Msimu wa Mateso kwa Watumishi: Halmashauri zimeanza kuwatishia Walimu na watumishi wengine kutoa mchango wa Mwenge, 2023

Msimu wa Mateso kwa Watumishi: Halmashauri zimeanza kuwatishia Walimu na watumishi wengine kutoa mchango wa Mwenge, 2023

Nadhani kama kuna watu wana maslahi kwenye huo ushirikina unaoitwa mwenge wangejaza wenyewe mafuta kuliko kuwafanya walimu kuishi katika hali ya mashaka kwenye nchi yao wenyewe.
 
Yaani mishahara yenu midogo, mapunjo na maslahi mengine kulipwa ni mbinde, matibabu mnayopaswa kugharamiwa ni kama fadhila lakini bado mnachangishwa kwa nguvu kutoka katika mishahara yenu kugharimia mbio za Mwenge kama kwamba nyie ndio mlioziomba zifanyike.

Na kwanini kila michango mnang'ang'aniwa nyie zaidi ya watumishi wengine wa Umma?

Hili la huko Ifakara nadhani ni la nchi nzima na hamuwezi kulipambania kwa sababu chama chenu CWT ni tawi la CCM na mmelikubali hilo kwa furaha.

Mpaka lini mtakubali unyonge huu?

Watajuana na mwajiri wao, kama wao wenyewe hawawezi kusimama kujitetea tuwaache wameridhika
 
Tafadhari sana Kiongozi kwa heshima ya kutosha nikupayo naomba uwaombe radhi walimu wate wa Tanzania kwa kauli yako hapo juu. binafsi naona umepitiliza sana katika uhuru wako wa kutoa maoni kikatiba lakini pia unajinasibu vipi wewe ni msomi na mwerevu katika mambo mengi kama unamdharau Mwalimu wako aliekufundisha mpaka kufika hapa?

Unaandika kwa kufuata taratibu za uandishi na kupangilia Herufi vizuri bila kukosea na unamtukana aliekufundisha kuwa MJINGA SANA hii ni sawa kweli? Nilikuwa na nguvu za kusoma komenti za wadau lakini nilivyofika kwenye mchango wako nikakwama na kujisikia vibaya.

Ukiwa askari unaweza kutambua hili kwamba Senior kwako hubaki senior tu hata akistaafu na cheo kidogo kupita wewe.

Kwangu naona umeikosea Taaluma ya ualimu nchini na umewakosea walimu wetu na umewakosea watu wote waliopewa na kurithishwa taaluma na walimu hao.
Hata mimi huyo MBWA amenikera sana sana!! Huyu mwalimu anayemtukana siye aliyeandika barua.

Sote kupitia barua hiyo tumejifunza namna ambavyo kundi hili muhimu linavyoonewa.

Hivi katika mazingira hayo angekuwa ni yeye angefanya nini? Kwa sasa walimu hawastahili kujipigania wao wenyewe, bali Watanzania wote tunatakiwa kuwapigania.

Ni bahati mbaya sana CWT siyo tena Chama cha kuwatetea...na bahati mbaya sana sana CHADEMA iliyokuwa ya Dr Slaa siyo hii ya Mbowe na Lema ambayo baada ya kushiba inatukana kila mtu!

Huenda huyu anayetukana walimu ni LEMA!! Kashiba burger
 
Huo moto wa kichawi si unayo bajeti yake KILA mwaka au wajanja wanataka kupitia humo humo
 
mpwayungu village njoo hapa kuna jambo lakooo.
Njoo utoe neno, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Itafika wakati hawa walimu tuanze kuwapima akili zao huenda huwa wanatolewa ubongo maana hawajawahi kuhoji hata kukataa wao kila agizo ni mwendo wa ndio. Itafika wakati nitawatembezea viboko akili iwakae sawa malofa haya, ni majinga sana, yapo yapo tu tena huenda mwanafunzi ana akili kuliko mwalimu maana Kuna wanafunzi hata kuchapwa huwa wanakataa nawanafanya mgomo ila sio Kwa hawa kuku (mialimu)
 
Asipochangia ataripotiwa kwa mkurugenzi na afisa elimu. Kisha atakumbana na yafuatayo:

1. Atajenga bifu la hatari na mkuu wa shule
2. Atajenga bifu la hatari na afisa elimu.
3.Atajenga bifu na wapambe wa mkuu wa shule.
4. Ataishi kama mkimbizi
5.Hakuna fursa atakayokutana nayo
6. Kama yuko maeneo ya mjini ajiandae kuhamishiwa kikijini.

Wewe ungefanyaje? Hii ndio tz.
Ataonekana shujaa akifanyiwa haya
 
Ahsee utapigwa spana za kutosha na mkuu wa shule hata kusalimiana hamtasalimiana, wakuu wa shule ni mbwa wanaombweka. Akibweka walimu wote kimya [emoji28][emoji28][emoji28]
Aisee, mimi ningeshafukuzwa kazini siki nyingi, kuna mambo siyo ya kuendekeza...
 
Yaani kuwa mtumishi Halmashauri ni Kama laana.

Kimshahara chenyewe Cha mtumishi ni kidogo, alipe Kodi ya nyumba.

Bado serikali inashirikiana na vyama vya wafanyakazi kukata pesa za mishahara ya watumishi bila msaada.

Then, kwenye kimshahara hicho hicho bado unatishiwa na kulazimisha kuchangia Mwenge.

View attachment 2566693
Kwaio mei mosi mtakuwa pamoja na walimu na watumishi wengine kudai maslahi Yao ?

Au nini kifanyike ?

Hao wenye laana ya kuwa watumishi wa HALMASHAURI wana muhudumia nani ? Je watoa huduma kwa niaba Yao wenyewe ?

Hakuna haja watu kutafuta taaluna za kuja kutumikia watu katika HALMASHAURI kwa sababu ni laana wanayoyafanya ?

Taaluma ya ualimu na ikimbiwe kwa hujuhudi zote maana ni laana, na hivyo serikali isijisumbue huko ?

Hitimisho: tuiopongeze serikali kwa kutokuajili walimu na kutotoa ajira kwa wataalami katika HALMASHAURI hivyo kuwaepusha vijana wetu na laana.


Siii Siii Eemu Oee.
 
Yaani mishahara yenu midogo, mapunjo na maslahi mengine kulipwa ni mbinde, matibabu mnayopaswa kugharamiwa ni kama fadhila lakini bado mnachangishwa kwa nguvu kutoka katika mishahara yenu kugharimia mbio za Mwenge kama kwamba nyie ndio mlioziomba zifanyike.

Na kwanini kila michango mnang'ang'aniwa nyie zaidi ya watumishi wengine wa Umma?

Hili la huko Ifakara nadhani ni la nchi nzima na hamuwezi kulipambania kwa sababu chama chenu CWT ni tawi la CCM na mmelikubali hilo kwa furaha.

Mpaka lini mtakubali unyonge huu?

 
Back
Top Bottom