Msimu wa Mateso kwa Watumishi: Halmashauri zimeanza kuwatishia Walimu na watumishi wengine kutoa mchango wa Mwenge, 2023

Msimu wa Mateso kwa Watumishi: Halmashauri zimeanza kuwatishia Walimu na watumishi wengine kutoa mchango wa Mwenge, 2023

MoseKing

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2017
Posts
4,928
Reaction score
8,976
Yaani kuwa mtumishi Halmashauri ni kama laana, kimshahara chenyewe cha mtumishi ni kidogo, alipe Kodi ya nyumba.

Bado Serikali inashirikiana na vyama vya Wafanyakazi kukata pesa za mishahara ya Watumishi bila msaada, then kwenye kimshahara hicho hicho bado unatishiwa na kulazimisha kuchangia Mwenge.

IMG_20230326_171821.jpg


MKURUGENZI AFAFANUA
Mkurugenzi Ifakara.JPG

Lena Nkaya

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Lena Nkaya amesema “Huo ndio utaratibu unaotumika kwingine, unaweza kuuliza kwingine pia.

“Mimi nilikuwa nimesafiri, ofisi nikamkabidhi Afisa Elimu Msingi, nadhani wao wamekaa na kukubaliana hilo suala, nitafuatilia kuona kama kweli kuna Walimu ambao hawakushirikishwa na wanalalamika.

“Lakini utamaduni wao huwa wanafanya hivyo, waliojiwekea kama Wadau wa Mwenge au Wadau wa maendeleo, mfano wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara, wafugaji na kigezo kimojawapo kinachotumiwa ni jinsi ambavyo walikusanya michango wakairudisha kwenye jamii.

“Sijui kuhusu Halmashauri nyingine wanafanyaje lakini unaweza kuuliza ukapata utaratibu wao upoje."
 
Yaani mishahara yenu midogo, mapunjo na maslahi mengine kulipwa ni mbinde, matibabu mnayopaswa kugharamiwa ni kama fadhila lakini bado mnachangishwa kwa nguvu kutoka katika mishahara yenu kugharimia mbio za Mwenge kama kwamba nyie ndio mlioziomba zifanyike.

Na kwanini kila michango mnang'ang'aniwa nyie zaidi ya watumishi wengine wa Umma?

Hili la huko Ifakara nadhani ni la nchi nzima na hamuwezi kulipambania kwa sababu chama chenu CWT ni tawi la CCM na mmelikubali hilo kwa furaha.

Mpaka lini mtakubali unyonge huu?

IMG-20230326-WA0022.jpg

 
Back
Top Bottom