Daah! kuna ndugu yake babu mmoja (R.I.P) alikuwa anaweza kufanya hiyo kazi aisee, Mzee yule hakuwahi tangu namjua sikuwahi kumuona anashikwa kiu ya kunywa maji( yaaani maji kwake ni kesi/sumu ilikuwa kwa mujibu wa maruhani yake,,,, na chakula alichokuwa anaweza kula ni ubwabwa pekeee). Yaani huyu Mzee alikuwa akifika sehemu anaweza kusema kuwa hapa leo hapako sawa au mambo yako vizuri. Kuna dada etu mmoja alikuwa anaweweseka sana mara maruhani yapande basi mzee anaongea nayo. Ikatokea kuwa kuna kajamaa kuwa ndiyo inatakiwa kamuoe huyo sista lakini Mzee akachungulia akasema huyu dogo Mungu amemuandaa kuwa Mchungaji na tunavyoongea Jamaa ni Mchungaji huko Rock City na Dada yeye amebakia kutanga tanga tuu na wanaume yaani.
Kwa kweli ungepata msaada kutoka kwa huyu Mzee maana ametafasiri ndoto &kuwatuliza sana akina KITI na jamii yao.