GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Nashauri tu bora 'wasipeleke' Timu yao.Hiyo ndio inaitwa Mbele moto nyuma moto Au Ugali wa moto, mboga ya moto.
ππ
Ni hii ambayo unaikwepa kwepa kila siku. Nasikia hata gemu na biashara nusu fainali mtajifungisha ili kukwepa dhahama kama ile ya nusu fainali last season. Ila kitu kimoja mjue kuwa kifo hakikimbiwi, kitakufuata popote ulipo.Simba mnayoizungumzia ni ile iliyopigwa miguu ya sturi kule sauz? Au ile iliyofungwa na Prisons pamoja na Ruvu shooting?
Daima mbele nyuma mwiko...uchawi upoMwendo mchubuyu π π π
Ukisimama nchale ukikaa nchale.Hayati Rais Mstaafu 'Genius' Benjamin William Mkapa aliwahi kusema kuwa Siku zote Kupanga ni Kuchagua.
Mna Maamuzi mawili tu ya ama msipeleke Timu katika 'Derby' ya tarehe 3 July, 2021 ili Kanuni zifuatwe na Simba SC apewe alama (points) 3 na Goli 3 atangazwe 'Bingwa' rasmi.
Au muamue kupeleka Timu ila mjue kuwa mnaenda kukutana na dhahama ya Kufungwa Goli 5 kwa 0 na Simba SC Kisha 'Ubingwa' unatangaziwa Kwenu na 'Kipigo' mlichokipata.
Ninasisitiza tena Kupanga ni Kuchagua.
Simba punguzeni vitisho,watagoma kweliNi sawa na uambiwe kuchagua kati ya Kufa au Kufariki.
π π
Msikie huyu mtopoloSimba wamepoteana awajui Yanga wanataka kufanya nini na hivi ndivyo Yanga walivyo wazuri ki mkakati. Kwasasa Yanga wanajua kila kinacho endelea ndani ya Simba Ila Simba awajui Yanga wanataka kufanya nini na hii ndio imekua njia ambayo Yanga imekua iki idhibiti Simba kwa Sasa.
Na ndo iliyoweka rekodi ya kukutungua 5_bilaSimba haijawahi kuwa tishio kwa Yanga, Simba ndio timu iliyofungwa na Yanga maranyingi zaidi kuliko timu yoyote apa Tanzania. Simba ndio timu dhaifu kwa miaka mingi katika timu ambazo zimejaribu kuleta upinzani na Yanga.
Simba ndio timu yenye mchecheto zaidi na ndio iliyoweka rekodi ya kung'oa viti baadaya kufungwa na Yanga.