Msishangae Diamond siku baba yake akifa akaandaa mazishi ya kifahari

Msishangae Diamond siku baba yake akifa akaandaa mazishi ya kifahari

Kuna mambo kamwe hauwezi kuyaelewa mpaka utakapokuwa Baba na kuyapitia. Sikatai ya kwamba Mama zetu huwa wanapitia changamoto nyingi katika ndoa,mahusiano na malezi ya watoto, ila kuna mengine husababiswa na wakinamama. Haswa unapoona baba anaamua kuondoka na kuendelea na maisha yake huwa kuna mengi sana nyuma ya pazia. Kwa kuwa jamii yetu imejikita kuwatetea na kuwabeba kinamama ndio maana kina Baba huwa wanaonekana kavu sana.
Mwisho wa siku kwa haswa kwa sisi watoto wa Kiume huwa tunakuja kuwaelewa mababa zetu kwa kina zaidi pale tunapokuwa kwenye Taasisi ya Ndoa na Ubaba wa familia. Mifano iko mingi tu.

Ndio Maana katika Amri kumi za Mungu namba 4 huwa inasema "Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako." Haikumtaja mama peke yake wala kusema baba aliyekulea na kukupa matunzo, bali imemtaja BABA na Mama.
Tunaangamia kwa kukosa maarifa.
unachosema ni kweli lakin mama hatakiwj kukufanya uwasahau watoto. Mtoto ukimpa mapenz ya kweli hata upokosekana hakai kwa aman. Sasa mfano wewe ni baba yangu mzazi umegombana na mama. Nakufuata baba naomba unisaidie hela ya ada unanichunia unategemea nitakupenda. Au nyumban tunashinda njaa ila kila siku tunasikia uko bar unagawa offer unategemea tutakupenda? Ukweli uliopo ni wanawake wachache ambao watamfundishwa mwanao ampende babake ila walio wengi watataka watoto wote wawe upande wao iwe kwa jema ama kwa ovu. Kwa hivyo ni jukum let kina baba na sie tujue ni kwanamna gani tutawalazimisha watoti wawe na mapenz nasi hata pale inapotokea tumeachana basi penzi la mtoto liendelee kuwepo
 
baba baba tuu mkikua mtajua thamani yake!!
long time dingi alkua nandunda had nkamchukia nkimuomba ela ya daftari ananambia sina na nnajua anazo.... mambo n mengi ila asaiv siezi mwacha adhalilike kwan naanza kudhalilika mie then family

na wamama punguzeni kuwalisha sumu watoto.. baba yenu ivi baba yenu vile....
m hata simshangai diamond namlaumu mama ake
 
Baba ni baba haijalishi ubaya wowote alokufanyia,mzazi atabaki kua mzazi wako tu pengine kama si baba ake kukytana na mama ake diamond unadhani angekua nani au wapi??
kuna wazaz wamewaumiza watoto wao mpaka basi. Ukiwa umetokea kwenye familia yenye maelewano huwez elewa kinachozungumzwa.
 
Ni Waislam, uzinzi una hukumu yake lakini si kigezo cha mtu kuto kuwa Muislam.
Kwani waislam wanaishi na wanawake ambao hawajawaoa kwa ndoa ya kiislam??ni waislam kweli hao!!
 
Hapo mama ake anachangia kias kikubwa mwanae asiwe na maelewano mazuri na baba yakr, hata kama wamtengwa kiasi gani hajaondoa uhalisia kua yule ni baba yake wa damu kabisa bado ana nafas ya kumsamehe wakaanza upya, ikiwa tumeamriwa kusamehe waliotukosea na Mungu mwenyewe tunamkosea mangapi na bado unaomba toba unasamehewa ije kiumbe mwenzangu??
kuna wazaz wamewaumiza watoto wao mpaka basi. Ukiwa umetokea kwenye familia yenye maelewano huwez elewa kinachozungumzwa.
 
Sasa kama baba aliwatenga yanini kumshobokea sasa hivi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wanawatafuta baba zao (hata kama mama zao walibakwa) ili angalau wawafahamu. Baba ni Baba tu, bila mbegu ya huyo "aliyewatenga", huyo star tungemjulia wapi? Kila jambo hutokea kwa makusudi ya Mungu. Mwambieni Diamond amthamini BABAAKE!
 
Kuna mambo kamwe hauwezi kuyaelewa mpaka utakapokuwa Baba na kuyapitia. Sikatai ya kwamba Mama zetu huwa wanapitia changamoto nyingi katika ndoa,mahusiano na malezi ya watoto, ila kuna mengine husababiswa na wakinamama. Haswa unapoona baba anaamua kuondoka na kuendelea na maisha yake huwa kuna mengi sana nyuma ya pazia. Kwa kuwa jamii yetu imejikita kuwatetea na kuwabeba kinamama ndio maana kina Baba huwa wanaonekana kavu sana.
Mwisho wa siku kwa haswa kwa sisi watoto wa Kiume huwa tunakuja kuwaelewa mababa zetu kwa kina zaidi pale tunapokuwa kwenye Taasisi ya Ndoa na Ubaba wa familia. Mifano iko mingi tu.

Ndio Maana katika Amri kumi za Mungu namba 4 huwa inasema "Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako." Haikumtaja mama peke yake wala kusema baba aliyekulea na kukupa matunzo, bali imemtaja BABA na Mama.
Tunaangamia kwa kukosa maarifa.
Point. Jamii imezoeleka kumwona baba ndo kavunja mahusiano kwenye ndoa. Ila ukweli ni kwamba kuna wanawake wengine huku duniani hawakuletwa kuolewa, najua wengi mtalipinga hili ila simlazimishi yeyote akubaliane nami. Sio kila mwanamke afaa kuwa MAMA! Ila kwa wanaume walio kwenye ndoa muda mrefu kwa asilimia kubwa wanatunza ile heshima ya ubaba kwa watoto wao, hawapendi kuwaona watoto wao wakimkosa mama yao ndo maana wanaendelea ku share chumba. Sikatai kuwa wapo pia wanaume wasiojitambua ila si jukumu au sahihi la mtoto kumrithi adui wa mamaake au babake. Hayo si yake bali ya wazazi wenyewe. Kids need to be neutral kwenye magomvi ya wazazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hapo ndio anapokosea kama amemkubali baba ake kwa uwezo alokua nao anashindwa nn kumsaidia? Halaf uislam umetuusia kuwatendea wema wazaz wawili tena na kuwaombea maghfira kabisa kama ameweza kujua umuhimu yule ni baba ake bas s amsaidie tu tayari kosa kafanya baba ake huko kukimbia na vyote lakini mama ake pia kashindwa kusema na mtoto wake?? Ila sishangai kwa zinaa anazofanya mwanae na akawapokea kila mwanamke anaekua na mwanae atashindwa kufitini mtu na baba ake wasipatane?
Kwani diamond kamkataa baba yake au hataki tu kujiusisha nae......kwani dingi alipokua kakimbilia kuishi katoswa au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond=MamaDiamond+BabaDiamond kwa hiyo haijalishi Baba kafanya nini kwa kuwa alishiriki katika kumuumba lazima apate heshima yake Mambo mengine ni kumuacha yeye na Mungu Ndo mwenye Kisasi
Ni kweli kabisa na hapo ndipo unafiki wa waliowengi utakapo jionyesha.

Ila wapo watakaopinga

Ehee ndio hivyo jinsi watu wanavyokukimbia wakati wa kuumwa ndivyo jinsi watakavyokuja kwa wingi kukuchangia hela ya geneza na sanda na wakaweka pombe na vyakula vya anasa msibani mwako

Ndio huyu Diamond msishangae siku baba yake akitangulia mbele za haki akatumia hata milioni hamsini 50 kwa shuhuli ya mazishi, na akafanya yawe ya kistar, naona siku hiyo viongozi wakubwa watakuja na wasanii watakuja, lakini akiwa hai hata kumsikia hataki kumsikia

Hii ndio dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
Acheni kufuatilia mambo ya watu, watoto siku zote hata tukikuwa kuna mzazi mmoja unamzoea kuliko mwingine kutokana na mazingira uliyolelewa na ndio maana hata kwenye familia zetu kuna wengine akiwa na tatizo analifikisha kwanza kwa mzazi mmoja then linafika kwa mzazi mwingine...kuna watu wamelelewa na wajomba na wa mama wadogo na wamejikuta wamewazoea zaidi waliowalea kuliko wazazi wao halisi lakini haina maana kwamba wanawachukia wazazi wao.

Kwa waliobahatika kulelewa na wazazi wote wawili hawawezi kumwelewa Diamond ila kama mtu alilelewa na upande mmoja kutokana na wazazi wa kutengena watamwelewa', lakini mwisho wa siku mbona ametumia na ubini wa mzee wake na bado anajitambulisha kupitia ukoo wa baba yake

Maisha ya mtandaoni tusiyafuate sanaaaaa maana huwa tunawapost watu tulionao karibu japokuwa tuna watu wengi tu wengine tunawapenda na kuwajali (mfano mdogo tu kwenye social network unakuta watu wameoana na unakuta anawapost watoto ila mke hampost
 
Sijawahi kusikia "mazishi ya kifahari" kwa Waislam.

Halafu nakushauri kuwa wachana na mambo ya kufatilia ya watu, huyajuwi. Wewe fata yako na familia yako. Ya Diamond na familia yake yatakusaidia nini?

Unajuwaje nani atatangulia?
Msamehe mwanga huyo anadhani waislamu Wana mazishi ya kifahari na mijeneza ya bei mbaya .Mchawi huyo anamuwangia kifo Mzee wa watu
 
Mambo tunayopitia wakina Baba na watoto wetu ni mazito sana. Watu wengi wanashindwa kuyaelewa kwa sababu wanayachukulia na kuangalia juu juu tu. ukiyaangalia kwa kutumia mtazamo tofauti utapata uelewa na masikitiko makubwa. Wengi wetu tumepitia haya au kushuhudia katika familia zetu zikipitia hizi changamoto za kulelewa na mzazi mmoja (Mama). God bless Our African women...strong Women on the Planet Earth.

Moja ya magwiji wangu pendwa wa muda wote Mr. Sean Carter aka Jay Z alipitia hizi figisu enzi za utoto wake na alipoanza harakati zake za Music aliandika baadhi ya nyimbo kadhaa akimponda sana Baba yake Mzee Adnis Reeves kwa maneno makali na hisia Kali sana.

Moja ya nyimbo hizo iliitwa "Where have you been". Nakumbuka nilikuwa nasafiri kutokea Washington D.C kuelekea Atlanta nikiwa ndani ya rental car niliweka hiyo track on repeat. Nilisikiliza kwa makini sana Jay alivyokuwa anatoa nyongo ya uchungu kwa Baba yake.
Moja ya mistari Jay alifoka akisema "And smoke Newports just like you
But you left me, now I’m goin to court just like you
I would say “My daddy loves me and he’ll never go away”
Bullshit, do you even remember December’s my birthday?"

Juzi kati Jay baada ya kupevuka kiumri na kuwa Baba alitoa album inaitwa 4:44 ikiwa na bonus track ikiitwa Adnis (jina la baba yake).
Katika moja ya Interview zake on Tidal Jay alisema haya "All my songs up this point have been about anger with my dad. Like, ‘You left and I didn’t see you for all these years and you don’t mean shit and I don’t https://jamii.app/JFUserGuide with you.’ As an adult, I look back on the situation and I have a different perspective on it. My dad married my mother at a time when everyone was leaving. He tried. My mom had four kids by 20, I was her youngest child. They were young… That don’t check the box of somebody that wasn’t shit. He married this woman with four kids and they was together for 11 years. So now the story gets different, because you wasn’t the scumbag who just broke out. What happened to you?"

Na moja ya vibao vyake nilivyotokea kuvipenda sana na kuvielewa inaitwa "Moment of Clarity"... Jay alisema haya "So pop, I forgive you for all the shit that I lived through
It wasn’t all your fault, homie, you got caught
Into the same game I fought, that Uncle Ray lost
My big brothers and so many others I saw"

Shout out to all the Pops out there......you are appreciated.
One love...
Am out.
 
Hapo mama ake anachangia kias kikubwa mwanae asiwe na maelewano mazuri na baba yakr, hata kama wamtengwa kiasi gani hajaondoa uhalisia kua yule ni baba yake wa damu kabisa bado ana nafas ya kumsamehe wakaanza upya, ikiwa tumeamriwa kusamehe waliotukosea na Mungu mwenyewe tunamkosea mangapi na bado unaomba toba unasamehewa ije kiumbe mwenzangu??
Ndio kuna nafasi ya kusamehe inatakiwa asamehe. Kwa diamond itakuwa ngumu maana kuna mamake ambae kiukweli hawez ruhusu hilo analokosea diamond ni kusimama na manake tu, unaweza kuta mpaka baba diamond anaondoka labda bibie alikutwa na kidume ndani. Sasa ishu iliyopo inasemekana wakat domo yuko seco alikuwa akimfuata mzee anamjibu mbovu hapo ndo maumivu yanazidi. Kiujumla mama anachangia diamond ashindwe samehe. Kuna interview moja nilisikia kipind domo yuko na wema. Wema alikuwa na tabia ya kwenda kwa mzee kusalimu. Nadhan kwa upande mwingine nahisi wema alicheza pati yake kumuunganisha nababae na lait wangeendelea nahisi angesamehe.
 
Tatizo watu wanamwangalia Diamond alafu wanamwangalia baba yake anavyoishi ambapo kimsingi anaishi maisha mazuri kulingana na vigezo vyetu vya kitanzania ila wanataka ajenge bungalow kali sana alafu ampatie. Maisha ya familia za wengine tuyaache tufanye yetu, humu wengi maisha tunayoishi kama kila mtu atamwonyesha mzazi wake, tutajikuta tunashangaana hapa
 
Back
Top Bottom