Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa


Mkuu tafadhali kamuone Gynecologist. Hilo tatizo inaonekana kuwa ya kizazi chake mkewe. Dawa haiwezi kusaidia. Lazima Daktari bingwa wa wanawake na mambo ya kizazi afanye vipimo na akupe ushauri juu ya swala hili. Bila vipimo haiwezekani. Tafadhali mtafute daktari bingwa wa wanawake.
 
Nasumbuliwa na maumivu kwenye korodani kwa Muda mrefu cjui tatizo ni nini

Yaonyesha una infection kwenye korodani. Chukua dawa hizi:

Ciprofloxacin 500mg kidonge kimoja.
Doxycycline 100mg, kidonge kimoja kutwa mara mbili kwa siku saba.
Metronidazole 400mg kidonge kimoja kutwa mara tatu kwa siku saba.

Nipe mrejesho.
 
Dr. Mke Wangu alijufungua mwezi wa pili, baada ya kujifungua ameanza tatizo la kuumwa kiuno mara mara je tatizo ni nini.

Hii tatizo ili anza pale pale baada ya kujifungua au ulianza wiki moja au mbili baada ya kujifungua?
 

Nimeelewa tatizo lako. Kunywa dawa hizi:

1. Neuroton, Kidonge kimoja kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.
2. Gabapentin 300mg, Kidonge kimoja kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.
3. Ukiwa na maumivu kwenye goti, kunywa Aceclofenac kidonge kimoja kwa siku.

Asante.
 
Natatizo mmoja.napokuwa na lala kabla sijapata usingizi Wa jumla au nikiwa naelekea kuchukulia na usingizi.nashutuka kwa nguvu sana na hapo ndio napata usingizi nalala moja kwa moja naomba msaada nini tatizo

Hilo tatizo linaitwa' "Hypnic Jerk". Hakuna haja kuchukuwa dawa yeyote kwaajili ya tatizo hili. Inabidi ubadilishe mambo machache kwenye maisha yako.

1. Ule chakula saa moja au zaidi kabla yakulala.
2. Usitumie simu, kompyuta, tv au chochote electronic nusu saa kabla ya kulala.
3. Unapolala usikuwe na fikra yeyote. Inabidi uwe umerelax na upo kwenye starehe.
4. Ni vizuri sana upate usingizi wa masaa sita au saba kila siku.

Zote hizi zitasaidia kupunguza tatizo hilo. Asante.
 

Mkuu, Unakunywa maji kwa idadi gani kila siku?
Rangi ya mkojo wako ni gani?
 
Dr habari yako, mimi nina tatizo la kupata choo, naweza pita siku tatu sijapata choo, ila nikinywa pombe napata choo kama kawaida nimecheki hospt wnasema hawaoni tatizo,

Niambie unakula chakula cha aina gani na unakunywa maji ya idadi gani?
 
Daktari nahitaji kujua ni vidonge gani huwa vinatumika katika kupunguza stress na pia kupunguza depression??

Kawaida watu waliokuwa wanadepression wanapewa Citalopram 20mg kila siku kwa muda wa wiki mbili.
Lakini kama mtu anatatizo hili lazima amuone daktari.
 

Natumai nimejibu swala hili. Kama sijajibu tafdhali niambie.
 
Tatizo la meno kuwa na ukakasi kiasi cha kushindwa perasi, nanasi

Piga mswaki kutwa mara mbili na tumia mouth wash ya Listerine kutwa mara mbili. Pamoja na hilo kunywa kidonge kimoja cha Calcivita kila siku kwa muda wa mwezi mmoja. Asante.
 
Dr hujajibu tatizo langu la uvimbe kwenye kizazi.

Uvimbe kwenye kizazi inabidi ukamuone daktari bingwa juu ya swala hilo. Daktari wa Gynecologist. Itabidi afanye vipimo alafu akushauri.
 
habari dr
last time niliuliza swali sijapata jibu hadi leo......narudia huenda leo sitadharauliwa
nilifanya mapenz na mpenz wangu after one wiki nikawa nasikia maumivu makali wakat wa kukojoa na na ute mweupe unatoka sehem ya kukojole....pia muda mwngine nasikia maumivu hata bila kukojoa je nn hyo na ni dawa gan naweza tumia
AHSANTE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…