Msumbiji yaanza kusafirisha Gesi kwenda Ulaya

Kwanza mngeuona huo mkataba unasemaje ndio mtoe tathmini zenu. !! Jamaa alisema pale tulishapigwa !! Kama sio kweli onyesheni mkataba hadharani watu wajue kilichomo. !!
 
Kwanini kile kiwanja cha kujenga LNG kilikuwa kinamilikiwa na mtu binafsi? Mbaazi ikikosa maua huwa ina tabia ya kusingizia jua.
Watanzania tunaona fahari kulaumu na kusingizia mambo ambayo wala hayana ukweli. Yenye ukweli tunayalinda ili yaendelee kulinda maslahi yetu.
Tatizo letu kubwa ni ubinafsi uliopitiliza. Kila mtu mbinafsi. Siamini mtu yoyote yule sasa hivi. We have just been confused and used, for the benefit of the few
 
Mwendazake aliamini kwenye 50/50 Kama alivyodanganya kule kwenye dhahabu! Yaani mtu awekeze mtaji wa trillion 60 wewe hata mia hujaweka alafu kwenye faida useme tulingane? Hata Urussi kwenye Gesi yao hawana hii kitu
 
Sasa hata kama mnapewa mrabaha asilimia 0.00000000000000001, uendeleze tu mazungumzo au sio?

Yale yale ya bandari ya Bagamoyo, masharti ambayo ni mlevi tu mdiye anaweza akasaini.
 
Mwendazake aliamini kwenye 50/50 Kama alivyodanganya kule kwenye dhahabu! Yaani mtu awekeze mtaji wa trillion 60 wewe hata mia hujaweka alafu kwenye faida useme tulingane? Hata Urussi kwenye Gesi yao hawana hii kitu
Mbona Botswana imewezekana.

Acha upotoshaji.
 
Mbinafsi ni yule aliyesitisha mzungumzo kwenye uwekezaji wa gesi pale alipoingia madarakani kwa chuki na husda zake tu
 
Mawazo ya mtu maskini ni kufikiria kila tajiri anamwibia. Ukimwuliza, wanakuibia nini, hajui na hawawezi kukuambia.

Eti wazungu wamewapiga Msumbiji! Wamewapiga kivipi? Msiwe mnarukia hata vitu ambavyo hamvijui.

Kama laiti ungekuwa umefika mji ule wa Pemba kabla ya uwekezaji mkubwa huu wa gas, halafu ukawa umeenda siku za karibuni, ungewaona wote waliowafanya wale wawekezaji kuondoka Tanzania na kwenda Msumbiji, ni mashetani wakubwa, na maadui wakubwa wa Taifa hili. Uwekezaji ule wa dola bilioni 28, ulikuwa ni uwekezaji mkubwa wa pili Duniani, wa kwanza mkubwa barani Afrika, na wa kwanza mkubwa nchini Msumbiji tangu mwanzo wa Taifa hilo.

Ukienda Pemba, watanzania wamejaa, unaweza hata kufikiria upo Tanzania.

Mapato ya gas ya Msumbiji, ukilinganisha na mapato yatokanayo na mauzo ya madini yetu yote kwa pamoja, ni tone katika bahari.

Muda si mrefu, Watanzania watakuwa watazamaji, wakati Msumbiji itakapokuwa ikipaa kwenye ukuuaji wa uchumi.
 
Kuna mtu mmoja aliniambia kwamba huwezi kupiga hatua ya maendeleo bila kubadili dominant system(os) na akatoa mifano kadhaa.
1. Mfumo wa magari yanayotumia mafuta ni wa internal combustion. Na ndio dominant sokoni. Ukitaka kuubadilisha ghafla ni hatari.
2. Key board za computer nyingi zina mfumo(?) Wa qwerty na ndiyo dominant japo azerty nayo ipo. Kuibadilisha itaathiri chumi nyingi.
3. Tanzania mfumo wetu ni Politically dominated tena na chama kimoja na uliojichimbia. Hofu kama tukibadili ghafla nini kitatokea? So watu wanakuwa na wasiwasi na hivyo. Matokeo yake tumewekeza kwenye siasa kwa ajili ya kuendelea kulinda huu mfumo. So like the IC engine tunahitaji kuubadili lakini tunahofia matokeo ya kubadilika kwa mfumo. Twende nao taratibu au tufanye overhaul?
 
Mbinafsi ni yule aliyesitisha mzungumzo kwenye uwekezaji wa gesi pale alipoingia madarakani kwa chuki na husda zake tu
Chuki haikufanyi wewe na watu hawa waliopo kuwa safi na watakatifu. This self-pity has been created over time by one team after another.
Nionyeshe mwangi wa tatizo, nikuonyeshe kivuli cha jinsi ambavyo hatuko serious,na tulivyobea kwa ubinafsi.
Tunapodhani tumesimama, waswahili wenzangu wanasema, tuangalie tusianguke. Kama tunataka usalama mbele ya safari, tuache hizi hadithi za kuonyeshana nani zaidi wakati wote tunafanya takataka zilezile.
 
Kwanza mngeuona huo mkataba unasemaje ndio mtoe tathmini zenu. !! Jamaa alisema pale tulishapigwa !! Kama sio kweli onyesheni mkataba hadharani watu wajue kilichomo. !!
Inawezekana unachosema na nia sio kumlaumu JPM, point ni kwamba hatuna umeme huku tuna trillions za gas ambazo zingeweza kutuwashia umeme mpaka wa ziada for the next 100 years na zaidi, kingine tunatumia trillion sita kujenga umeme wa maji ambao unategemea mvua na kuharibu mazingira (sio lazima ukubaliane na mimi kwa hili), tuna kila kitu lakini bado tunaishi kwenye umaskini na migawo kila siku kwa ajiri ya maamuzi yetu wenyewe (serikali ya CCM lazima ilaumiwe ndio waliotufikisha hapa)
 
Hivi kama wananchi wananunua gas kupikia vyakula vyao, kwanini TANESCO wasinunue gas na kununua turbines za kutosha kumaliza tatizo la umeme once and for all nchi nzima, gas ipo na turbines zipo zimejaa ukiweka order mjerumani au mchina atakuja kuzifunga in 3 month, tatizo ni nini? nafikiri kuna ujinga unaendelea na lazima uwe mjinga kuuelewa
 

Thread closed...,,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
We mweupe Sana kichwani,gesi itoke msumbiji Hadi ulaya kwa Bomba!?..ndege gani ilisafirisha gesi!?..picha umewekewa bado inauliza tu
Sasa wewe uliye smart kichwani,ina kuwaje unashangaa eti gesi itoke msumbiji hadi ulaya?!?kwa bomba?wakati sasa kuna mpango wa ujenzi wa bomba la gesi toka NIGERIA hadi SPAIN lenye urefu wa km 4000!!!halafu mbona lipo lenye urefu wenye zaidi ya km 8000?!!sasa unashangaa nini la kutoka Msumbiji?!!

We mweupe Sana kichwani,gesi itoke msumbiji Hadi ulaya kwa Bomba!?..ndege gani ilisafirisha gesi!?..picha umewekewa bado inauliza t
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…