Msioajiriwa kwa wahitimu wa Chuo Kikuu mna nini cha kuisifu awamu ya 5?

Msioajiriwa kwa wahitimu wa Chuo Kikuu mna nini cha kuisifu awamu ya 5?

Ukitaka kujua nguvu ya upinzani angalia jinsi CCM bila siri inakiri kuwa waliyoyapigia kelele wapinzani huko nyuma ndio Chama tawala inatekeleza. Hili si dogo ni kubwa sana kwani huko nyuma madude yaliyoyokuwa yanafanyika ndani ya serikali yalikuwa hayaweki hadharani, kwa kisingizio kuwa hayo ni mambo ya siri za ndani. Milinga aliharibu ATC - Adhabu yake eti kupewa ukuu wa mkoa Mara. Jamani hawa watu wametutesa!!!!

CCM ni sikio la kufa, halisikii dawa. Kufanya mabadiliko haiwezi kamwe. Kinachofanyika si strong party bali ni strong man. Usiponiamini subiri mkuu aondoke, sera zote zitakifa na kuendelea na bussiness as usual.

Kila rais aingiae madarakani haishi kumkosoa aliyepita/waliopita na yeye (mpya) kuanza upya. Ukianza upya kila baada ya miaka kumi, huna mabadiliko wewe. Hata nia ya mabadiliko huna ila ulikua unalilia tumbo lako kwa slogans za kinadharia tu.

Licha ya kuuponda upinzani, lakini moja wanalo - Kuwainua vijana ili iwe sauti ya umma kesho na keshokutwa. Na vijana ndio wataoleta mabadiliko sio Mwenyekiti. Ukitumia muda mwingi kulilia Mbowe unapoteza muda wako, ongeza mawazo yako na fikiri nje ya box.
Boss, Hayo yalijulikana hata kwa mwananchi mtaani. Siyo mambo ya vyma avya siasa au viongozi wa kisiasa. Tatizo ilikuwa ni utashi wa rais haukuwepo. Leo yanafanyiwa kazi kwa nguvu, munarudi na kusema bora awamu ya 4! Hiyo ni akili au kitu gani? Tena anayesema ni Lissu, anayeungwa mkono eti ni shujaa.
 
Niliwahi kumshauri Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh.J.J.Mnyika kwamba "Wahitimu wa vyuo vikuu wasiokuwa na ajira hasa kada kama ualimu, Udaktari, Ufamasia na fani nyingine yoyote ambayo kujiajiri mpaka muwe team na muwe na pesa za kutosha (15 millions and above) awashike mkono na HOJA ya AJIRA iwe moja kati ya malengo makuu ya serikali itakayoundwa na chama chake baada ya uchaguzi mkuu 2020.Hajawahi kunijibu!
Wabunge baadhi hasa Mh.Heche na Mh.Kishimba wamelitumia wazo langu na hoja yangu ya AJIRA KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU leo kila mtu anawaona ni watu makini sana.
Ninatoa wito tena, ajira za kujisikia au mpaka uombwe physically sasa baaasi!
Kunatakiwa kuwe na utaratibu na mipango ya kikatiba inayoelekeza kiasi na kiwango cha AJIRA MPYA kila mwaka kwa percent ya wahitimu!
CHADEMA nieleweni, ndugu zangu.
Dhana kuwa awamu ya 5 imeleta maendeleo pengine maneno haya ni magumu kuyaelewa kwa kijana aliye na shahada ( degree) ya chuo kikuu na yupo mtaani hajapata ajira kwa miaka kati ya 4 mpaka sasa.

Kwa maneno ya Rais mwenyewe (mkutano na chama cha madaktari) alikiri kuwa madaktari 2700 wapo mtaani bila ajira. Akaahidi kuajiri 1000 ahadi ambayo kaitimiza hivi punde. Hii inamaanisha kwamba madaktari 1700 bado wapo mtaani wanasota. Kumbuka hii ni fani adimu kuliko zote TZ kwa wakati huu.

Fani nyingine hazijakumbukwa kabisa, hii inamaana kuwa zaidi ya wahitimu 40,000 katika fani mbalimbali wapo mtaani wamekata tamaa ya kupata ajira. Maendeleo yazungumzwayo kama Ununuzi wa ndege, ujenzi wa barabara, SGR, St Gauge bado si jibu kwenu. Kimsingi kila mmoja hulia na shida zake, ni wakati wa kujiuliza hivi maendeleo yote akina POLEPOLE wanayoyapigia debe yamekusaidia nini wewe binafsi?

Ushauri wangu kwenu msioajiliwa. Huu ni wakati muafaka wa kuja na siasa mbadala zitazowaokoa kutoka mtaani na kukuza vipaji vyenu katika fani zenu. Kama chama tawala hakijawasaidia, si wakati tena wa kuimba mwimbo huo huo usiokupatia mafanikio yeyote.

Jibu la matatizo yenu lipo katika maamuzi magumu ya kisiasa. Anzisheni harakati maalum katika chama chochote cha upinzani utachoona kitawasikiliza na muendeshe hoja za msingi zitazowakomboa. Mkibweteka hamtaweza kutatua matatizo yenu, mkibaki kulia tu na kuitwa wazururaji. COME ON VIJANA WAKATI NDIO HUU.
 
Back
Top Bottom