Msioajiriwa kwa wahitimu wa Chuo Kikuu mna nini cha kuisifu awamu ya 5?

Jamani tatizo la ajira kwa wana vyuo duniani ni "shida ya Dunia" sio hapa tu Tz. Labda waalimu wajaribu kutunga mitiani migumu ili wanafunzi wasipass.
 
Awamu ya tano imewekeza nguvu nyingi sana kwenye kubambikia watu kesi na kutumia nguvu nyingi ili isifiwe.
 
Hakuna hata maendeleo zaidi ya maigizo, JK aliajiri kila mwaka zaidi ya watu elfu 20, kupandisha mishahara, ujenzi wa hosps(B.Mkapa, Mloganzila, MOI), vyuo Nelson Mandela, Udom nk, barabaraq za kutosha(lami), madaraja(Kingamboni na Mkapa), ofisi za kisasa za Mikoa na Wilaya, bei ya mazao juu na mengine mengi lakini hatukuona mbwembwe hata kidogo,
 
Jamani tatizo la ajira kwa wana vyuo duniani ni "shida ya Dunia" sio hapa tu Tz. Labda waalimu wajaribu kutunga mitiani migumu ili wanafunzi wasipass.
Kwa nini JK alikuwa ana ajiri zaidi ya watu elfu 20 kila mwaka?
 
Sisi kwa sasa tunatekeleza
 
Mhe. Mtaka (RC Simiyu) kama angekuwa Waziri wa Kazi au Waziri wa Ajira ana open mind on how we can arrive towards the solution of generating opportunities za kutengeneza kazi au kama ni kujiajiri aje na mtu with a working model
Your browser is not able to display this video.
 

Mbwembwe ndio zinazouwa TAIFA. Na bahati mbaya baadhi ya watanzania sio wengi pengine ni 10% wanazishabikia mbwembwe kwa ajili ya matumbo Yao.

Kama tuko makini na tunataka kutoka huko, ni lazima tuwaokoe hawa mafahari wa mbwembwe. Umejenga kisima cha maji, unakwenda kufungua na umati wa viongozi - Mkurugenzi, mbunge, waziri na mkuu. Jamani hii nchi ina watu milioni zaidi ya 50.
 
Awamu ya tano imewekeza nguvu nyingi sana kwenye kubambikia watu kesi na kutumia nguvu nyingi ili isifiwe.

Hii ni ishara ya mtu aliyeshindwa na badala yake anatumia nguvu alizokuwa nazo kimadaraka. Ni dhambi kubwa sana, haitamuacha mtu yeyote anayehusika na dhambi namna hii bila adhabu. Tena hapa hapa duniani.
 
Chama kipi? Unataka wakanyanyaswe kingono na boss wa CHADEMA? Usiwinde shida za watu kuwafanyisha wasiyoyataka bhana!

Vyama vipo vingi si CHADEMA tu. Ukiona CHADEMA kwako haifai, achana nacho nenda NCCR, kama nao una walakini nao kuna CUF, ukiona LiPumba myeyusho kuna ACT ni maono yako tu. Mwisho wa siku ni nyie vijana ndio mtaobadili mtazamo wa hao viongozi.

Ni rahisi kubadili mtazamo wa viongozi wa chama chochote cha upinzani kuliko chama Tawala. Huko wako hivyo hivyo, hawabadiliki kamwe.
 
Jamani tatizo la ajira kwa wana vyuo duniani ni "shida ya Dunia" sio hapa tu Tz. Labda waalimu wajaribu kutunga mitiani migumu ili wanafunzi wasipass.

Kwahiyo ni ugonjwa usiokuwa na dawa! Au unataka kusema nini? Kifupi Siasa ni sayansi iliyojikita katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya watu. Kama wewe unajiita mwanasiasa na huna jibu la matatizo ya wananchi wako, ni bora utafute kazi nyingine kwani hii ya SIASA imekushinda.

Tafakari na ujaribu kuliangalia tatizo hili kama linalowezekana kupata uvumbuzi ili uwe umepevuka kisiasa.
 
Awamu hii imekuwa hostile na segregative na education imebaki ile ile traditional knowledge based hasa vyuo vikuu. Ni tatizo kubwa sana na Tanzania graduate wake hawatoki nje ya nchi kutafuta fursa tofauti na wakenya na waganda, Mungu atusaidie sana, umakusudi na misifiri g kwenye ishu pertinent imekuwa utamaduni.
 
Tumesha waona wajinga nyiny kila mwaka watu wanamaliza chuo mkitaka wote waajiriwe mnawawrka wapi
 
Tuna DJ na pia tuna saccos, hivyo Maisha yanaendelea
 
Hajasema walokosa ajira za serekali, bali walio kosa Ajira kwa ujumla wao. Kujiajili na kuajiliwa sekta binafsi kunategemea sana sera za serekali.
 
Hata Iddi Amini alikuwa na watu wengi hivyo usishangae
 
Hivi ni mabadiliko gani ambayo ungependa yafanyike CCM lakini hayafanyiki na sasa yanafanyika CHADEMA, CUF, NCCR, n.k.? NI yapi? Kuna kiongozi gani upinzani unayemtumaini kufanya mabadiliko? Hawa akina Mbowe, Zitto, Mbatia, Mrema, Lipumba, nk. Unawaona ni watu wa kutawala nchina ikaonesha mabadiliko. Hawa wanaokimbilia kushitaki nje ya nchi utadhani tunatafuta uhuru leo hii?
 

Ukitaka kujua nguvu ya upinzani angalia jinsi CCM bila siri inakiri kuwa waliyoyapigia kelele wapinzani huko nyuma ndio Chama tawala inatekeleza. Hili si dogo ni kubwa sana kwani huko nyuma madude yaliyoyokuwa yanafanyika ndani ya serikali yalikuwa hayaweki hadharani, kwa kisingizio kuwa hayo ni mambo ya siri za ndani. Milinga aliharibu ATC - Adhabu yake eti kupewa ukuu wa mkoa Mara. Jamani hawa watu wametutesa!!!!

CCM ni sikio la kufa, halisikii dawa. Kufanya mabadiliko haiwezi kamwe. Kinachofanyika si strong party bali ni strong man. Usiponiamini subiri mkuu aondoke, sera zote zitakifa na kuendelea na bussiness as usual.

Kila rais aingiae madarakani haishi kumkosoa aliyepita/waliopita na yeye (mpya) kuanza upya. Ukianza upya kila baada ya miaka kumi, huna mabadiliko wewe. Hata nia ya mabadiliko huna ila ulikua unalilia tumbo lako kwa slogans za kinadharia tu.

Licha ya kuuponda upinzani, lakini moja wanalo - Kuwainua vijana ili iwe sauti ya umma kesho na keshokutwa. Na vijana ndio wataoleta mabadiliko sio Mwenyekiti. Ukitumia muda mwingi kulilia Mbowe unapoteza muda wako, ongeza mawazo yako na fikiri nje ya box.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…