Msumbiji: Inasemekana Magaidi wamevamia Msafara wa Wanajeshi wa Tanzania na Lesotho

Wajomba wamekimbia?
Kuna kipindi tuliambiwa vijana wa Kagame wamewamaliza magaidi na kila kitu ni shwali! Sasa nini Tena.
 
Wimbo wangu ni uleule, serikali ya Tanzania nunueni silaha chache za muhimu wala sio gharama kubwa sana. Acheni uzembe wa kutumia Toyota as if sisi ni ISIS au Taliban. Hizo Toyota wars waliziziasisi Chad walipovamiwa na Libya mwishoni mwa 1980s ila nchi maskini za Kiafrika na waasi wakaona ndio cheap alternative wakaiga.

Wanajeshi wanabidi wafanye patrol kwenye MRAP hata wakikutana na IEDs hawapati madhara zaidi au wakipigwa ambush wanaweza jitetea vizuri. Hii ni MRAP imekanyaga bomu la ardhini juzi hapo Ukraine na probably wamesalimika waliokuwa ndani

Majeshi kadhaa ya West Africa baada ya kuona waasi wako very manouverable hutumii heavy armour kama vifaru kuwapiga wakachukua MRAPs hata za 4×4 na zinapiga kazi vizuri.
 

Mimi naona wasiwaamini sana wanajeshi wa Msumbiji wamo pia wanajeshi waliokuwa kwenye kundi la RENAMO waliojiunga na jeshi la Msumbiji baada ya malidhiano - sina shaka hao ndio wanaweza kuwa wanawapatia taarifa hao magaidi kuhusu movement ya majeshi ya kuleta amani nchini Msumbiji - hata hivyo miaka yote hiyo tangu Msumbiji ipate uhuru wanashindwa nini kujilinda??
 
Hii ni Hiriz 4×4 imetengenezwa na Uturuki hapa wanaotumia Gambia

Hawa ni Botswana. Nimeona AK-47 hapo na JWTZ, hiyo bunduki ni outdated kijeshi labda kama wangekuwa militia. Botswana nowadays sijaona wana bunduki za zamani, hata Kenya hapo wamepunguza kutumia AK-47

Hawa ni Uganda General Muhoozi akiwa anakagua Cavalier Hamza 6×6 armoured personnel carrier

Sio mambo magumu hata. Hata kutoka South Africa hapo tunaweza ongeza idadi ya protected vehicles. Hao waasi kwa haraka wametumia risasi tu, haikutakiwa iwe tishio kivile. Niko tayari kukosolewa
 
tangu Msumbiji ipate uhuru wanashindwa nini kujilinda??
Mkuu Msumbiji ilikuwa inachezewa na Serikali ya Makaburu wa Afrika ya Kusini.
Na lengo lao ilikuwa ni kuwadhoofisha ili vikundi vya Ukombozi kutoka Afrika ya Kusini ambavyo baadhi yao viliweka Makambi ndani ya Msumbiji kabla ya ukombozi wa Zimbabwe.

Serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini ilishtuka sana baada ya Serikali ya Walowezi ya Zimbabwe kusarenda na kuanza mazungumzo.

Renamo ya akina Dlakama ilianzishwa na mashushushu wa Afrika ya Kusini.

Mpaka leo Msumbiji haija recover.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…