Msioajiriwa kwa wahitimu wa Chuo Kikuu mna nini cha kuisifu awamu ya 5?

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Posts
4,367
Reaction score
2,407
Dhana kuwa awamu ya 5 imeleta maendeleo pengine maneno haya ni magumu kuyaelewa kwa kijana aliye na shahada ( degree) ya chuo kikuu na yupo mtaani hajapata ajira kwa miaka kati ya 4 mpaka sasa.

Kwa maneno ya Rais mwenyewe (mkutano na chama cha madaktari) alikiri kuwa madaktari 2700 wapo mtaani bila ajira. Akaahidi kuajiri 1000 ahadi ambayo kaitimiza hivi punde. Hii inamaanisha kwamba madaktari 1700 bado wapo mtaani wanasota. Kumbuka hii ni fani adimu kuliko zote TZ kwa wakati huu.

Fani nyingine hazijakumbukwa kabisa, hii inamaana kuwa zaidi ya wahitimu 40,000 katika fani mbalimbali wapo mtaani wamekata tamaa ya kupata ajira. Maendeleo yazungumzwayo kama Ununuzi wa ndege, ujenzi wa barabara, SGR, St Gauge bado si jibu kwenu. Kimsingi kila mmoja hulia na shida zake, ni wakati wa kujiuliza hivi maendeleo yote akina POLEPOLE wanayoyapigia debe yamekusaidia nini wewe binafsi?

Ushauri wangu kwenu msioajiliwa. Huu ni wakati muafaka wa kuja na siasa mbadala zitazowaokoa kutoka mtaani na kukuza vipaji vyenu katika fani zenu. Kama chama tawala hakijawasaidia, si wakati tena wa kuimba mwimbo huo huo usiokupatia mafanikio yeyote.

Jibu la matatizo yenu lipo katika maamuzi magumu ya kisiasa. Anzisheni harakati maalum katika chama chochote cha upinzani utachoona kitawasikiliza na muendeshe hoja za msingi zitazowakomboa. Mkibweteka hamtaweza kutatua matatizo yenu, mkibaki kulia tu na kuitwa wazururaji. COME ON VIJANA WAKATI NDIO HUU.
 
Haijawi kutokea duniani kila anaemaliza chuo anaajiriwa serkalini

Jiongeze tu brother

Kama sio wote wataopata ajira, hivi kwa mtazamo wako asilimia ngapi ya wahitimu wapate ajira ili useme tunaendana na matarajio ya wahitimu wetu vijana. Kumbuka wengi wao wana mikopo, umewahi kujiuliza kuwa watailipaje?
 
Ndio maana nimesema watapata ajira lkn sio wote

Kama sio wote wataopata ajira, hivi kwa mtazamo wako asilimia ngapi ya wahitimu wapate ajira ili useme tunaendana na matarajio ya wahitimu wetu vijana. Kumbuka wengi wao wana mikopo, umewahi kujiuliza kuwa watailipaje?
 
Nani alikwambia ukimaliza chuo lazima upate ajira
Nilitengemea utasema tupeni mda tubadili mtaala wa elimu, lakini kwasababu ya kutokuwa frika hiyo uwezi elewa.

Maana uwezi kuwa na watu wasomi kama kabudi, n.k ukatengemea utaelewa nini Maana ya ajira

Yani tuna vyuo kibao lakini tunavyazo vya maji chumvi,eti wanachindwa kuyatakaza yasiwe na chumvi. Narudia uwezi kuelewa nini Maana ya ajira
 
Mkuu hutaki kabisa tren ee! Huoni huo ni ubinafs kwa wakulima na wafanyabiashara ?
Hata madaktari mmeshindwa kuwaajiri? Mnaajiri madr 45%.
Mnatupigia makelel treni sjui makonda.
Pumbavu
 
Serikali huajiri kulingana na uhitaji, ulitegemea hayo Malaki ya wahitimu wote wangeajiriwa serikalini?

Tuacheni tupotoshana upumbavu, nitaona la maana kwa mtu atakayehoji kwanini watumishi wa umma hajaongezewa mishahara au kupandishwa madaraja! Yes the government is answerable for this!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini tren itarahisisha maisha ya mkulima na mfanyabiashara pia
KWa nini hamtaki kujiri madokta? Potele mbali hizi fani zingin tushajua uwezo wenu umefika mwisho ila madokta msiwaache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…