Msomi ni nani

Msomi ni nani

Msomi ni mtu aliyepitia mfumo wa formal education na kufikia kiwango fulani cha elimu,lkn mtu mwenye elimu yuko free either elimu yake kaipata kupitia formal education or informal education.....there fore neno msomi liko ndani ya mwenye elimu...
 
"Si kila mwenye elimu ni msomi lakini kila msomi ni mwenye elimu" na "Elimu haina mwenyewe ila ina watu wake"
 
Msomi ni mtu aliyepitia mfumo wa formal education na kufikia kiwango fulani cha elimu,lkn mtu mwenye elimu yuko free either elimu yake kaipata kupitia formal education or informal education.....there fore neno msomi liko ndani ya mwenye elimu...
mkuu umeondoa utata
 
Elimu ni ya Yesu.Ukimjua Yesu basi wewe una elimu, Alikuwepo kabla ya Kuumbwa kwa Ulimwengu. Ref katika kitabu cha Yohana Mt, Hapo mwanzo kulikuwapo na NENO naye NENO alikuwa kwa MUNGU na vyote vilifanyika kwa NENO. So without NENO ambaye ni Kristo leo hii tusingejua chochote. Hata hiyo Physics, Biology, Psychology, Maths, Medicine and everything vimekuja baada ya neno.

Usomi ni kwa Mwanadamu.Tupo na Wahandisi,Wanasheria, Madaktari, Wahasibu, Wachumi nk. Neno Msomi limetokana na neno Soma. Na msomi wa kwanza Duniani ni Sauli ambaye baadaye alikuja kuwa Mtume Paulo.

Ndiye msomi aliyefanya kazi kubwa ambayo hadi sasa haijafanywa na yeyote na haitokaa ifanywe na yeyote.

I stand to be corrected.
 
Msomi ni mtu aliye soma akafika katika level fulani na kuwa na uwezo wa kuchanganu mambo. Mtu mwenye elimu ni yule aliyesoma na kufikia level fulani kisha akaenda kusomea taaluma.
 
Je !kwenda shule/chuo ukawa na sifa ya kumliki vyeo vya kisomi ndo unakuwa umeelimika au umesoma?

Hivi kwenda shule then ukaishi maisha ya umasikini je!unakuwa hujui kutumia usomi wako vizuri?

Leo nimeinamisha kichwa nikijiuliza maswali hapo juu na nikaona pia Wasomi ni zao la elimu na kupitia elimu tunapata wasomi,baada ya hapo kwa leo nimepata sifa mbili za wasomi wenye faida nakuzitazama katika jicho lifuatalo.

1.Wasomi ni wale wenye ari ya kuisaidia jamii kukua na kubadilika kimaendeleo(Nyenzo ya mabadiliko). zaidi ya hapo utakuwa ni usomaji na si usomi unaokusudiwa,na Kwa bahati mbaya sana asilimia kubwa katika sisi elimu tunayoipata tunalenga tu kujipatia mahitaji binafsi (private needs),mwisho wa siku inapelekea profesa au daktari nk. anaishia katika kadhia ya ufisadi.

2.Wasomi wanatakiwa wawena uwezo wa kufanya mambo ya sawasawa kwa namna ya sawasawa na kwa wakati wa sawasawa katika mazingira ya sawasawa(hekima),zaidi ya hapo ni msomi ambaye jamii itakuwa inapata hasara kwa usomi wake.

NB:Tunaweza kumtambua daktari mzuri kwa kupata matibabu na sio kwa mavazi ya udaktari,Tunaweza kumpata mpishi mzuri kwa kuonja chakula alichokipika japo sio kila kitu kizuri lazima ukipate kwa kuonja isipokuwa hata harufu nzuri inatosha,kwa namna kama hiyo tunaweza kutambua msomi mzuri kwa matunda yake.

(UTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO)
 
SIFA 50 ZA MSOMI...JITATHMINI KAMA UNAFITI.


  1. Msomi ni mtu mwenye uwezo fikra huru na mwenye uwezo wa kujitegemea.
  2. Msomi ana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
  3. Mtu mwenye elimu anajua jinsi ya kujifunza.
  4. Msomi anajua kuiandika na kuizungumza kwa ufasaha/usahihi lugha yake ya kwanza na lugha ya kujifunzia.
  5. Msomi anajua namna sahihi ya kutumia rasilimali zilizopo, kuimarisha mchakato unaohitajika ili ajifunze ujuzi fulani, na kujaribu njia zinazofaa.(my take: Hapa wale wanaokosa ajira angali ni wasomi wajitathmini).
  6. Msomi hufanya bidii kuepuka unafiki.
  7. Mtu mwenye ujuzi ana uwezo wa kuwasiliana/kuwasilisha mawazo yake au ya kitaaluma kwa maandishi, kwa uwazi na kwa ufupi; atabainisha chanzo cha ujuzi huo.
  8. Msomi ana uwezo wa kusema vizuri.
  9. Msomi ana uwezo wa kufikiria kwa uchunguzi na kwa kiasi kikubwa.
  10. Msomi ana uwezo wa kufikiria kwa hesabu za KUJUMLISHA,KUZIDISHA na KUTOA.
  11. Msomi ana ufahamu mkubwa juu ya Habari muhimu za Taifa lake,Kimataifa na nyanja za taaluma yake(Current Affairs). Sio tukuulize Profesa M. Assad ni nani hujui hapo tunakufuta usomi. Au nini kinaendelea Venezuela hujui. Tunakufuta.
  12. Msomi hakubali kwa upofu yale anayoambiwa; msomi huenda kuona/kushuhudia yeye wenyewe kile anachoambiwa(ataenda kuona ana kwa ana ama kwa utafiti tunduizi).
  13. Msomi anajua jinsi ya kutofautisha kati ya taarifa zinazofaa na zisizo (anatofautisha kati jambo muhimu na jambo dogo).
  14. Msomi anajua jinsi ya kufanya matumizi mazuri ya maarifa; anajua wapi atapata ujuzi ambao anauhitaji, na ana uwezo wa kuandaa ujuzi huo katika mpango wa utekelezaji unaoelekezwa mwisho wenye hatima chanya.
  15. Msomi anaelewa asili ya mwanadamu na ana uwezo wa kuanzisha, kudumisha, na kuboresha uhusiano wa kudumu na mwanadamu mwenzake.
  16. Mtu mwenye elimu anajua jinsi ya kuanzisha uhusiano na wengine(ku-establish rapport); anajua jinsi wengine wanavyomuamini na kumheshimu kwa sifa yake ya usomi(Si mjivuni kwa usomi wake).
  17. Msomi ana nidhamu (Katika kauli,mavazi,mahusiano,imani,taasisi na serikali).
  18. Msomi anajua jinsi ya kutatua migogoro na/ya wengine.
  19. Msomi anajua jinsi ya kuwashawishi wengine.
  20. Msomi ana uwezo wa kufikiria na kutatua matatizo.
  21. Msomi anajua jinsi ya kufanya maamuzi.
  22. Msomi anaweza kuvuka mipaka ya tahadhari na kuchunguza matatizo na kupata ufumbuzi wake kwa kutumia njia mtambuka.
  23. Msomi ni mtu ambaye amefundishwa kikamilifu: kiubunifu, kiutamaduni, kiroho, kimaadili, kimwili, teknolojia, na kiakili.
  24. Msomi ana elimu ya upana wa sanaa. Ana maoni mazuri ya masomo yafuatayo: sayansi ya asili; sayansi ya kijamii;hisabati; historia; jiografia; fasihi; falsafa; na teolojia.
  25. Msomi ana ujuzi wa kina-yaani, ujuzi maalum - katika fani fulani.
  26. Msomi amefanikiwa kushinda; anajua jinsi ya kufikia malengo muhimu ya muda mfupi na mrefu (Msomi si mtu wa kulia lia anatafuta suluhu kwani jamii inamtegemea atoe majawabu).
  27. Msomi ana uwezo wa kuvumilia na kuvumilia.
  28. Msomi anajitambua; anajua jinsi ya kuzisimamia hisia zake za ndani.
  29. Msomi ana maadili na huyazingatia kwa dhati.
  30. Msomi ana uwezo na nidhamu ya kufanya yaliyo sawa.
  31. Msomi anaufahamu na kuuenzi utamaduni wake mzuri.
  32. Msomi ana heshima kwa kila mtu, bila kujali jinsia, rangi, dini, nchi ya asili, na kadhalika.
  33. Msomi anatambua wajibu wake.
  34. Msomi anaweza kufanya mambo mapya; ana uwezo wa kuzalisha mawazo na kugeuza kuwa ukweli/uhalisia. Msomi ni mbunifu.
  35. Msomi ni mdadisi.
  36. Msomi ana uwezo wa kutambua tabia na tabia zinazohitajika katika jamii husika.
  37. Msomi ana uwezo wa kutambua tabia na sifa za hatari- Mfano ngono zembe.
  38. Msomi ana uwezo wa kuirekebisha jamii.
  39. Msomi hukubali wakati anapokosea na hujirekebisha.
  40. Msomi habishani,bali hutoa hoja (Ukibishana tu ushaondoa sifa ya usomi)
  41. Msomi anaweza kubadilika na anajua jinsi ya kukabiliana na mabadiliko.
  42. Msomi anajua jinsi ya kushughulikia utata.
  43. Msomi ana uwezo wa kuchunguza mawazo mbadala.
  44. Msomi ana shukrani;
  45. Msomi anaweza kufanya moja kati ya kuimba, kucheza vizuri, kucheza angalau chombo cha muziki kimoja, na anaweza kufahamu usanifu, sanaa nzuri, na maneno mengine ya ubunifu wa ubunifu.
  46. Msomi anafahamu umuhimu wa familia na jinsi ya kuimarisha familia kama msingi wa kuendeleza kizazi/vizazi bora.
  47. Msomi ni yule ambae anayo falsafa yake binafsi ambayo itawawezesha kuwa na furaha na mafanikio.
  48. Mtu mwenye elimu ana uwezo na kuhariri wazo katika mfumo wowote wa maandishi au mfumo wowote.
  49. Msomi hadharau elimu mpya inayopatikana kwenye mazingira yake.
  50. Msomi huwa nadhifu.
 
Back
Top Bottom