Msimamo wa China kuhusu mgogoro wa Ukraine

Msimamo wa China kuhusu mgogoro wa Ukraine

Hakuna karaha yoyote! Nimeshangaa pale uliposema "always Mchina anamuunga mkono Mrusi". Kihistoria, si kweli!

Kinachowaweka pamoja ni maslahi ya pamoja. Maslahi hayo yasipokuwepo, wanaweza kukorofishana au hata kupigana vita. Historia imeonesha hivyo!

Asante mkuu nimekuelewa
Pamoja sana
 
Sema pia Kuna sababu ya kufanya haya wanayoyafanya
Mfano
Russia iki introduce tu democracy......chaap mmarekan ataweka puppet pale Russia .....as well as CHINA
Nchi ikiwa ya demokrasi, kiongozi anachaguliwa na wanachi wenyewe, wakiona ni puppet wa nchi nyingine wanamuandoa; ndiyo maana ya demokrasi.
 
Hakuna karaha yoyote! Nimeshangaa pale uliposema "always Mchina anamuunga mkono Mrusi". Kihistoria, si kweli!

Kinachowaweka pamoja ni maslahi ya pamoja. Maslahi hayo yasipokuwepo, wanaweza kukorofishana au hata kupigana vita. Historia imeonesha hivyo!
Kweli kabsa mkuu.....now Russia kaona kidgo apunguze makali kwa kumgeukia Xi wa china
 
Katika Democracy, kiongozi wa nchi si anapatikana kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi huru na wa haki? Huyo 'puppet' wa Marekani anatokea wapi hapo?
Mkuu ....marekan ni kitu kingine kuhusu haya mambo......Nadhan una mkumbuka yule Alex.Navaz....mwanaharakati wa urusi aliyekamatwa.... Aliungwa mkono na nchi za magharibi...... assume Kama ndo anakuwa president
 
Mtu kudai anataka ahakikishiwe usalama ina maana kuna kitu anaogopa; ni nini anachoogopa. Vita ya pili ya dunia ilianzishwa na kichaa mmoja huko Ujerumani; kuna hatari vita ya tatu ikaanzishwa na kichaa mmoja huko urusi. Katika nchi iliyoendelea mtu kujitangaza (kwa njia yoyote) kuwa yeye rais wa maisha ni jambo la hatari sana; wote wawili kwenye picha hiyo ni marais wa maisha!

Mtoto wangu aliyemaliza College mwaka huu alizaliwa wakati Putin ni Rais wa urusi, na clinton ni rais wa marekani. Leo hii marekani wamepita Bush, Obama, trump na sasa Biden, lakini Urusi ni Putin tu. Alipoona aibu akajiita Waziri Mkuu kwa muda lakini akiwa ndiye kinara
kuna ubaya gani kwan kuna ulazima kila mmoja aendeshe ist wengin si wanaweza wakaendesha hata harrier wakiamua
fikra zakitumwa mpaka leo zinawatesa kweli kweli
nyie mlobadilisha marais mmewazidi nini RUSSIA na UCHINA kwenye angle za KISIASA KIJESHI KIUCHUMI nk mmewazidi kwenye sekta gani?
 
Haya ndio madhara ya kutosoma historia. Una habari kuwa China na Urusi zimeshawahi kuzichapa (kupigana)?

Una habari kuwa Marekani na Urusi zimeshawahi kuwa nchi washirika kijeshi katika vita?
ukisoma historia unahabari US alishawahi kua koloni la UK
mambo yanakawaida yakubadilika
 
Sawa! Pia rudi nyuma zaidi katika mgogoro wa kimipaka wa China na Urusi (Soviet Union) wa mwaka 1969. Walizichapa kwa zaidi ya miezi saba!

Urusi ilikuwa mshirika wa Marekani katika vita kuu mbili za dunia. Katika kipindi cha WWII, moja ya nchi zilizopokea misaada mingi ya kijeshi na kibinadamu kutoka Marekani ni USSR.
Yaaah mkuu ....nakumbuka but baada tu ya Ww2 ...1945 uadui ulirud Tena[emoji23][emoji23][emoji23] baada ya cold war kuanza ..... mmoja anaamini socialism huku mwingine capitalism
 
ukisoma historia unahabari US alishawahi kua koloni la UK
mambo yanakawaida yakubadilika
Pia kwa saiz.....ukichek vizr unaona kabisa .....saiz Uk ni kolon la marekani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].....coz kila marekan anachosema ......nao wapo
 
Kikubwa ukitaka kufaidi.....nenda kutokana na anavyotaka

Mfano Djbout Wana rais dictator toka kitambo ......but USA hawajawahi mzungumzia .......kwasabu .....Kuna military bases zake pale

Kweli kabisa uwe kibaraka wao na wanachotaka uhakikishe hakuna kukataa
Ila siku ukienda tofauti na wao utaondoka na utafanyiwa vitimbwi
 
Fuatilia kwanini kwenye janga la korona waliokufa wengi ni weusi
huko marekani .
Mtu anayeishi kijijini Tanzania ni bora x100 kuliko mtu anaeishi kwenye slums huko Marekani na ulaya.
Huu ni ushabiki sasa,
Wewe unaishi wapi? tuanzie hapo
Umefika vijiji vingapi Tanzania hii?
 
Mkuu ....marekan ni kitu kingine kuhusu haya mambo......Nadhan una mkumbuka yule Alex.Navaz....mwanaharakati wa urusi aliyekamatwa.... Aliungwa mkono na nchi za magharibi...... assume Kama ndo anakuwa president
Akiungwa mkono na mataifa ya nje sio shida.

Demokrasia haikomei katika uchaguzi wa kiongozi wa nchi pekee, bali inakwenda mpaka katika mfumo wa utawala na taasisi zake. Kuna bunge, upinzani, mahakama, vyombo vya habari ambavyo ni huru n.k. Rais asipowafaa wananchi, anaondolewa madarakani kupitia bunge lenye wawakilishi wa wananchi au uchaguzi mkuu.
 
kuna ubaya gani kwan kuna ulazima kila mmoja aendeshe ist wengin si wanaweza wakaendesha hata harrier wakiamua
fikra zakitumwa mpaka leo zinawatesa kweli kweli
nyie mlobadilisha marais mmewazidi nini RUSSIA na UCHINA kwenye angle za KISIASA KIJESHI KIUCHUMI nk mmewazidi kwenye sekta gani?
....Huelewi maana ya demokrasi. Na vile vile hujui maisha ndani ya Urusi na Uchina, unaangalia yale mapambo ya nje tu.
 
Back
Top Bottom