Msukuma: Nyie wasomi huko shuleni mnafundishwa kuliibia taifa? Kila mahali nchi hii wamejaa wezi wanaovaa suti na tai!

Msukuma: Nyie wasomi huko shuleni mnafundishwa kuliibia taifa? Kila mahali nchi hii wamejaa wezi wanaovaa suti na tai!

Hii nchi inavyoliwa nina wasiwasi huko mbeleni hakuna mtu atajitoleza kugombea urais, maana nchi imejaa madeni ambayo kiufupi hayalipiki. Rais ameweka watu ambao wana hulka na tabia za fisi kula hadi mizoga, mtu kama Mwigulu, Makamba na Nape hawa ni wezi kabisa na wizara zao zinaongoza kwa madudu lakini kila siku wanapewa nafasi za kiuongozi. Halmashauri za wilaya na majiji kumejaa majizi na ndiko fedha nyingi za serikali zinapelekwa. Mungu tu ndo anajua hatma ya taifa hili.
 
Nchi ina maajabu hiyo
Watunga sheria wanalalamika, Rais anasema ibeni kidogo
Mtu analalamika akiwa bungeni seriously?

Wanaogopa kutunga sheria kuwafunga maana hapo bungeni patageuka jela
 
Bila shaka yeye anauhakika sio mwizi, na mali yake haijapatikana kwa wizi.

Kama mwakilishi wa wananchi anapaswa kutoa solution kuliko kulaumu wasomi, shida sio wasomi bali shida ni system na uongozi makini ngazi za juu.

Kama siasa inalipa zaidi kuliko kazi yeyote unawezaje kulaumu wasomi, maana hao wasomi nao itabidi wakimbilie siasa ili wapige hela, matokeo yake kila Mtanzania ni mwanasiasa.
 
Hao anaowaita wasomi na wezi wanatoka kwenye jamii yetu humu humu, ni baba zetu, mama zetu, shangazi zetu, wajomba zetu n.k.
Kwa kifupi Taifa limepoteza uelekeo katika upande wa maadili. Kila anayepewa kazi ya umma anaona ni fursa ya kupiga. Mbaya zaidi mtu akipewa kazi ya umma watu wanaomzunguka yaani ndugu , jamaa na marafiki wanamwona mjinga asipojitajirisha kwa wizi.

Inasikitisha sana but ndiyo nchi imeshafika hapo.
 
Msukuma ana hoja asikilizwe...!

Waajiriwa wa serikalini na mashirika ya umma ambapo ndiyo wizi umetamalaki ni wasomi wabobevu...huko kuna lundo la bachelor degrees, masters na PhD za kumwaga, wahasibu wao wamejaza CPAs kwenye CV zao lakini bado nchi imekwama...Je, imekwamishwa na nani?

Bila shaka wasomi hao wana mchango mkubwa kwenye mkwamo huo!

Tuseme ukweli...elimu ya mzungu haijamsaidia mwafrika kujitambua!

Acheni lawama za kijinga. Shida ya hii nchi ni mfumo wa utawala wa CCM . Ulitaka muhasibu afanye Nini wakati Rais anatetea kukopa nje.
 
Kipind cha Mwalimu Nyerere waliiba sana mpaka kugawana mali za mkoloni ndio chanzo cha ukwasi kwa jamii nyingi na kuendeleza kizazi.

Mwalimu alikuwa na mengi ya kusema mpaka akang'atuka wengi walikuwa wanafaidika na mfumo ....Sema hapakuwa na media ila watu walijimiliksha hekari za kutosha na mali za mkoloni.

Punguza uongo, waliiba Nini wakati nchi ndio ilikuwa inajitafuta?. Tuache kuongea tusiyoyajua.
 
Kwanini shule za serikali zisiwe kama feza?
Ajuza pole na mafuriko, nasikia huko kwa Bibi Nyau mlizingirwa na mafuriko siku 3 upo ndani, hilo swali muulize Mzanzibar mwenzako ndiyo ameshika mpini. Ameachia nchi watu wanagawana pesa za umma kama vile hakuna serikali.
 
Watanzania wote ni WEZI.

Ni kwa vile tu wengine hawajapata nafasi ya kuiba.

Kwenye maongezi ya watanzania wengi utasikia wakisema akipata kazi serikalini yani michongo na madili kama yote atafanya.

Wizi ni asili ya mtanzania.Ukitaka thibitisha hili angalia mentality za watanzania wengi kutaka nafasi za kazi kwenye taasisi kubwa kubwa kama TRA,TPA n.k

Lengo si ili wafanye kazi kwa weledi, Ni kwa vile wanaona taasisi hizo madili ya maokoto ni chapu chapu.

Sasa ukiwa na kizazi cha namna hii, Hakuna maendeleo zaidi ya wizi, rushwa, uhujumu uchumi, ubadhirifu wa fedha za umma..
 
Kama mabosi wanaiba wewe utaachaje? mfumo mbovu ndiyo shida ya Tanzania
 
Hatuna bunge, nashangaa hata mnaopoteza mda kuangalia bunge live, its either mna maslahi yenu au hamna kazi za kufanya.
 
Watanzania wote ni WEZI.

Ni kwa vile tu wengine hawajapata nafasi ya kuiba.

Kwenye maongezi ya watanzania wengi utasikia wakisema akipata kazi serikalini yani michongo na madili kama yote atafanya.

Wizi ni asili ya mtanzania.Ukitaka thibitisha hili angalia mentality za watanzania wengi kutaka nafasi za kazi kwenye taasisi kubwa kubwa kama TRA,TPA n.k

Lengo si ili wafanye kazi kwa weledi, Ni kwa vile wanaona taasisi hizo madili ya maokoto ni chapu chapu.

Sasa ukiwa na kizazi cha namna hii, Hakuna maendeleo zaidi ya wizi, rushwa, uhujumu uchumi, ubadhirifu wa fedha za umma..
Kwa sababu ya mfumo mbovu unaolea wiziwizi
 
Back
Top Bottom