Kuna jamaa yangu kaamua kuachana na mwanamke wake, kaamua kuachana na mtoto, hatoi huduma wala chochote kaamua kuanza maisha mapya kaoa mke mwingine na ana mimba
Hayo yote ni baada ya kuchoshwa na mbilinge, fedheha, dharau na mambo kedekede ya mke wake ambayo tumeyasuhudia
Na si kwamba hampendi mtoto lakini amepima kati ya kuendelea kuwa karibu na familia yake akaja kuishia pabaya ama kujitenga kipi afadhali
Kesho na keshokutwa mtoto bila kujua sababu ni nini na baada ya kulishwa sumu na mama yake atakuja kumchukia baba yake
Mimi binafsi sijawahi kuhukumu kwa haraka mababa wenye kadhia kama ya baba yake na diamond ni mpaka ujue sababu
Hakuna kichaa atatelekeza tu watoto bila sababu ya msingi labda awe karogwa
Kwa akili ya mama diamond huwa nafikiri huenda yeye ndio alikuwa sababu
Kuna wengi hasa vijana ambao bado ndoa kwao ni msamiati hawaelewi haya mambo
Mheshimiwa Makonda alizua sekeseke la kusaka baba waliotelekeza watoto wao, nafikiri kwa asilimia kubwa tulijionea aina ya wanawake waliojitokeza
Mwanamke anaongea mpaka mic inalowa mate