Kama kweli Simba inahitaji kufanya vizuri kimataifa inatakiwa isajili wachezaji wanne/watano watakaoingia moja kwa kwa moja kwenye first eleven:-
1. Beki mmoja wa kati mwenye uwezo sawa au kumzidi Inonga ili Onyango abaki kucheza kwenye ligi ya ndani kwani ndio saizi yake kwa sasa. Iwapo Simba watakuwa na uwezo wa kuaachana naye waachane anaye kiungwana/ kistaarabu kwani ni mmojawapo wa wachezaji walioisaidida Simba kufika hapa ilipofika ndani ya misimu mitatu/minne iliyopita
2. Beki wa pembeni mweye uwezo wa kucheza kushoto na kulia kwa ufasaha ili kufanya "rotation" na Kapombe na mwenzake Mohamed Hussein kwani hawa jamaa hawapumziki kwa sababu hawana mbadala na hasa mechi muhimu zinapofuatana. Mara nyingine mpaka nawaonea huruma. Ikishidikana kupata beki mwenye uwezo wa kucheza pande zote mbili basi asajiliwe wa upande wa kushoto Gadiel aachwe kwa heshima na taadhima na apewe zawadi kwa kuonyesha nidhamu na uvumilivu kwa kipindi chote alichodumu Simba.
3. Kiungo mkabaji wa chini asili mwenye uwezo mzuri wa kupora mipira na kuilinda "back four"" na uwezo wa kuanzisha mashambulizi. Huyu awe na uwezo sawa au kuwazidi viungo wa zamani wa Simba Tadeo na Fragga.
4. Mshambuliaji wa kati mwenye nguvu na uwezo wa kukaa na mali kama alivyokua mshambuliaji wa zamani wa Simba Mugalu. Huyu atasaidia sana kwenye zile mechi ambazo timu inakwenda kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza. Mfano mzuri mechi ya Waydad kule Morocco Simba ilikosa fowadi wa aina ya Mugalu kwani Baleke alifichwa na watu wawili na kwa kua hana nguvu sana alipotea kabisa. Ifahamike kuwa kwenye mechi kama ya Waydad inatakiwa mshambuliaji wa kati apokee mpira katikati ya mabeki wawili au watatu na aweze kuudhibiti mpira na kuwadhibiti mabeki wa timu pinzani kwa sekunde 30 mpaka dakika mmoja ili washambuliaji wenzake waliokuwa wanazuia wapande mbele haraka awape mpira waweze kushambulia kwa haraka.
5. Winga mmoja mwenye kasi anayeweza kucheza kushoto na kulia kwa usahihi na awe na uwezo wa kufunga magoli. Hapa bila kupepesa viongozi wa Simba wafanye kazi usiku na mchana wamrudishe Miquisone kwani kisingizio cha pesa hakipo tena kutokana na fedha watakazopewa na CAF kwa ajili ya Super League.
Naamini kabisa iwapo viongozi wa Simba watafanya "homework" yao vizuri na kuwapata wachezaji sahihi kwenye nafasi nilizotaja hapo juu hapo ndio itakuwa sahihi kwao kuzungumzia suala la nusu fainali, fainali au ubingwa wa Afrilka. Vinginevyo wakirudia makosa waliyoyafanya kwenye usajili uliopita ambapo wachezaji tena wa kimataifa Okwa na Akpani unawapeleka kwa mkopo ndani ya miezi sita ya usajili na huku Outtara anaozea benchi kwa kweli ni mzaha na kuhujumu uchumi wa Simba na pesa za mwekezaji.
Na kitendo cha kutamka tu kufika nusu fainali au kuchukua ubingwa wa Afrika bila ya kufanya usajili sahihi wa kufika huko ni mzaha wa hali ya juu kwa wanachama, mashabiki wa simba na watanzania kwa ujumla. Bara ala Afrika limejaa wachezaji wengi tena vijana wenye vipaji vikubwa suala kubwa tu Simba kuanza sasa usajili wasisubiri ligi ziishe wataambualia makapi.
Ni mtizamo tu.