Msimu wa Mateso kwa Watumishi: Halmashauri zimeanza kuwatishia Walimu na watumishi wengine kutoa mchango wa Mwenge, 2023

Tija ipi kwa mfano
Barabara ukarabatiwa kwa wakati, miradi mingine ya maendeleo ufufuliwa , uchochea amani, mahusiano mema kwenye jamii nakadhalika.

Kwa ufafanuzi zaidi, fuatilia majibu ya Mweshimiwa Waziri huko bungeni hapa chini.
=====

MHE. KHATIB SAID HAJI aliuliza:-
(a) Je, bado kuna faida kwa Watanzania kuendelea kukimbiza Mwenge wa Uhuru kila mwaka, kama zipo ni faida gani?
(b) Kama hakuna faida, je, ni lini Mwenge huo wa Uhuru utasitishwa?


Answer​

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,
KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze muuliza swali leo kwa kukaa upande ule alioulizia swali. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Khatib Said Haji, Mbunge wa Konde, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, faida za Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Kimataifa ni pamoja na kuendelea kuhamasisha ari ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika Taifa letu; kuwa ni chombo pekee cha kujenga umoja, mshikamano na kudumisha amani pale ambapo Mwenge unapita bila kujihusisha na itikadi za kisiasa; kuendelea kuhamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa Watanzania wa pande mbili za nchi yetu; na kila mwaka hufungua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya wananchi na kuhamasisha uzalendo wa kuendelea kujitolea. Mfano mzuri ni kutokana na takwimu zilizopo ambazo zinaonyesha miradi ya maendeleo iliyozinduliwa pamoja na kuwekwa mawe ya msingi kupitia Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015/2016 ni pamoja na miradi 1,342 yenye thamani ya shilingi 463,519,966,467.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Kimataifa Mwenge
wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana na maudhui yake ya kumulika hata nje ya mipaka yetu kwa kuwa msuluhishi wa amani katika Bara la Afrika na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine ya Afrika duniani kote. Umoja, mshikamano, upendo na ukarimu wa Watanzania ni matunda pia ya Mwenge wa Uhuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na faida na mafanikio makubwa yanayopatikana kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru, Serikali inaamini kuwa zipo faida za kuendelea kukimbiza Mwenge huo wa Uhuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, Serikali haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru. Dhana hii itakuwa ni endelevu na tungependa kuiendeleza kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.
 
Walimu wanaonew
Walimu wakuu wanaonewa zaidi. Iweje walimu wa kawaida walipie sh 5000 wakati mwalimu Mkuu atoe sh. 50,000? Hali hii inachangia walimu wakuu kudokoa pesa za michango ya wazazi ili waweze kulipa pesa hizo . Hii si sawa hata kidogo.
 
Hili li nchi hili! Hata hawajui priorities zao! Wanachezea pesa za kodi zetu kama nini, halafu wanakuja kuwakamua walimu? Wakitoka hapo wanaenda kununua V8, nasi tupo tumekaa kimya kama wajinga fulani hivi!
 
Wanawatisha ndio ukitaka kujua kuwa wanatishwa soma hiyo barua hadi mwisho utaona wanapotishwa, mwalimu mkuu anaambiwa akusanye zote na atume na aandike majina wale wote watakao changa na wasio changa waandikwe pia sasa hiyo ni nn kama sio kuwatisha wasiotoa?????
 
Hivi mtu asipotoa wanamfanyeje?

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…