Msimamo wa nchi za Afrika juu ya suala la Urusi na Ukraine ni jambo dogo sana linalopaswa kuongozwa na kanuni, sio maslahi ya nchi zetu

Wewe unamfahamu Putin kuwazidi Warusi wenyewe? Waulize watu wanaoenda Russia mara kwa mara wakubie utawala wa Putin ni wa namna gani.

Udikteta wa Putin, hakuna hata mtawala mmoja wa Afrika anayeufikia. Huwezi kumkosoa Putin halafu kesho ukawa mtaani unarandaranda. Utakuwa na bahati ukiwa gerezani, lakini mara nyingi hitaonekana milele.

Anatumia hela ya Serikali kama yake binafsi. Watu wa karibu naye, mpaka binti yake, ni miongoni mwa mabilionea wa Russia. Na ole uhoji.
 
Kwa hiyo Misnky Agreement sijui inasema Zelensky akikiuka makubaliano Urusi ina haki ya kuvamia Ukraine na kuchukua sehemu za Ukraine, sivyo?
Unafanya argument na mtu ambaye haelewi hata hoja inayoongelewa.

Umenena vema sana, kila mwenye akili amekuelewa.

Kanuni zinasemaje kuhusu mipaka ya nchi. Hapa Tanzania kuna mkataba ulisainiwa kati ya Tanganyika na Misri juu ya matumizi ya maji ya Ziwa Victoria. Sisi tuliamua kwa makusudi kukiuka kwa sababu tuliona siyo sawa. Kwa hiyo baada ya sisi kukiuka, Misri ituvamie na ichukue sehemu ya eneo la Ziwa Victoria? Nadhani ndugu yetu wailer hov angesema ni sawa kwa vile Tanzania imekiuka makubaliano!!
 
Je, kitendo Cha Gadaffi kufanya hivyo ndo kiliwapa kibali NATO kuivamia Libya? Na hiyo ndo haki ambayo unataka kuisema hapa?
 
Kwa tulipo fikia dunia ya leo hakuna taifa ambalo lina heshima principles hasa pale linapo kuja suala la maslahi (interest) hakuna hilo taifa kwa sasa.

Maslahi ya kitaifa ndio chanzo Cha migogoro mingi ya dunia kwa Sasa leo USA na washirika wake wanaichokonoa China kuhusu Taiwan je, umekuwa kuja na mada humu kuomba viongozi wa Afrika walaani kitendo hiki au unayaona ya Urusi na ukrein?
 
Kwanza, maamuzi, hasa ya kisiasa siyo rahisi kama tunavyofikiria. Mimi ninachojuwa maamuzi ya namna hiyo kuna wakati yanafuata principle kuna wakati hayafuati kabisa principle. Kwa maana nyingine tusikimbilie kuilaani Urussi kwa principle peke yake.

Ni kweli Urussi ni kama amevamia Ukraine, lakini kila mtu anajuwa kisa na chanzo cha hili. Wafuasi wa siasa za dunia wanajuwa wazi, baada ya kusambaratika Urrusi kulikuwa na makubaliano yenye nia ya kuhakikisha Urussi haizungukwi na NATO hii ikiwa na maana nchi yoyote inayoingia NATO/EU inahatarisha usalama wa Urussi. Sote tunajuwa bifu kati ya Magharibi na Urussi.
Msimamo wa TZ kuhusu hili mimi nauafiki. Huko nyuma msimamo huu ulikuwa wa nchi zisizofungamana na upande wowote (East or West).

Ningependa kukubali kufuata principle ni kitu kizuri, lakini usiwe wewe tu unakuwa principled wengine hawaishi hivyo. Nitoe mfano kwa nchi ya Marekani. Marekani wao hawako principled na hawafuati principle isipokuwa pale tu principles zinainufaisha. Marekani kila siku inapiga kelele juu ya haki za binadamu za nchi zingine, lakini wao hawajioni kama wakiukaji wa haki hizo nyumbani kwao na nje. Na kila mahali Marekani imejiwekea kinga. Kwa mfano Mmarekani, wanasiasa wao, askari wao hawawajibiki kwenye mahakama ya "The Hague", lakini wakati huohuo wanataka nchi zingine zote ziwajibike isipokuwa wao. Hasa hapo wanafuata principle gani.

Kila mara tunasikia kelele zao kuhusu ukiukwaji haki za binadamu kwa mataifa ya nje, kitu ambacho ni kizuri, lakini ingekuwa vizuri zaidi wawe principled, kwa maana nao wanapokuwa na matatizo kama hayo wawajibike. Chukuwa mfano wa Iraqi, Afghanistan, Palestine ambako kumekuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu nyingi, lakini askari wao wana kinga. Kilichotokea au kinachotokea Ukraine ni sawa na yale yaliyotokea Palestine, Lebanon, Vietnam, Korea, Iraqi, Afghanistan, na kwingineko ambako Marekani iliyenda kupigana na kukimbia kwa aibu maana hakuna sehemu yoyote waliposhinda, mara nyingi kwenda kwao huko kulizigawa nchi hizo kuwa nchi mbili au tatu bila ridhaa.

Mmarekani siku zote anaamini kwenye interest zake at the expense of interest za nchi nyingine. Kwao kama kitu kina maslahi kwao basi hapo hakuna cha principle. TZ nayo inatakiwa iangalie ni wapi kuna faida kwetu sisi kama TZ, siyo kufuata principle kama vipofu. Hata kuendesha na kuisimamia familia yako, panapokuwa na tatizo siku zingine unatakiwa kwenda nje ya box, na hapo ndiyo unaweka principle pembeni na kuangalia kipi chenye maslahi kwa familia.

Maisha yetu binadamu tunakumbwa na kitu kama "kuchukuwa maamuzi magumu" na wakati mwingine maamuzi magumu ni pamoja na maamuzi yanayokinzana na convetional wisdom au principle. Najuwa wengi wetu humu JF tuna dini tunazofuata, uwe wislamu, mkristo, dini asilia, n.k. tuna misingi inayotukataza ushirikini na kuamini na kutumia njia au nguvu za giza. Ukweli ni kuwa hata hao staunch muslims, christians, born again kuna wakati wnapata shida au matatizo wanamuomba Mungu lakini hawapati majibu wanayotegemea. Ikifikia hapo wengi hukimbilia nguvu za giza kuona kama huko itawezekana! Wakristo, Waislamu, na walokole wangapi walikwenda kunywa kikombe cha babu Loliondo. Kwani hawa hawakuwa principled Christians/ Muslims. Mpaka rais wetu alienda kupata kikombe cha babu.

Kwa kifupi, binadamu hawezi kuishi na kutenda kwa principle peke yake. Principles zipo kufuatwa lakini siyo kuzifuata blindly. Msimamo wetu kuhusu Ukraine ni vizuri usifungamane na upande wowote. Kwanza hao Ukraine ni wabaguzi na vita ilipoanza wanafunzi wa Kitanzania walipata shida saana, sioni kwa nini tuwapige tafu. Hata Yesu alitumwa kutuokoa, lakini mateso yalimzidi akasahau kilichomleta duniani na kumuomba Mungu Baba ikiwezekana kikombe (mateso) kimpite.
 
Hawa viongozi wa kiafrica ni kama “malaya“; hustlers!
Na hawakumbuki kuwa hata Ukraine wakati ule ilikuwa Soviet Union; we are ruled by hustlers
 
Waafrica wakikumbuka haya yaliyotokea kwa waafrica wenzao wanajawa na huzuni sana na kuona hao unaowatetea ni wanafiki tu.
 
Elites wa Putin ulikutana nao Brazil na wakakuueleza matatizo ya Putin
Ww utakuwa Samia?
 
Je, kitendo Cha Gadaffi kufanya hivyo ndo kiliwapa kibali NATO kuivamia Libya? Na hiyo ndo haki ambayo unataka kuisema hapa?
Sheria za kimataifa zinasemaje? Unafahamu azimio la umoja wa mataifa lilikuwa linasema nini? Una uhakika ni NATO ndiyo iliyotekeleza mashambulizi dhidi ya utawala wa Gadafi au unahisi?

Kama hufahamu:

Under United Nations Security Council Resolution 678, a coalition of 35 countries, led by the United States, fought Iraq in the Gulf War from 1990–1991.
 
Ndahani una uelewa mdogo sana kuhusu masuala ya kimataifa. Mgogoro wa Taiwan na Hong Kong dhidi ya China mainland, chanzo chake ni nini? Unafahamu ulianza lini? Au umeanza kuusikia kipindi hiki kwa sababu kumekuwa na outlets nyingi za habari? Nini maslahi ya Marekani ndani ya Taiwan?
 

Ewa! Huu uzi unatisha kuona akili za watu wengine kukomalia uvivu mpaka wanageuzwa jinsia walahi uwiii [emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji33][emoji33]
 
Kwani hizo Sheria za kimataifa zinasema nini kuhusu kutumia raia Kama ngao ya Vita na hiyo ukrein ilifanya nini na ripoti mbali mbali tayali zilithibisha kwamba jeshi la ukrein lilitumia raia Kama ngao ya Vita je hatua gani zimechukuliwa na UN na hayo mabaraza ambayo yamejipa mamlaka ya kusimamia hizo principle ?

Acha kujitoa ufaham kuhusu suala la Libya liko wazi halihitaji hata tafiti kuling'amua
 
Kwa hiyo yako ndiyo data pekee iliyopo kuhusu mgogoro wa Urusi vs Ukraine?
 
Tunarudi pale pale mkuu masuala ya Taiwan na china ni suala la wachina na wataiwan wenyewe yeye Marekani yupo America uko yana muhusu nini ya China na Taiwan? Yeye mbona kaikalia kimabavu Hawaii na hakuna anaye mpigia kelele

Hayo mamlaka ya USA kujiona kila mgogoro una muhusu anatoa wapi ? Na kwa principle gani? Kama sio maslahi tu

Hakuna taifa la kijinga kwa Sasa ambalo lipo tayali ku-risk watu wake na resources zake kupigania taifa lingine pasi kuwepo maslahi hasa kwa USA na EU
 
Kwa hiyo tayari wewe ushafanya conclusion kujua mwema ni nani na mwovu ni nani katika pande hizo mbili. As if una barometer ambayo ukiitumbukiza tu kwa mgogoro itakuonyesha mrusi mwovu, myukraine mwema. Kwa kukosokena barometer hiyo ndiyo maana halisi ya neutrality -- katika hili tupo neutral kwa sababu kila upande una hoja zake za msingi, kila upande unaona upande mwingine ni mwovu, kila upande unajihesabia haki. Kwa nchi za kwetu zisizo na maslahi katika hili kulaani upande huu vs upande ule katika situation kama hii ni kujipendekeza tu.
 
Mie hapa wala sielewi ulichoandika, na ninahisi hata we mwenyewe ukiambiwa ufafanue ulichoandika hutaweza!
 
Waafrica wakikumbuka haya yaliyotokea kwa waafrica wenzao wanajawa na huzuni sana na kuona hao unaowatetea ni wanafiki tu.
I got several words for you; two wrongs don't make a right.

Yes there is discrimination in Ukraine against blacks just like in Russia, Germany, Italy, Greece and God knows where. Does that make it right for Russia to invade Ukraine?

And by the way, if you think Ukraine discriminates against blacks, try Russia!
 
Usimsemee Nyerere , maana hua hata iota ya uwezo wake wa kufikiri.
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…