Uchaguzi 2020 Msipompitisha Lissu watampigia Membe, msipompitisha Membe watampigia Rungwe, msipowapitisha wote raia watasusia uchaguzi

Joined
Feb 18, 2019
Posts
53
Reaction score
539
Tunawaambia ukweli kabisa, ili mnapofanya maamuzi yenu mkae mkijua raia wamechoka na hizo ndizo options walizonazo.

Kimbilio la wengi kwa sasa ni Lissu. Ila kwa sababu kuna kila dalili ya kukatwa, basi option ya pili waliyonayo raia ni Membe. Mkimkata na yeye raia wanaona ni bora hata wampe Hashim Rungwe sababu angalau kwa mbaali ana uchungu na hali zao.

Mkiwakata hao watatu basi mjue uchaguzi utakuwa ni wenu peke yenu na watu watakuwa washafunga mahesabu hawana hata haja ya kusubiri hata hiyo Oktoba.






 
[emoji38] [emoji38] jf na uhalisia mtaani.

leo nikiwa kwenye daladala, mkuu mmoja akaanzisha mada kuhusu upinzani tz(kisa ilikuwa foreni). daladala zima kimyaa anasikilizwa yeye. alipochomekea uwezi wa jpm dhidi ya lissu watu karibia gari zima wakaanza kumpayuka.

huyu rais aachwe, asihusishwe na upuuzi wowote, lissu anatafuta huruma nk. yaani nikawaza mambo kadhaa.je jamaa kama alikiwa akipima upepo ameondoka na ujumbe gani!!!
 
Sitoshangaa baadhi ya majina ulotaja yakakatwa kwenye urejeshwaji wa fomu za wadhamini keshokutwaa

Hakidhi/hawakidhi vigezo 😎😎
 
Watu wanaogopa kukamatwa mzee hakuna freedom of speech ata ningekuwa umo ningefanya unafiki ndiyo tunavyoenda sikuizi bro
 
Wajumbe wabaya sana, usiwaamini wajumbe hata siku moja.
 
Watu wanaogopa kukamatwa mzee hakuna freedom of speech ata ningekuwa umo ningefanya unafiki ndiyo tunavyoenda sikuizi bro
ukamatwe na nani, kama wangelikaa kimya una hoja ya msingi.

lakini sio kumvunja moyo mwenzao wanayefanana naye itikadi, hata kwa kumpa ujumbe kwamba tunaogopa tu, ila tuko pamoja nawewe.
 
Enjoy your moment kamanda!
sio vizuri kuwakatisha tamaa watu, hasa ukizingatia kuwa hata wanaCCM wanaenjoy comedy zake.
 
ukamatwe na nani, kama wangelikaa kimya una hoja ya msingi.

lakini sio kumvunja moyo mwenzao wanayefanana naye itikadi, hata kwa kumpa ujumbe kwamba tunaogopa tu, ila tuko pamoja nawewe.
Hakuna mda watanzania ni wanafiki kama wakati huu washamsoma bro anapenda kuabudiwa
 
Rais ni mmoja tu. JPM
 
Mwenyekiti wa Tume asikibali kitumiwa, atende haki kwa mujibu wa sheria za nchi; Taifa likivurugika wa kwanza ni yeye!!
 
Wasipompitisha Lissu nchi italipuka moto.
 
Hii stori mbona ata hainogi Kama huna nyingine nyamaza maana akuna kitu kinaitwa foreni tz.
 

Wakimkata Lisu huo uchaguzi utakuwa na wapiga kura wachache kuwahi kutokea nchi hii. Wagombea wote kuanzia Magufuli, Membe nk hakuna mwenye mvuto wa kuvuta wapiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…