Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jonas Ziganyige (71) mstaafu wa Jeshi la Wananchi, Mkazi wa Mbezi Juu kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Patient Romwadi (48) mfanyabiashara, Mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni katika mgogoro wa mipaka.
Mtuhumiwa anadaiwa kufanya tukio hilo Julai 9, 2022 ambapo marehemu alifika eneo akiongozana na Recy Renso (52) kwa lengo la kuangalia mipaka ya kiwanja chake, ndipo mtuhumiwa akatoka ndani akiwa na hasira akampiga risasi Romward na baada ya tukio alikimbia kabla ya kukamatwa Julai 10, 2022 akiwa Kibaha Maili Moja, Pwani alikokuwa amejificha.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Muliro Jumanne amesema wameipata silaha aliyotumia ambayo ni Mark IV ikiwa na risasi 4, atafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka yanayo mkabili.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendelea pia na jitihada za kuzuia vitendo vya kihalifu kwa kufanya Oparesheni kali inayoongozwa na taarifa fiche dhidi ya Uhalifu na Wahalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Watuhumiwa 8 sugu wa uvunjaji nyumba na kuiba vifaa vya magari akiwemo Jumanne Omary (28) Mkazi wa Mikwambe na wenzake 7 wamekamatwa wakiwa na Tv flat screen za aina ya mbalimbali 4, laptop mbili, sab ufa moja, simu aina mbalimbali tano pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu vikiwemo mikasi miwili mikubwa ya kuvunjia, panga moja, kisu kimoja, Prize na Bisibisi, Tochi na Nyaraka mbalimbali.
Pia gari lenye namba za usajili T.787 DGW aina ya Toyota Gaia limekamatwa kwa kuhusishwa na kutumiwa kwenye vitendo vya kihalifu.
Jeshi la Polisi Kanda Maaluma ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwani kwa kufanya vitendo hivyo watakamatwa na watajikuta wakiwa katika msuguano mkali wa kiseria na vyombo vya dola.