Msukuma: Nyie wasomi huko shuleni mnafundishwa kuliibia taifa? Kila mahali nchi hii wamejaa wezi wanaovaa suti na tai!

Msukuma: Nyie wasomi huko shuleni mnafundishwa kuliibia taifa? Kila mahali nchi hii wamejaa wezi wanaovaa suti na tai!

Mbunge wa Geita vijijini Dr Msukuma amesema nchi hii imejaa Wezi kwenye Ofisi zote yaani ni Wizi kila kona na hakuna hatua zinachukuliwa na Mawaziri hawako serious kabisa

Msukuma amesema ni aibu kuwa na taifa la Wezi ambalo kila mwaka CAG anatuletea Taarifa za Wezi tu

Msukuma ametaka Bunge liwe na meno na Serikali ijiangalie sana katika Utendaji wake

Source: TBC
Ukiona mdogo anabehave vibaya basi kaa ukijua mkubwa wake anatabia ya hovyo. Naona wangeanza na wajuu hawa watching wata jirekebisha wenyewe.
 
Huyu mbunge anaonekana kuumia sana kwa kukosa elimu ya juu.

Yaani ana Mali lakini hajiamini na hajipendi kwa sababu haziendani na kiwango cha elimu yake.

Bora ukose Mali upate akili
 
Hayo yamekuwa majizi kwa sababu ndivyo yalivyo, siyo kwa sababu yamesoma.

Musukuma anakosea sana kusema kywa eti mawaziri hawawachukulii hatua wevi?! Nchi hii majizi makubwa ni kuanzia ofisi za juu kabisa mpaka za mwusho kabisa.

Sasa, tangu lini mwizi mkubwa akamchukulia hatua mwizi mdogo? Utawala mzima ni wa wizi, ufisadi na rushwa, hakuna palipoachwa. Kama mtu anataka kujitenga na wizi, ni lazima ajitenge na CCM. Haiwezekani mtu aseme anachukia wizi halafu yupo kwenye chama cha wezi, itakuwa ni unafiki mkubwa!!
 
Mbunge wa Geita vijijini Dr Msukuma amesema nchi hii imejaa Wezi kwenye Ofisi zote yaani ni Wizi kila kona na hakuna hatua zinachukuliwa na Mawaziri hawako serious kabisa.

Msukuma amesema ni aibu kuwa na taifa la Wezi ambalo kila mwaka CAG anatuletea Taarifa za Wezi tu.

Msukuma ametaka Bunge liwe na meno na Serikali ijiangalie sana katika Utendaji wake.

Chanzo: TBC
Yeye mwenyewe kapiga za DP kama falsa ya chama ni uwizi nani atazuia
 
Msukuma ana wivu na wasomi [emoji23][emoji23]

Wakati wenzake wakisoma yeye alikimbilia kuchunga ng'ombe

Wizi wa Mali ya umma hauna Cha elimu wala nini
Msukuma ana hoja asikilizwe...!

Waajiriwa wa serikalini na mashirika ya umma ambapo ndiyo wizi umetamalaki ni wasomi wabobevu...huko kuna lundo la bachelor degrees, masters na PhD za kumwaga, wahasibu wao wamejaza CPAs kwenye CV zao lakini bado nchi imekwama...Je, imekwamishwa na nani?

Bila shaka wasomi hao wana mchango mkubwa kwenye mkwamo huo!

Tuseme ukweli...elimu ya mzungu haijamsaidia mwafrika kujitambua!
 
Tangu Utawala wa miaka 24 wa Mwl. Nyerere kutamatika mwaka 1985 baada ya hapo Viongozi wote wakaamua Kuchukua Chao Mapema
Kipind cha Mwalimu Nyerere waliiba sana mpaka kugawana mali za mkoloni ndio chanzo cha ukwasi kwa jamii nyingi na kuendeleza kizazi.


Mwalimu alikuwa na mengi ya kusema mpaka akang'atuka wengi walikuwa wanafaidika na mfumo ....Sema hapakuwa na media ila watu walijimiliksha hekari za kutosha na mali za mkoloni.
 
Msukuma ana hoja asikilizwe...!

Waajiriwa wa serikalini na mashirika ya umma ambapo ndiyo wizi umetamalaki ni wasomi wabobevu...huko kuna lundo la bachelor degrees, masters na PhD za kumwaga, wahasibu wao wamejaza CPAs kwenye CV zao lakini bado nchi imekwama...Je, imekwamishwa na nani?

Bila shaka wasomi hao wana mchango mkubwa kwenye mkwamo huo!

Tuseme ukweli...elimu ya mzungu haijamsaidia mwafrika kujitambua!
Huko pamejaa uwizi na dhuluma yaani mtu kupata stahiki zake ni kimbembe ila wanaiba mabillion ya pesa....Hapa bongo mtu akiajiriwa tu basi kashakuwa tajiri
 
Nay wa Mitego alipoimba wimbo wake alionekana amekosea...kuna mstari unasema panya road wanavalishwa suti na tai nadhani wengi ndiyo tunaanza kuelewa. Haya matatizo yanatokana mfumo mbovu wa kijanjajanja na kujuana siyo wasomi.

Hii tabia ya viongozi kuwatukana wasomi na kudhalilisha elimu ni tabia ya kipuuzi sana na haifai kuachiwa iendelee kwa hatua iliyofikia. Hakuna chuobkinachofundusha mtu kuwa mbadhirifu, mlarushwa na mwizi Tanzania, na siyo makengo ya elimu.

Mifumo dhaifu na mibovu ya waliokabudhiwa dhamana ndiyo inayoruhusu masuala ya ajabuajabu kuendeleza kushamiri. Wabunge ni wawakikushi wa wananchi, wanapaswa kuishauri Serikali iimarishe mifumo yote ya usimamizi na utawala wa raslimali za Taifa.
 
Back
Top Bottom