Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Pole na majukumu Dr.
Umekuwa kimya sana.
Niliuliza swali hili hapo juu "Je kupishana kwa tarehe za kuingia bleed period kila mwezi linaweza kusababisha mtu asipate mimba? Na je tiba yake ni ipi?"

Nitashukuru sana nikipata majibu.

Hapana, haisababishi mtu asipate mimba. Tiba yake ni dawa za homoni. Hizo dawa siwezi kukuambia kwasababu inabidi daktari bingwa wa wanawake amuone mtu aliyokuwa na tatizo hilo. afanye vipimo kama ya ultrasound alafu amuandikie dawa.
 
@Dr Sajjad Fazel

Dr miguu inauma sana
sina balace
misuli Ina spasm ,pin and needles

diclofenac hainisaidii kabisa labda kidogo Ligaba
Je ni multiple sclerosis?
Nini dawa yake maana maumivu ni non stop
thanks

Nahisi ni peripheral neuropathy na diclofenac haiwezi kusaidia. Tumia dawa hizi mkuu alafu nipe mrejesho:

1. Nuerorubine tablet, kunywa kidonge kimoja kila siku asubuhi kwa miezi moja
2. Pregabalin 75mg tablet, kunywa kidonge kimoja kila siku usiku kwa miezi moja.
 
Mkuu Dr.SajjadFazel! Nina tatizo kubwa ka miaka na miaka. 1. Naumwa chronic migraine hii ni almost kila siku 2. Napata uchovu na kuchoka pasipoishi pia mwili kuumwa karibia wote. Nateseka sana hapa Kipanda uso nimetumia dawa nyingi sana ikiwa ni pamoja na Botox injections

Ushauri mzuri ni kama upo Dar, uje Hospitali ya SANITAS iliyopo Mikocheni na umuone Daktari Hussein Bhalloo. Yeye ataweza kupa ushauri nzuri zaidi kwenye tatizo hilo kuliko mimi.
 
Doctor tunaomba msaada wa hilo swali lakupishana tarehe za blead

Hapana, haisababishi mtu asipate mimba. Tiba yake ni dawa za homoni. Hizo dawa siwezi kukuambia kwasababu inabidi daktari bingwa wa wanawake amuone mtu aliyokuwa na tatizo hilo. afanye vipimo kama ya ultrasound alafu amuandikie dawa.
 
Habari Dr pole na majukumu,Lakini naamini upo hapa kwa kutusaidia zaidi MUNGU akubariki..Dr tatizo langu ni kuwa na mbegu chache sana hivyo kutokupelekea kusababisha mimba kwani nimepima na Dr ameniambia Nina mbegu milioni 1 na ili usababishe
Mimba inafaa angalau ziwe mil4 sasa nataka kujua nifanye nini ili ziongezeke maana hata Kama nitapiga bao 3 bado ni kiasi kile kile,Au dawa gani itasaidia ahsante.

Tumia dawa hii mkuu, inaongeza idai ya mbegu za kiume pamoja nakuongeza kasi yake
- Provirone 25mg tablets, kunywa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa miezi moja.
 
asalam aleikum Doctor
Leo ni siku ya 3 nahisi maunivu chini ya kitovu. maumivu yenyewe yapo kama vile ukibanwa na mkojo halafu ukabonyeza kwwnye kibofu. maumivu yalianza chini ya kitovu pande zote siku ya kwanza then siku ya pili yakawa katikati na upande wa kulia sasa leo nimeamka naona ni upande wa kulia tu ndo kuna maumivu. sasa sijajua ndo yanakwisha ama ni tatizo ambalo linahitaji uchunguzi zaidi. Maumivu siyasikii hata nikiwa nakimbia au kufanya shughuli yoyote ile ila nayasikia nikibonyeza sehemu husika. Naomba ushauri wako nitumie dawa gani kama tatizo hili litaendelea. Asante

Inabidi umuone daktari bingwa wa upasuaji akupime kwanza alafu akupe ushauri.
 
Habari dokta pole kwa majukumu ya kazi me Nina tatizo la miguu toka mwaka 2003 nikitembea huwa inajigosha kwenye joint nisaidie dokta nimetumia supu ya kongoro...bamia...lakini tatizo ninalo mpaka Leo... Na nikitembea mwendo mrefu nachoka Sana... Dada Miriam

Tumia dawa hii alafu nipe mrejesho:

- Glucosamine Chondroitin, Kunywa kidonge kimoja kila siku asubuhi kwa muda wa miezi moja.
 
Habari za leo Dr. S. Fazel!!
Mimi niatatizo la muda mrefu kwamba kila ninapoenda haja kubwa huwa ninawashwa sana sehemu ya haja. Aidha hivi karibuni kuliibuka tatizo lingine nalo ni kwamba choo huwa na chembechembe za damu, nilienda kituo cha afya walinipatia dawa ila baada ya kumaliza dawa hizo tatizo limerejea palepale. Tafadhari naomba msaada wako mkuu.

Ushauri wangu ni hivi:

1. Jaribu kupunguza vyakula vyenye pilipili na viungo vingi.
2. Kula mboga na matunda mengi.
3. kunywa maji yakutosha.
4. Pakaa dawa hii kutwa mara mbili kwenye eneo inayowasha: Anusol Ointment
 
Una tatizo la fangasi na hiyo inafanya pia ikipata vibration ianze kuwasha. Ushauri wangu ni yafuatayo:

1. Hakikisha huvai nguo zinazobana
2. Hakikisha unabadilisha nguo za ndani
3. Kausha eneo la siri na mapaja baada kumaliza haja ndogo au kubwa.
4. Tumia dawa hizi:
- Terbinafine tablet, kunywa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa siku 28.
- Terbinafine cream na Hydrocortisone cream changanya hizi dawa mbili alafu, pakaa asubuhi na usiku kwa muda wa siku 28.
Dr. Sajjad nakushukuru sana na ubarikiwe sana kabisa.
 
Doctor naomba msaada kuhusu dawa hii "GYNEXIN" kama unaifahamu na inatibu nini na inapatikana wapi?
 
Ushauri wangu:

1. Rabeprazole 20mg, Kunywa kidonge kimoja kila siku asubuhi kwa muda wa miezi moja.
2. Punguza kula pilipili na vyakula vyenye pilipili au viungo vingi (spices).
asante kwa ushauri dr
ila naomba pia kuuliza je kunywa juice ya vtu vchahu kama vle ukwaju haina madhara kwa mimi ninaesumbuliwa na acid?
 
ila niliwahi kupewa dawa inatwa omeprazole je hy ni tofauti na hii rebeprazole? ki matumiz?

Ni bora kupunguza juisi kama hizo. Rabeprazole inafanya kazi vizuri zaidi. Hakikisha unazingatia ulaji bora kama nilivyokueleza.
 
Back
Top Bottom