Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,367
- 2,407
Dhana kuwa awamu ya 5 imeleta maendeleo pengine maneno haya ni magumu kuyaelewa kwa kijana aliye na shahada ( degree) ya chuo kikuu na yupo mtaani hajapata ajira kwa miaka kati ya 4 mpaka sasa.
Kwa maneno ya Rais mwenyewe (mkutano na chama cha madaktari) alikiri kuwa madaktari 2700 wapo mtaani bila ajira. Akaahidi kuajiri 1000 ahadi ambayo kaitimiza hivi punde. Hii inamaanisha kwamba madaktari 1700 bado wapo mtaani wanasota. Kumbuka hii ni fani adimu kuliko zote TZ kwa wakati huu.
Fani nyingine hazijakumbukwa kabisa, hii inamaana kuwa zaidi ya wahitimu 40,000 katika fani mbalimbali wapo mtaani wamekata tamaa ya kupata ajira. Maendeleo yazungumzwayo kama Ununuzi wa ndege, ujenzi wa barabara, SGR, St Gauge bado si jibu kwenu. Kimsingi kila mmoja hulia na shida zake, ni wakati wa kujiuliza hivi maendeleo yote akina POLEPOLE wanayoyapigia debe yamekusaidia nini wewe binafsi?
Ushauri wangu kwenu msioajiliwa. Huu ni wakati muafaka wa kuja na siasa mbadala zitazowaokoa kutoka mtaani na kukuza vipaji vyenu katika fani zenu. Kama chama tawala hakijawasaidia, si wakati tena wa kuimba mwimbo huo huo usiokupatia mafanikio yeyote.
Jibu la matatizo yenu lipo katika maamuzi magumu ya kisiasa. Anzisheni harakati maalum katika chama chochote cha upinzani utachoona kitawasikiliza na muendeshe hoja za msingi zitazowakomboa. Mkibweteka hamtaweza kutatua matatizo yenu, mkibaki kulia tu na kuitwa wazururaji. COME ON VIJANA WAKATI NDIO HUU.