Msukuma: Nyie wasomi huko shuleni mnafundishwa kuliibia taifa? Kila mahali nchi hii wamejaa wezi wanaovaa suti na tai!

Mbunge wa Geita vijijini Dr Msukuma amesema nchi hii imejaa Wezi kwenye Ofisi zote yaani ni Wizi kila kona na hakuna hatua zinachukuliwa na Mawaziri hawako serious kabisa...
Ccm mliko huko ndio imewalea ndio maana unaona hawataki kutunga sheria ya kuwafilisi achilia mbali kuwanyonga.

Hakuna wizi mkubwa hata mmja ambao haunufaishi wezi na wanaoiba ni wanaccm walio na Vyeo
 
Sina hakika kuhusu hilo Mkuu, ila Utambue hakukuwa na Kiongozi anaogopwa Nchi hii Kama Mwl Nyerere.

Hao viongozi kama kujimilikisha mali watakuwa walifanya miaka ya kuanzia 1985 kuja 2000

Ukisoma Kitabu cha Marehemu Mzee Mengi cha I can, I will, I must ameelezea vizuri.

Hayo matumbo makubwa ya Viongozi yameanza baada ya Kifo cha Mwl. 1999
 
Mwalimu ndie alikuwa soft sana hakuwa mkali kabisa ....Ila wezi walikuwepo tangu zamani amini .
 
Vp lile V8 la DP World analizungumziaje?
 
hiyo inamaana
 
Msukuma ana wivu na wasomi [emoji23][emoji23]

Wakati wenzake wakisoma yeye alikimbilia kuchunga ng'ombe

Wizi wa Mali ya umma hauna Cha elimu wala nini
Wivu wake ni kwamba nyinyi ni majizi tu hamna la maana
 
Pumbafu kabisa. Kuna wanaolipwa na ni kazi yao kuchunguza na kupeleka mahakamani wezi. Unajua maana ya serikali?
Hawajaona kwakuwa wewe umeona hebu, kimbia chap mahakani usiogope.
 
Hawajaona kwakuwa wewe umeona hebu, kimbia chap mahakani usiogope.
Narudia. Tunachagua serikali na kuipa vyombo kama ili kuchunguza na kupeleka mahakamani wahalifu. Siyo kazi ya raia.
 
Narudia. Tunachagua serikali na kuipa vyombo kama ili kuchunguza na kupeleka mahakamani wahalifu. Siyo kazi ya raia.
Kwani mbona huwa tunaona watu wana mshtaki mwanasheria mkuu na viongozi wengine wa serikali, hebu Mkuu okoa jahazi wapeleke kortini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…