Mstaafu wa Jeshi atuhumiwa kuua kwa risasi kisa mgogoro wa mipaka

Mstaafu wa Jeshi atuhumiwa kuua kwa risasi kisa mgogoro wa mipaka

BRO usimlamumu marehemu bila sababu mtu akichomoa akakoki hata ukimbie itakupata tu.
Huyu jamaa alikuwa na chawa wake anaitwa Ranso, mtu hawezi kutoka akiwa na cha moto na kuanza kumwaga ndugu tu, lazima kulikuwa na mzozo na kwanini ampige mmoja mwingine a mwache, maswali ni mengi kuliko majibu
 
Binafsi kuna jamaa a lini chukua tukaangalie shamba lake kumbe alikuwa na mzozo na jirani kufika tulianza kushambuliwa nilitumia busara nikaanza kumgombeza jamaa yangu, baada ya kuona vile jamaa munkari ukashuka akaanza kunipa story ndo ikawa pona yetu, na hawa jamaa wangetumia busara wangetoka salama
 
71 afungwe kifungo Cha nyumbani, maana segerea atakata Moto mapema! Lakini mzee nae,huo Ni umri wa neema tu anapaswa atulie karibu na MUNGU wake[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Nimepakana na jamaa mmoja (mhirack) pasua kichwa! Kichwani mweupe haelewi kila siku ugomvi! Uzuri natenganishwa naye na barabara. Anatamani ahamishe/achepushe barabara ije kwangu! Ukiwa na jirani kama huyu na ukawa mpole, uwe na uhakika atakunyanganya eneo lako! Wakati mwingine inabidi ukomalie mali yako na ya watoto wako no matter what!

Ni kweli kabisa, huna jinsi, lazma utetee eneo lako na la watoto. Lakini ni hatari, huyo jamaa anaweza kukudhuru. Haya mambo sio marahisi kama picha inavyochorwa hapa JF kwamba uachie tu ardhi iende.

Omba Mungu mgombea ardhi mwenzio asiwe kichaa ambae hajali kuua au kwenda jela maisha.
 
Ni upuuzi kugombea futi 3 za mpaka na kuwekeana uhasama hata kufikia hatua ya kuuwana. Futi 3 ambazo hata kuchimba kaburi hazitoshi. Mimi jirani akisema huku kwangu, nikatumia njia yote kumwelewesha kuwa sio kwake, akang'ang'ana na kuhamaki na njia zote kusuluhisha zimegoma. Namwachia.
Wachaga wana Mila yao ukigombania kwake anapiga hatua tatu anaweka sale ukiwa kichwa maji ukikubali hiko kipande huchukui round lazima wakuzike
 
Undava wote na ardhi yetu yote mali ya jamhuri unapangishwa miaka 33 au 66. I can't imagine nchi zingine ambapo ukinunua ardhi ni miliki yako binafsi (private property).
 
Mimi ninaye jirani kama huyo wa kwako, tena huko huko maeneo ya wazo. Yeye kafukia barabara ili ihamie kwenye ardhi yangu, hivyo kaongeza kiwanja chake kwa kufukia barabara ya zamani. Naye ni askari mtaafu alafu Mchaga. Ukiirudisha barabara kwenye njia yake ya asili, yeye anaamka saa 8 usiku anaifukia tena. Yaani ni shida!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kazi ipo.
 
Kuna mzee mmoja nae ni mstaaf wa geshi basi hua ananikataza mpk kupaka rangi nyumba yangu et matone yatadondokea kwake
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Inawezekana kabisa walikuwa na ugomvi wa mipaka kwa muda mrefu.
Hata kama ndiyo uue kwa ardhi ambayo utaiacha hapahapa duniani!!!! Halafu ukute eneo wanalogombea hata mita za mraba 6 hazifiki.
 
Wajeda huwaga wanajikuta miungu watu sana , sasa akapambane na vijana wa Brig. Gen Mzee kule Segerea. unaua mtu kisa vimiguu viwili sasa kapata nini
Mi nadhani tunakomenti kwa kuegemea upande mmoja wa habari.

Tungelipata habari za pande zote kindaki ndaki tungelichekecha vizuri na kuboresha maoni yetu.

Je chanzo cha mauwaji haya chaweza kuwa ni sababu ya watu kuja kuoneshana mipaka tu, au kuna jambo jingine nyuma ya pazia?

Mimi si muumini mzuri wa kusikiliza maneno ya upande mmoja!

Sababu inayoelezwa kuwa ndiyo sababu ya chanzo cha mauaji haya, haiingii akilini na haitoshi.

Siyo kwamba kabla walishatiana ghadhabu siku nyingi na siku ya tukio ikawa ni siku iliyopangwa kwa ajili ya utekelezaji tu?

Nimeyageuza geuza haya maneno kifikra hayajai hata kiganjani kukubaliana na sababu zilizopekekea muuaji kufanya aliyoyafanya!
 
Kama hio bastola aliiacha ndani akaifata akatoka mpaka nje akaikoki akampiga huyo mwingine hio ndo malice afore thought sababu kwa muda alioutumia kwenda ndani kuitafuta katika akili ya kawaida anaweza hata ghairi kutaka kuitumia ila kama ilikua ipo kiunoni akampiga jamaa mara moja..hio ni manslaughter ila kwa kupiga risasi tatu huyo alidhamiria kumuua
Bunduki iliyotajwa katika habari ni mark4 ambayo ni Rifle na si Bastola.

Mtu hawezi kukaa na bunduki aina hiyo nje kama hana shughuli za ulinzi.

Nilitaka kusahihisha upande huo tu.
 
Back
Top Bottom