Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Nimefanikiwa kuupitia muongozo wa mtaala mpya wa elimu hapa Tanzania ambao umezinduliwa hivi karibuni, na hichi ndicho nilichoweza kukiona kwa jicho la upeo.
1. Kwa mfumo wa elimu yetu kwa shule za serikali hauwezi kutekelezeka.
2. Hauna kipimo chochote MADHUBUTI cha kumpima mwanafunzi kila mara wakati akipewa elimu hiyo ama kupima ufanisi wa mwalimu wake wakati akitoa elimu hiyo mpaka mwanafunzi atakapohitimu miaka 10 ijayo.
3. Hakuna maandalizi yoyote kabambe yaliyofanywa kuweza kuubeba kikamilifu huu mtaala mpya. Kuanzia vyuo, waalimu, maafisa elimu, miundo mbinu, vitendea kazi na mazingira havikuandaliwa vyema kuweka kuubeba huu mfumo.
Kwa mtaala huu mpya, upo uwezekano kwa 100% kwa mtoto yoyote anayesoma shule ya serikali akaanza darasa la awali mpaka akahitimu kidato cha nne hajui kusoma, kuandika au kuhesabu. Kwanini? Mtaala umeweka wazi kabisa kuwa, mtoto yoyote anayeandikishwa shule hapaswi kufeli wala kurudia darasa (hata kama hajui chochote) mpaka atakapohitimu kidato cha nne!