Msingi tu iwe 13m?! Huyu fundi mbona kama anataka kuleta za kiinjinia!

Mkuu ukifuata stages zote za ujenzi huwezi kuwa suprized na bei. kuna watu wako soo professional mtu aliyekuchorea ramani kama ni mtaalamu na umemlipa hela yake nzuri anakupa bill of material kutokana na stage ya ujenzi unayofanya sasa ukimpata huyo foreman unatambaa tu na karatasi yako inayoonyesha mgawanyo wa gharama kulingana stages,... tatizo watu wengi wanazarau hizi stage za ujenzi. ukitaka upate unafuu katika ujenzi usiruke stage hata moja ( cheap is always expensive)
 
Fundi ndio anataka 13m ya ufundi tu
  1. Tofali nzito zipo 2150
  2. Nondo 16mm zipo 75
  3. Cement zipo 150. Anasema haitoshi msingi na nguzo

Principle ya ujenzi ni moja...

Gharama ya ufundi isizidi gharama ya material, mara nyingi inapaswa icheze kati ya 20% ~ 60% ya gharama ya material, hii ni kulingana na ugumu wa kazi...

Mathalani kazi kama ujenzi wa msingi, paa, kupandisha boma hizi ni ngumu na muhimu kwenye ujenzi, hivyo ufundi wake huwa ni asilimia za juu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…