Magaidi wao wenyewe wana intelligence na wanajua kutafuta maadui zao. Hakuna haja ya kuuziwa taarifa, na jeshi letu unasema sio dhaifu ila ndio hilo hapo na magari yao yanayotumiwa na makampuni ya kitalii pale Arusha. Na hapo wapo kwenye warzone.
Rwanda hawa hapa wako warzone na magari yao hilo la mbele ndio yanaenda patrol
View attachment 2423959Nionyeshe lini umesikia Rwanda, Botswana au South Africa wamepigwa kizembe kama hivi hapo Mozambique, tena mission kubwa inapigwa na Rwanda kuliko sisi. Na ninahisi waasi watakuwa wanafanya ambush zaidi kwa Tanzania kwa maana hakuna upinzani. Toyota hardtop itumike warzone sijui kufanya patrol au kulinda msafara? Tuachane na hiyo Iveco hiyo lazima iwe hivyo. Huku kuendekeza umaskini tunapitiliza.
Ni kawaida ya serikali kutojali kila kitu. Nchi serious zinajali uhai na usalama wa wanajeshi. Hiyo ni mission ya wanajeshi hata 1,000 hawafiki na magari machache tu. Unaona hao Rwanda na Kenya wanaojitutumua nje ya nchi si kwamba wanajeshi wake wote wana sare nzuri, silaha bora na uwezo mkubwa bali kuna wachache wa kuzugia kwenye adversaries wadogo kama magaidi na waasi. Vita ya taifa na taifa watajua mbele ya safari. Sisi mission ya wanajeshi wachache tuna silaha za hivi sijui lengo ni nini.
Huwezi kuwa na jeshi lenye confidence wakati halina zana basic