Msimhukumu Rais Samia pasipokuwa na uhakika

Kwahiyo akiupiga mwingi anaupiga na hao unaotaka kujifichia kwao?
 
Ndio maana serikali duniani uwa zikishatoa elimu, asietaka kuelewa awamsubiri atawakuta wenzake mbele ya safari.
Ni kweli, hata wakati wa ubinafshaji wa viwanda serikali iliamua na tukawakuta mbele tukiwa tumechoka sana. Kisha Mkapa ambaye ndio alikuwa kinara wa ule uwekezaji tena kwa jeuri, akakiri kwenye kitabu chake kuwa alifanya kosa kubwa kubinafsisha viwanda! Kibaya zaidi hakuna aliyeweza kumchukulia hatua huku tukiwa tumeumia vibaya.
 
IGA sio sheria. Usitudanganye.

Amandla...
 

Kwanza yule ni felia elimu yake yenyewe yakuungauga kwa plasta,kaingizwa cha kike anakenua mimeno tu huku akiwapa waarabu hatmilik ya nchi,katiba ya hii nchi ya hovyo sana.
 
Inaonekana mkataba hujausoma au umeusoma ila hujauelewa. Unaposema mkataba hauna kipengere cha muda bali mikataba midogo ya kibiashara ndio itakuwa na muda hapo naona hujauelewa Mkataba huu. Mkataba huu ndio mama wa hiyo mikataba hiyo ya kibiashara. Huu mkataba umeshasema kabisa kuwa muda wake utaisha pale shughuli za bandari zitakapoisha sasa jiulize lini shughuli za bandari TZ sitaisha!!? Hii maana yake ni wa milele. Wanasheria wengi waliousoma wameutafasiri hivyo wakiwemo viongozi wastaafu.
 
Wakosoaji wamejikita hapa. 1. Kama jambo hili ni neema na litatuleletea faida, kwanini bandari za zanzibar hazijajumuishwa? Je, hawa wazanzibar wanaoamua kuingia mkataba na bandari za Tanganyika Je, wao hawayataki mapesa hayo kwao Zanzibar? 2. Kulikuwa na sababu gani kumpa mwarabu bandari zetu milele? Kwanini isiwe miaka kadhaa inapoisha wana-renew mkataba.
 

Hivi kwa mfumo wa chama cha mapinduzi na katiba ya hii nchi,kuna mtu yuko above rais??wengi ni puppets hasa humo kwenye chama ndio vichwa maji wamejazana.
 
Kwa uelewa wangu mdogo nilionao sehemu za bandari kati ya Tanzania bara na Zanzibar kwa sasa sio miongoni mwa vitu vya kimuungano.

Kama utakuwa na kumbukumbu mzuri mwezi uliopita tu katika harakati za kupunguza/kuondoa kero za Muungano bandari ilikuwa ni sehemu moja wapo iliyokuwa inatafutwa suluhu.
 
Wawekezaji wengi walioshindwa kuendeleza hivyo viwanda walikuwa wa ndani.

Ule aukuwa ubinafsishaji bali ufisadi.

Ukitaka mifano chanya angalia mabank angalia airtel. Fananisha faida zao na biashara hizo hizo zilizo chini ya serikali leo kwa asilimia 100.
 
Hivi kwa mfumo wa chama cha mapinduzi na katiba ya hii nchi,kuna mtu yuko above rais??wengi ni puppets hasa humo kwenye chama ndio vichwa maji wamejazana.
Anza kujipima ww kwanza
 
Vizuri uvitaje ivyo vipengele unavyoviongelea ili twende sawa.

Maana hayo unayosema hayapo kwenye IGA.
 
Swala la uendeshwaji wa bandari ni devolved matter toka mwaka 97, na Zanzibar wana mamlaka yao kuendesha bandari ambayo inasimamiwa na serikali ya mapinduzi.

Samia ni raisi wa muungano ata kama ni mzanzibari hana mamlaka ya kuwapangia Zanzibar on devolved matters; hayo ni mambo ya Mwinyi kwa sasa na baraza lake la mawaziri na bandari yao washampangisha mtu hivi tunavyoandika.

Hayo yakumpa bandari Mwarabu milele hayapo mahala popote ni upotoshaji tu, vinginevyo taja hiko kifungu.
 
jamaa lipuudhi sana na halijielewi
Angalia vizuri utaona sign zao zimo humo upande wa pili.

Acha uongo basi ni kwamba aliyesaini hilo li IGA sio mtu wa Serikali ya Dubai wala sio mwakilishi wa Serikali ya Dubai Bali ni mtu wa DP .
Embu nionyeshe hao waliosaini upande wa Serikali ya Dubai

Angalia vizuri utaona sign zao zimo humo upande wa pili.
 
Angalia vizuri utaona sign zao zimo humo upande wa pili.

His Highness Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, huyu ndiye kiongozi wa Serikali ya Dubai.
Kwenye hilo li IGA hakuna signature yake wale power of attorney yake .
Wakati upande wetu kuna saini ya Rais na power of attorney yake ya kumuidhinisha mzanzibari mwenzake auze bandarini zetu zote

content://com.android.chrome.FileProvider/images/screenshot/1688498991925861510822.jpg
 
Wewe kweli msomi. Nakuvulia kofia.
1. Unasema kuwa paragraph ya kwanza haizumzii IGA. Hivi hiyo Agreement itakayo remain in force ni nini kama sio IGA? Hicho unakazania ni vitu vitakavyotokea ili IGA isite kuwa enforceable. Navyo ni:
1. Miradi yote iishe.
2.HGAs zote na Mikataba ya miradi iishe.
Kwisha kwa mradi mmoja au miwili na hata HGAs nyingi zikiisha ili mradi ziko ambazo ni active IGA inakuwa enforceable. Hilo la haki ya kuvunja mkataba kiholela umelitoa wapi?
2. Bado unajichanganya. Article 20 kinahusu IGA sio HGA. Na ni kimbilio pekee kama upate mmoja hautaridhika na IGA maana para 4 ya Article 23 inasema IGA haiwezi kubezwa, kuahirishwa au kuvunjwa kwa sababu yeyote ile. Wewe unatujia na mambo yako ya kufikirika ya kuvunja IGA kiholela.
3. Hii Bilateral Agreement sio mkataba wa kujenga barabara, kiwanda, kununua mafuta n.k. ndio maana sio commercial agreement. Ni mkataba wa ushirikiano baina ya mataifa mawili katika maeneo yaliyoainishwa ndani yake.
4. Mtetezi wa serikali katika masuala ya mikataba ni AG, sio wakili wa wizara. Hauoni katia pua halafu kasepa. Amewaachia nyie wanasheria uchwara na wakina Steve Nyerere kutetea kitu ambacho hakiwezi kutetewa.
Baada ya huu mjadala ndio naanza kuelewa kwa nini Law School inawafelisha kiasi kile maana hata basic reasoning hamna. Mnajiona mna uelewa zaidi ya maprofesa wenu kama wakina Shivji na former AGs kama Warioba. Mnasikitisha sana.
By the way, condition katika mkataba sio sheria. Kama hata hilo haulijui basi there is no hope for you.

Amandla...
 
Hilo jamaa Mayor Quimby ni lijinga kabisa litakuwa lilikwenda shule kusomea ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…