Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yes Kuna majirani wapuuzi sanaAkisha hukumiwa kifungo cha maisha familia hiyo hiyo itaiuza ardhi(ya mstaafu) na kwenda kuishi mbali.
Ila kuna majirani wanakera jamani!
Ni upuuzi kugombea futi 3 za mpaka na kuwekeana uhasama hata kufikia hatua ya kuuwana. Futi 3 ambazo hata kuchimba kaburi hazitoshi. Mimi jirani akisema huku kwangu, nikatumia njia yote kumwelewesha kuwa sio kwake, akang'ang'ana na kuhamaki na njia zote kusuluhisha zimegoma. Namwachia.Ukubwa wa eneo sasa linalogombewa
Utakuta vihatua 3,4 tu
Na siku zote ugomvi wa ardhi huwa mmbaya sana,kama watu hamuelewani iko siku ardhi hiyo hiyo
Itammeza mtu
Ova
Bad enough unakuta yeye ndo mkorofiDuuh watu waache kupenda dhulma
Key word 'K'Mipaka ina mambo ya ajabu sana... Ni kama K tu.. watu wanauana sana kwenye mipaka..
Na ana sevente wan years ndio hivyo Tena ataozea jela. Kaua halafu kakimbia kwenda kujificha. Murder case siyo ya kuchezea hata kwenye nchi judiciary system ni dhaifu Bado tu murder case ni serious.Afu kaeneo kanakotumika kukuzika nikadogo sana. Mnauana kwa ajili ya ardhi?
Unaenda jela na kuacha familia yako kwa ajili ya ardhi?
Kupakana na askari yeyote wa jeshi la Tanzania ni changamoto kubwa sana. Wale wanao pakana nao nikiwemo mimi tulio wengi itakuwa tunajuta sana. Japo si wite, ila walio wengi wao wanajifanya wababe sana.Nimepakana na askari wawili kwenye eneo langu wote tuliuziwa na mtu mmoja aliyeamua kuuza eneo lake vipandevipande, mmoja alinikuta nimeshanunua na mwingine nilimkuta. viwanja vyote vilikuwa vimepimwa. tuliamua kupitia mipaka kwa pamoja ukaibuka mgogoro wa mipaka.
Nilijaribu kutafuta suluhu bila mafanikio, mmoja alikubaliana na bikoni zilizowekwa mwingine alikataa nikaamua kumwachia kijisehemu anakong'ang'ania.
lakini wote 2 walikuwa wababe. Ingawa mmoja alikuwa muelewa na alivitambua vipimo na bikoni za wataalamu.
Itakuwa ni shule na shughuli za jeshi zinawaathiri kwa kiasi fulani baadhi yao hawa wenzetu.
tunawaomba wenzetu mjitahidi kuishi vyema na jamii. Matumizi ya nguvu sio mara zote huleta suluhu.
Very true. Sasa yeye ataozea jela, na watoto/ndugu hawataitaka hiyo ardhi tena iliyosababisha mauaji. Kuna watu wajinga sana dunia hii. Sasa sijui kapata faida ganihuyo aliyoua. Alidhani kwenda kujificha kungemsaidia?Akisha hukumiwa kifungo cha maisha familia hiyo hiyo itaiuza ardhi(ya mstaafu) na kwenda kuishi mbali.
Ila kuna majirani wanakera jamani!
Umeandika utafikiri umekurupushwa, tulia andika uzi wako kwa mpangilio hata mtu akisoma anaelewa.Jonas Ziganyige (71) mstaafu wa Jeshi la Wananchi, Mkazi wa Mbezi Juu kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Patient Romwadi (48) mfanyabiashara, Mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni katika mgogoro wa mipaka.
Mtuhumiwa anadaiwa kufanya tukio hilo Julai 9, 2022 ambapo marehemu alifika eneo akiongozana na Recy Renso (52) kwa lengo la kuangalia mipaka ya kiwanja chake, ndipo mtuhumiwa akatoka ndani akiwa na hasira akampiga risasi Romward na baada ya tukio alikimbia kabla ya kukamatwa Julai 10, 2022 akiwa Kibaha Maili Moja, Pwani alikokuwa amejificha.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Muliro Jumanne amesema wameipata silaha aliyotumia ambayo ni Mark IV ikiwa na risasi 4, atafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka yanayo mkabili.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendelea pia na jitihada za kuzuia vitendo vya kihalifu kwa kufanya Oparesheni kali inayoongozwa na taarifa fiche dhidi ya Uhalifu na Wahalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Watuhumiwa 8 sugu wa uvunjaji nyumba na kuiba vifaa vya magari akiwemo Jumanne Omary (28) Mkazi wa Mikwambe na wenzake 7 wamekamatwa wakiwa na Tv flat screen za aina ya mbalimbali 4, laptop mbili, sab ufa moja, simu aina mbalimbali tano pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu vikiwemo mikasi miwili mikubwa ya kuvunjia, panga moja, kisu kimoja, Prize na Bisibisi, Tochi na Nyaraka mbalimbali.
Pia gari lenye namba za usajili T.787 DGW aina ya Toyota Gaia limekamatwa kwa kuhusishwa na kutumiwa kwenye vitendo vya kihalifu.
Jeshi la Polisi Kanda Maaluma ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwani kwa kufanya vitendo hivyo watakamatwa na watajikuta wakiwa katika msuguano mkali wa kiseria na vyombo vya dola.
Alipo niacha hoi,kwamba kaua harafu kakimbia kwenda kujificha!!yeye alifikiri ameua kuku!!Hawa watu ni wepesi sana,Richa ya kujitapa na magwanda yaoJonas Ziganyige (71) mstaafu wa Jeshi la Wananchi, Mkazi wa Mbezi Juu kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Patient Romwadi (48) mfanyabiashara, Mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni katika mgogoro wa mipaka.
Mtuhumiwa anadaiwa kufanya tukio hilo Julai 9, 2022 ambapo marehemu alifika eneo akiongozana na Recy Renso (52) kwa lengo la kuangalia mipaka ya kiwanja chake, ndipo mtuhumiwa akatoka ndani akiwa na hasira akampiga risasi Romward na baada ya tukio alikimbia kabla ya kukamatwa Julai 10, 2022 akiwa Kibaha Maili Moja, Pwani alikokuwa amejificha.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Muliro Jumanne amesema wameipata silaha aliyotumia ambayo ni Mark IV ikiwa na risasi 4, atafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka yanayo mkabili.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendelea pia na jitihada za kuzuia vitendo vya kihalifu kwa kufanya Oparesheni kali inayoongozwa na taarifa fiche dhidi ya Uhalifu na Wahalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Watuhumiwa 8 sugu wa uvunjaji nyumba na kuiba vifaa vya magari akiwemo Jumanne Omary (28) Mkazi wa Mikwambe na wenzake 7 wamekamatwa wakiwa na Tv flat screen za aina ya mbalimbali 4, laptop mbili, sab ufa moja, simu aina mbalimbali tano pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu vikiwemo mikasi miwili mikubwa ya kuvunjia, panga moja, kisu kimoja, Prize na Bisibisi, Tochi na Nyaraka mbalimbali.
Pia gari lenye namba za usajili T.787 DGW aina ya Toyota Gaia limekamatwa kwa kuhusishwa na kutumiwa kwenye vitendo vya kihalifu.
Jeshi la Polisi Kanda Maaluma ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwani kwa kufanya vitendo hivyo watakamatwa na watajikuta wakiwa katika msuguano mkali wa kiseria na vyombo vya dola.
Nimetoka hapo muda sio mrefuNipo msibani hapa wazo. Kesho tutazika. NADHANI HUZUNI NA SONONEKO LA FAMILIA HII NI KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.
Hilo eneo jamaa alienda kuangalia ni la rafiki yake yupo nje ya nchi, alimuomba akaangalie. Huyo babu wa miaka 71 kwa wenge akadhani huyu ni mmiliki nikiua huyu namiliki ardhi yote hii...POMBE NA BANGI VINAATHIRI SANA WANAJESHI.