Msomi Nguli wa Sheria Prof. Palamagamba anaenda kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo? Atakataa!

Masayuni alistahili kwenda kulima karafuu huko visiwani.
 
Muda wa kupumzika, kufuga kuku na kulinda heshima yake sasa, sio lazima awepo kwenye kila cabinet.
 
hapana bado atafanya vizur.kwanza prof anaipenda historia na malikale.bahat mbaya tu atakuta kuna confusion ya utamaduni na heritage per se. ila kwa kuwa wakil msom still anafaa hapo kwanza kuihabarisha jamii juu ya vitu mbalimbal na uhalali wake kisheria. pamepata mwenyewe hapo. by the way kwan yeye ndio mtendaj mkuu.?
 
sasa si amuondoshe tu kuna mamlaka ukifika hakuna tena aibu, penye kuondosha unaondosha tu
Very very true. Kiongozi ni myu ambaye anafanya maamuzi magumu...ata ikibidi kuua mtu kwa manufaa ya wengi
 
Uwenda akawa kwa Muda,kuwanoa walio kuwepo.Aysee CCM inamipango kabambe sana...
 

Token jalalani halafu halafu ukatae Uwaziri. Maybe it's not Tanzania tuijuayo.
 
Moja ya Wizara za hovyo.
 
Ukishakiwa mtu wa jalalani na kutolewa huko popote tu unaenda
 
Tena mzee wetu apewe na viboko, wakizingua kina Chino wanaman ni kuwatembezea bakora
 
Tanzania kila kitu kinawezekana hata Kingwendu anaweza kuwa rais.

Unafikiri kuna nchi inayojielewa Samia angewahi kuwa hata makamu wa rais achilia mbali urais wenyewe?
 
Huyu mtu atafanya nini cha maana kwenye wizara kama hiyo! Hii nchi yote kweli haina mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi kwenye wizara kama hiyo?
 
Hii inanikumbusha Prof. Sarungi naye mtaalamu wa mifupa alishawahi teuliwa nafasi hiyo hiyo.
Lakini Sarungi alifiti sana kwenye nafasi hiyo. Kwanza utaalamu wake wa mifupa ilidhaniwa itasaidia kwenye michezo. Pili, Sarungi kwa tabia zake zile za kusema sema sana, kwenye mambo ya michezo na sanaa inakubalika sana. Tatu, Sarungi alikuwa ni Shabiki mkubwa wa Simba; kwa hiyo michezo halikuwa jambo geni kwake.
Sasa huyu Kabuti; Michezo, Sanaa, Utamaduni...; wapi na wapi?
 
Nakubaliana nawe, lakini hebu kwanza angalia ujuha unao fanyika: pamoja na kuwa na uzoefu wa kushika nyadhifa za uwaziri kwa muda mrefu, na kuwa mtaalam wa mambo ya sheria; katika muda huo mfupi wateuzi wake kweli wameweza kufanya tathmini ya mambo aliyo weza kufanya na aliyo shindwa kuyafanya na kuamua kuwa hafai kwenye nafasi hiyo?
Hawa watu wana teuliwa, hata kabla hawajatulia kwenye nafasi mpya walizo teuliwa, hapo hapo wana tibuliwa na kupelekwa eneo jingine wakaanze upya!
Nani hufanya kazi namna hii halafu upate mafanikio.

Jambo la kujiuliza ni kama wateuliwa hawa hupewa na kuelezwa malengo wanayo takiwa kuyafikia katika muda maalum wa kazi zao (Performance Indicators). Je, huyu Kabuti kashindwa kufikia malengo aliyo pangiwa katika muda mfupi huo, au kuteuliwa ni basi tu kujaza nafasi wizarani?
 
Kabudi kutoka kuzungukwa na kuongea na watu wa maana kama mabalozi sasa anazungukwa na akina shishi na steve.................................... na chino man.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…