Msimu wa Mateso kwa Watumishi: Halmashauri zimeanza kuwatishia Walimu na watumishi wengine kutoa mchango wa Mwenge, 2023

Msimu wa Mateso kwa Watumishi: Halmashauri zimeanza kuwatishia Walimu na watumishi wengine kutoa mchango wa Mwenge, 2023

Walimu ifike muda wajitambue, yaani ktk watumishi wote ni wao tu Ndio wa kuchambia namna hii,

Mbona sekta zingine haya mambo hayapo? Lakini pia nao hawa wakurugenzi waone aibu kama unyanyasi umezidi kiwango na huu ni udhalilishaji watumishi kwa kuchagua nani awe mnyonge kwao na wengine waachwe.

Rais alione hili na ikiwezekana alikemee litaleta chuki dhidi ya serikali hata kama walimu ni wanyonge ama kuendelea kutukanwa kwao .
 
Ivi mwenge unahusu walimu tu? Kwanini wachange peke yao? Aya mambo sio ya kuendekeza mwenge una bajeti yake iweje uchangiwe kwa account za michongo? Hivi vitu vinafanyika nchi nzima mwaka jana nilikisikia malalamishi kuwa pesa hizo zilipigwa na watoto waliohusika kuchezea mwenge walitolewa kapa.

Tutafika kweli? Wapi nchi inaelekea! Tulishasema zima mwenge uweke makumbusho hatuna faida za mwenge ni hasara tupu na matumizi mabaya ya kodi zetu.

IMG-20230327-WA0000.jpg
 
Yaani mishahara yenu midogo, mapunjo na maslahi mengine kulipwa ni mbinde, matibabu mnayopaswa kugharamiwa ni kama fadhila lakini bado mnachangishwa kwa nguvu kutoka katika mishahara yenu kugharimia mbio za Mwenge kama kwamba nyie ndio mlioziomba zifanyike.

Na kwa nini kila michango mna ng'ang'aniwa nyie zaidi ya watumishi wengine wa Umma?

Hili la huko Ifakara nadhani ni la nchi nzima na hamuwezi kulipambania kwa sababu chama chenu CWT ni tawi la CCM na mmelikubali hilo kwa furaha.

Mpaka lini mtakubali unyonge huu?

View attachment 2567023
Waalimu ndio the most loyal of all! Huwa wanakubali kila kitu.
P
 
Kwani mkikataa kuchangia watawafanya nini? Huu ni upumbaf
Asipochangia ataripotiwa kwa mkurugenzi na afisa elimu. Kisha atakumbana na yafuatayo:

1. Atajenga bifu la hatari na mkuu wa shule
2. Atajenga bifu la hatari na afisa elimu.
3.Atajenga bifu na wapambe wa mkuu wa shule.
4. Ataishi kama mkimbizi
5.Hakuna fursa atakayokutana nayo
6. Kama yuko maeneo ya mjini ajiandae kuhamishiwa kikijini.

Wewe ungefanyaje? Hii ndio tz.
 
Ivi mwenge unahusu walimu tu? Kwanini wachange peke yao? Aya mambo sio ya kuendekeza mwenge una bajeti yake iweje uchangiwe kwa account za michongo? Hivi vitu vinafanyika nchi nzima mwaka jana nilikisikia malalamishi kuwa pesa hizo zilipigwa na watoto waliohusika kuchezea mwenge walitolewa kapa.

Tutafika kweli? Wapi nchi inaelekea! Tulishasema zima mwenge uweke makumbusho hatuna faida za mwenge ni hasara tupu na matumizi mabaya ya kodi zetu.

View attachment 2567090
Kada zote zina changa kumbuka hiyo barau ni kada ya Elimu,bado kuna barau kada ya afya Arudhi utumishi nakadhalika
 
Back
Top Bottom