama. Does ACT have any ideology that its members can be identified with? au ndio chama kimeibuka kutokana na opportunity ya mkwamo wa katiba. Au ni fursa ya kumpa mtu nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama au kugombea urais?

Umesema ni muhmu ACT ijitofautishe na vyama vingine, in other words una maana kwa sasa kiko sawa na vyama vingine. My question is why do we have a system which allows for redundancy of political parties?

Pia umesema muda wa CHADEMA umekwisha, hapo mkuu sielewi. Ina maana sera zake zimekuwa irrelevant? au chama kilundwa kwa msingi wa personality ya mtu na sasa huyo mtu hayupo chama hakipo tena.
 

Sawa kabisa mkuu. Unajua ili chama kiwe chama ni vizuri tujue kinaleta nini kwenye jamii na kwa nchi yetu.

Tatizo moja ambalo CCM inakumbana nalo ni kuwa kimetupa sera zake na itikadi zake zote. Kwa sasa tunaona wazi kabisa ujamaa na kujitegemea sio sera ya CCM tena (japo katiba yao imeandika hivyo), kwa hiyo waliokuwa kwenye CCM kutokana na kuamini ndio inawaongoza kwa hilo wanaona wameachwa njia panda. Kwa sasa sera kubwa ya CCM ni ubepari/ukabaila na kuombaomba....kuna mengi ya kuthibitisha kuwa vitendo vya chama kwa sasa ni hivyo.

Nimeweka pointi hii nikitaka kusisitiza kuwa kama chama hakina sera wala itikadi, basi sio chama. Litakuwa ni famba tu. Naona ACT ni chama kilichoanzishwa bila kuwa na sera.

It is stup!d for a person who was in CDM singing all along that CDM policies are best, and then starting a political party without telling us what went wrong with policies he screamed that were best.

Kwa wanaohama CCM ni wazi kuwa sera za CCM ya leo ni tofauti kabisa na sera za CCM 15 or 30 years ago. Au wanaojiunga sasa na CCM watakuwa wanafuata de facto policies za CCM ya sasa.

kwa hiyo sera na itikadi za Chama zinatakiwa kuwa wazi, ili tujue ni chama kipi kinalenga matarajio ya mtanzania.
 
Starehe ya Tz bw hata adui yako akikupa chakula unabugia tu bila hata tahadhari, km kina sumu wote wanapuputika. Fikria chama hiki kilipozinduliwa ccm walikuwa wageni rasmi waalikwa, hivi huu upendo wa ccm na ACT ulianza lini!!! Una faida gani?? Hivyo untegemea siku moja kutakuwa na karamu ambayo mungu atashiriki na shetani kuongoza kondoo???? Hivi ccm anaweza kumpenda anaetaka kumuondolea kitumbua chake mdomoni!! ACT ni branch ya CCM wawadanganye wenye uelewa mdogo. (Divishen v)
 

Kwahiyo wananchi wasubiri mikutano ya hadhara kujua ACT ni chama kikuu mbadala cha upinzani?

Kuna watu wanazungumzia habari ya mjini sasa kuwa ni Tanganyika tu ata kama Tanzania itakufa, ni kweli lakini ACT hapa inajipambanua kuwa Tanzania Kwanza kisha Tanganyika, means tumlinde Tanzania aendelee kuexist pamoja na uwepo wa Tanganyika.

Tanzania itakujaje kwanza Kabla ya Tanganyika? Huo Ndio muungano imara kwa maoni na mtazamo wa ACT? Hakika hii ni failure at launch.
Tanzania kwanza, Tanganyika Kabla, nje ya hapo hakuna muungano imara wala legelege.
Again, hizi ni pro active politics, not pre emptive. Mmesubiri miezi Sita kusoma upepo wa Tanganyika, Leo Ndio mnakuja na hoja za serikali Tatu baada ya kuona maoni ya wananchi. Katika mchango wake ndani ya BLK, zitto hakugusia suala la serikali Tatu Bali alikwepa hoja kwa kusema Kwamba haijalishi kuna serikali Ngapi huku akimaanisha Kwamba hata Mbili za sasa zinaweza kudumisha muungano. Huyu ni Mwenyekiti mtarajiwa wa ACT ambae sasa amebadili msimamo na kuegemea kwenye msimamo wa vyama Vinginevyo vyote vya upinzani.

Hoja ya ukawa kufa baada ya katiba mpya pia imewahi jadiliwa na zitto. Ni Kama vile chadema kiliundwa na kufanikiwa kwa misingi ya serikali Tatu. As long as chadema kinaendelea kupigania maslahi ya wananchi, kitaendelea kuwepo na kuzidi kufanikiwa. Ni mafanikio haya Ndio mnataka kubomoa huku Mkiwa hamna lolote kwa wananchi Kama mbadala zaidi ya ombwe lenye faida kwa CCM.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Muundo na mission ya serikali tatu halijawahi kuwa suala la ubishi. Kwanza tumalizane na ama serikali mbili au tatu ndipo tuje na muundo wa hizo serikali tatu. Inaonekana Kitila anafanya kile Wamarekani wanaita putting the cart ahead of the horse, ili tu kujionyesha ACT inatofautiana na UKAWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…