Dr. Sajjad Fazel
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 435
- 428
- Thread starter
- #301
Dr mi nauliza tatizo la mimba, mke wangu anateseka sana na hili tatizo, na tulishajaaliwa kupata watoto bila shida, ila kwa sasa tangu mimba ya mwisho ilipoharibika ukiwa na Miezi 3 akacheleweshwa kisafishwa tangu hapo sasa ni zaidi ya miaka 4 hatujafanikiwa tena, na utra sound akipimwa majibu ni kizungumkuti, kwingine unaambiwa kizazi na mirija safi, kwingine unaambiwa mirija imeziba madawa amekunywa ya kufungua mirija karibu nafungua famasi, mimi nimepima mbegu zimejaa, nisaidie la kufanya maana umri nao unatukimbia sasa hivi mke wangu Ana 42 age lakini bado anableed
Mkuu tafadhali kamuone Gynecologist. Hilo tatizo inaonekana kuwa ya kizazi chake mkewe. Dawa haiwezi kusaidia. Lazima Daktari bingwa wa wanawake na mambo ya kizazi afanye vipimo na akupe ushauri juu ya swala hili. Bila vipimo haiwezekani. Tafadhali mtafute daktari bingwa wa wanawake.