Mstaafu wa Jeshi atuhumiwa kuua kwa risasi kisa mgogoro wa mipaka

Mstaafu wa Jeshi atuhumiwa kuua kwa risasi kisa mgogoro wa mipaka

Unatishwaje na raia? Chomoa cha moto maliza kazi, jamaa nalo jinga mtu ana cha moto unaanza kumwomba nipige uone, unakula ya kichwa, hiki kibabu nadhani kilikuwa kibodigadi cha Nyerere moja tu jamaa chali
Acha ujinga,MTU mzima wewe,we are discussing about human life lost unnecessarily, hahaha mbuzi pale!
 
Mimi ninaye jirani kama huyo wa kwako, tena huko huko maeneo ya wazo. Yeye kafukia barabara ili ihamie kwenye ardhi yangu, hivyo kaongeza kiwanja chake kwa kufukia barabara ya zamani. Naye ni askari mtaafu alafu Mchaga. Ukiirudisha barabara kwenye njia yake ya asili, yeye anaamka saa 8 usiku anaifukia tena. Yaani ni shida!
Dalili za maisha kuwa magumu
 
Unatishwaje na raia? Chomoa cha moto maliza kazi, jamaa nalo jinga mtu ana cha moto unaanza kumwomba nipige uone, unakula ya kichwa, hiki kibabu nadhani kilikuwa kibodigadi cha Nyerere moja tu jamaa chali
Hii ni zao la kuchua waliofeli na mabogus ndio muwe maaskari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hauz wew si unagombea mpaka labda unagombea hatua mbili yey anakuongezea na tatu juu uku akichomeka sale ogopa sana
Duu hatari sana. Hiyo sale ni kifaa gani mkuu? Na je, kama yeye ndo mkorofi anakudhulumu hizo hatua 2 inakuwaje?
 
Jonas Ziganyige (71) mstaafu wa Jeshi la Wananchi, Mkazi wa Mbezi Juu kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Patient Romwadi (48) mfanyabiashara, Mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni katika mgogoro wa mipaka.

Mtuhumiwa anadaiwa kufanya tukio hilo Julai 9, 2022 ambapo marehemu alifika eneo akiongozana na Recy Renso (52) kwa lengo la kuangalia mipaka ya kiwanja chake, ndipo mtuhumiwa akatoka ndani akiwa na hasira akampiga risasi Romward na baada ya tukio alikimbia kabla ya kukamatwa Julai 10, 2022 akiwa Kibaha Maili Moja, Pwani alikokuwa amejificha.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Muliro Jumanne amesema wameipata silaha aliyotumia ambayo ni Mark IV ikiwa na risasi 4, atafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka yanayo mkabili.

Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendelea pia na jitihada za kuzuia vitendo vya kihalifu kwa kufanya Oparesheni kali inayoongozwa na taarifa fiche dhidi ya Uhalifu na Wahalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Watuhumiwa 8 sugu wa uvunjaji nyumba na kuiba vifaa vya magari akiwemo Jumanne Omary (28) Mkazi wa Mikwambe na wenzake 7 wamekamatwa wakiwa na Tv flat screen za aina ya mbalimbali 4, laptop mbili, sab ufa moja, simu aina mbalimbali tano pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu vikiwemo mikasi miwili mikubwa ya kuvunjia, panga moja, kisu kimoja, Prize na Bisibisi, Tochi na Nyaraka mbalimbali.

Pia gari lenye namba za usajili T.787 DGW aina ya Toyota Gaia limekamatwa kwa kuhusishwa na kutumiwa kwenye vitendo vya kihalifu.

Jeshi la Polisi Kanda Maaluma ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwani kwa kufanya vitendo hivyo watakamatwa na watajikuta wakiwa katika msuguano mkali wa kiseria na vyombo vya dola.
Huyu ziganeje ni jirani yetu ametusumbua sana tokea tukiwa watoto kutoa bunduki na kupiga hewani ni jàmbo la kawaida ,amedhurumu mipira yetu tulipokuwa tunacheza jirani na kwake coz ni uwanja wa shule ya msingi mbezi juu, pia amekata eneo la shule kwa kudhurumu ,mwaka juzi wananchi walimpiga nusu kumuua baada ya kumpiga mwanafunzi mpk kuzimia polisi wakaja kumuokoa . Huku tunamwita putin
 
hakuna justification yoyote ya kuua mtu kwa namna yoyote ile uwe umesikiliza kila upande ama lah! nasisitiza hakuna na wala haipo kuua wewe ni muuaji tu Period.
Mi nadhani tunakomenti kwa kuegemea upande mmoja wa habari.

Tungelipata habari za pande zote kindaki ndaki tungelichekecha vizuri na kuboresha maoni yetu.

Je chanzo cha mauwaji haya chaweza kuwa ni sababu ya watu kuja kuoneshana mipaka tu, au kuna jambo jingine nyuma ya pazia?

Mimi si muumini mzuri wa kusikiliza maneno ya upande mmoja!

Sababu inayoelezwa kuwa ndiyo sababu ya chanzo cha mauaji haya, haiingii akilini na haitoshi.

Siyo kwamba kabla walishatiana ghadhabu siku nyingi na siku ya tukio ikawa ni siku iliyopangwa kwa ajili ya utekelezaji tu?

Nimeyageuza geuza haya maneno kifikra hayajai hata kiganjani kukubaliana na sababu zilizopekekea muuaji kufanya aliyoyaf
 
Ukubwa wa eneo sasa linalogombewa
Utakuta vihatua 3,4 tu
Na siku zote ugomvi wa ardhi huwa mmbaya sana,kama watu hamuelewani iko siku ardhi hiyo hiyo
Itammeza mtu

Ova

Na kweli utakuta hatua tatu zinawagombanisha
 
Isee mambo ya mipaka ni pasua kichwa, nina kakiwanja kangu 20×30M nilinunua mwaka 2010, nikafanikiwa kujenga na kuweka kaukuta kafupi mpakani kwa kua kulikua na kangema nyuma, baada ya miaka kadhaa yule kijana niliyekua nimepakana nae upande wa ukuta akamuuzia mhaya 1, tukafahamiana mshkaji fresh sana akajenga maisha yakaenda, Sasa mimi sio mkaaji wa pale nyumbani nahangaikia riziki mikoani narudi kila week nakaa siku 2 au tatu naondoka ila familia yangu ipo hapo, Sasa serikali ya kijiji ikaja kupima viwanja na kuweka bicon ili tupewe hati, sijui kilitokea nini mke wangu hakuwepo wa huyu jamaa jirani yangu hakuwepo mke wa jamaa akawaonyesha waweka bicon mpaka ndani ya ukuta wangu. Wakati mpaka halisi unaonekana kabisa nje ya ukuta niliojenga tena karibu 1m. Sio mimi wala wife hakuna aliyona ile bicon kumbe mama mmoja jirani aliona lile tukio la kuwekwa bicon ndani ya ukuta wangu. Baada kama siku tatu ndo akamwambia wife mbona bicon imewekwa huku, wife akavurugwa akanipigia baada ya week nilipopata nafasi nikaenda aisee kidogo nichanganyikiwe. Ikumbukwe natakiwa kuvunja ukuta sababu bicon ipo ndani ya eneo la jiran yangu na ukuta alikukuta wakati anauziwa,nikamfuata mwanaume mwenzangu namwambia vipi ananiambia hapo ndo mpaka, nikaita majirani wanao jua kile kiwanja pamoja na shahid jamaa amekataa katakata, mimi nikabomoa ukuta nikahamisha. Ugomvi ukahamia mimi na wife yeye anataka nikaze mimi nikamwambia sitaki. Mi nikasamehe maisha yakaenda, kumbe na upande wa juu huko yule mama alifanya hivyo hivyo kwa mama mwingine aliye pakana nae, yule mama akaongea na jamaa ikagoma kama mimi, yule mama akamwita shemeji yake kumbe ni mwajeshi kuja akamwambia nionyeshe mpaka ni upi, alipoonyeshwa tunashangaa kesho watu wakaja chimba mtaro tena ukutani kwa jamaa waka mimina zege wakapiga ukuta na nguzo za zege tena alijenga ndani kabisa ya kiwanja cha jirani yangu aliyenizulumu. Sashivi wanalia wanahangaika kila mtu hataki kuwasaidia. Yule mwanajeshi alienda kubadilisha ile karatasi ya mauziano na ana hati. Jamaa analalamika tu hadi leo

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Haya masuala ya mipaka ardhi ukiyachunguza kwa undani ni tamaa, upumbavu, ujinga, ubinafsi, wivu, uwelewa mdogo na roho mbaya tu kati ya mtu na mtu na wala hayahusiani na kazi, kabila, dini wala elimu ya mtu.

Kuna rafiki yangu mmoja wapo familia mbili jirani (mojawapo ni ya rafiki yangu) wamejenga wamefuatana lakini barabara ya kufika kwao inapita ubavuni kwenye kiwanja cha jirani yao ambaye ni kijana wa makamo tu ambaye ameenda shule vizuri na mkristo safi anatokea kanda ya Ziwa na mkewe anatokea kanda ya Kaskazini. Japo hizo familia mbili ndio zilizotangulia kujenga na kuhamia jamaa alipofika akajenga halafu akaweka ukuta kwenye usawa kabisa wa barabara. Jamaa ndani ya ukuta wake akaweka vyumba vya kupanga halafu akatoboa milango kwenye ukuta kwa hiyo mpangaji akifungua tu mlango kutoka nje yupo barabarani kabisa. Kama haitoshi akaongeza vijibaraza vya ngazi barabarani kiasi wakikaa nje gari ikipita inawabidi wainuke ili gari ipite. Barabara ilikuwa kubwa ya kupishana gari mbili sasa inapitisha gari moja tu hamna kupishana. Na ujinga wa kutamani kiwanjani chake kitanuke wakati ardhi haitanuki kajenga geti lake la kuingilia mwishoni kabisa mwa kiwanja matokeo anakuja kujenga kile kipaa kikawa kichekesho kimeingia kabisa barabarani ili kisigongwe na magari ikabidi akiinue juu kabisa kama mti wa mnazi.

Siku moja rafiki yangu alijaribu kumuuliza jirani yake kama anaona anachokifanya ni sahihi maana alikuwa ameweka tofali zake barabarani magari yakawa yanapita kwa shida. Jamaa akaja juu sana rafiki yangu akaachana naye sio kwa kumuogopa bali jama yangu ameshika sana dini na hapendi kabisa ugomvi. Na siku zote msemo wake ni kuwa ukitaka ushindi wa muda mfupi na laana ya muda mrefu basi dhulumu mtu ardhi hata hatua moja tu.

Kiukweli watu wengi wanaponunua hivi viwanja ndio uwezo wao kwa wakati huo. Lakini wakija kupata pesa zaidi baadaye badala ya kutumia akili wakanunue maeneo makubwa zaidi nje ya mji wanatamani eneo lile walipo liongezeke wakati ardhi haitanuki ndipo hapo sasa ugomvi wa mipaka na majirani unapoanzia.
Ni kweli kabisa jamaa amesema kweli,kudhulumu ardhi ni kosa kubwa mbele za mungu, Kwa wale wanao amini kuwa IPO siku tutaulizwa mbele za mungu,mjiepushe na dhulma ya ardhi
 
Hawa wazee waliotumikia Jeshi wanakuaga na PSTD yani wakikorofishwa wanaona kama bado wako vitani...!!!
Sifa za kijinga tu... ..

Kujiona muhimu zaidi ya wengine.. ..Kuna mmoja huku alikuwa analazimisha kuchota maji bila kukaa foleni..kisa JW..na mkewe ndio balaa.. ..walichofanyiwa sasa..mpaka kesho ..wanaishi Kama raia wengine na Wana staha haswa.. ...ulimbukeni flani tu!

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom