Msimamo wa China kuhusu mgogoro wa Ukraine

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wazee wa kuchochea...nyuma ya keyboard
 
Mtu kudai anataka ahakikishiwe usalama ina maana kuna kitu anaogopa; ni nini anachoogopa. Vita ya pili ya dunia ilianzishwa na kichaa mmoja huko Ujerumani; kuna hatari vita ya tatu ikaanzishwa na kichaa mmoja huko urusi. Katika nchi iliyoendelea mtu kujitangaza (kwa njia yoyote) kuwa yeye rais wa maisha ni jambo la hatari sana; wote wawili kwenye picha hiyo ni marais wa maisha!

Mtoto wangu aliyemaliza College mwaka huu alizaliwa wakati Putin ni Rais wa urusi, na clinton ni rais wa marekani. Leo hii marekani wamepita Bush, Obama, trump na sasa Biden, lakini Urusi ni Putin tu. Alipoona aibu akajiita Waziri Mkuu kwa muda lakini akiwa ndiye kinara
 
Haya ndio madhara ya kutosoma historia. Una habari kuwa China na Urusi zimeshawahi kuzichapa (kupigana)?

Una habari kuwa Marekani na Urusi zimeshawahi kuwa nchi washirika kijeshi katika vita?

Yote hayo nayajua
Hata Tz ni rafiki pia
Siasa mchezo mchafu sana hata Saddam na Bush walikuws wanashonesha viatu kwenye kampuni moja Italy
Mswahili bwana
Kwani ukinielewesha bila karaha haiwezekani?

Have a nice day
 
Sema pia Kuna sababu ya kufanya haya wanayoyafanya
Mfano
Russia iki introduce tu democracy......chaap mmarekan ataweka puppet pale Russia .....as well as CHINA
 
Haya ndio madhara ya kutosoma historia. Una habari kuwa China na Urusi zimeshawahi kuzichapa (kupigana)?

Una habari kuwa Marekani na Urusi zimeshawahi kuwa nchi washirika kijeshi katika vita?
Yaaaah mkuu

Baada ya kuanguka kwa USSR ....kulianzishwa na east western relations .....ndipo dini zilianza kuingia Russia...

USA alibaki unchallenged kwenye siasa za kimataifa.....

But

kuingia kwa Putin kuliiamsha urusi kurudi kuwa mpinzani mkubwa wa US........that's y warusi hawataki rais mwingine

Upande wa china...waligombana na Russia kipind Cha Gorbachev. Akiwa ni rais wa USSR baada ya kukubali mazungumzo ya amani na JF kennedy mwaka 1965's. Baada ya RUSSIA kufanya installment ya nuclear pale CUBA
 
Yote hayo nayajua
Hata Tz ni rafiki pia
Siasa mchezo mchafu sana hata Saddam na Bush walikuws wanashonesha viatu kwenye kampuni moja Italy
Mswahili bwana
Kwani ukinielewesha bila karaha haiwezekani?

Have a nice day
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]marekan Hana rafki wa kudumu
 
Yote hayo nayajua
Hata Tz ni rafiki pia
Siasa mchezo mchafu sana hata Saddam na Bush walikuws wanashonesha viatu kwenye kampuni moja Italy
Mswahili bwana
Kwani ukinielewesha bila karaha haiwezekani?

Have a nice day
Hakuna karaha yoyote! Nimeshangaa pale uliposema "always Mchina anamuunga mkono Mrusi". Kihistoria, si kweli!

Kinachowaweka pamoja ni maslahi ya pamoja. Maslahi hayo yasipokuwepo, wanaweza kukorofishana au hata kupigana vita. Historia imeonesha hivyo!
 
Sema pia Kuna sababu ya kufanya haya wanayoyafanya
Mfano
Russia iki introduce tu democracy......chaap mmarekan ataweka puppet pale Russia .....as well as CHINA
Katika Democracy, kiongozi wa nchi si anapatikana kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi huru na wa haki? Huyo 'puppet' wa Marekani anatokea wapi hapo?
 
Sawa! Pia rudi nyuma zaidi katika mgogoro wa kimipaka wa China na Urusi (Soviet Union) wa mwaka 1969. Walizichapa kwa zaidi ya miezi saba!

Urusi ilikuwa mshirika wa Marekani katika vita kuu mbili za dunia. Katika kipindi cha WWII, moja ya nchi zilizopokea misaada mingi ya kijeshi na kibinadamu kutoka Marekani ni USSR.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…