Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Msaada na ushari kwa mtu anayesumbuliwa na Figo pamoja na kuvimba tumbo mara kwa mara. Nini anatakiwa afanye?

Kama mtu huyu anatatizo la Hernia au tatizo inayohusika na hicho Ni vizuri akamuone daktari bingwa wa upasuaji
 
Dr please nisaidie: nina tatizo la sehem ya mwili kuwa ngumu (SUGU) mfano kwenye unyayo wa mguu na kidole kidogo cha mguu kwa juu sielew hili tatizo linatokana na nini na tiba yake ikoje DR NAOMBA UNIJIBU MIMI HUKUNIJIBU PLEASE

Tumia dawa hii: Entezma, Pakaa kutwa mara mbili kwa muda wa miezi moja.
 
Dokta msaada!! Nasumbuliwa na matatizo ya mguu hasa wa kushoto unakua kama unawaka moto au kama nyama za ndani zinajikata kata
 
Ok, doctor habari! Mimi nauliza dawa ya fangasi ya miguu inapatikana wapi na matumizi yake yakoje, inatibu au inapunguza tatizo tu
 
Naulizia dawa nzuri ya m'ba.

Tumia Ketoconazole Shampoo inayopatikana kwenye duka la dawa. Tumia kama shampoo unapooga kila siku kwa muda wa wiki mbili alafu hakikisha unasuza nywele yako na kuipangusa na kukausha na taulo baada ya kuoga.
 
Ok, doctor habari! Mimi nauliza dawa ya fangasi ya miguu inapatikana wapi na matumizi yake yakoje, inatibu au inapunguza tatizo tu

Habari Mkuu,
Dawa ya fangasi inapatikana duka la dawa na ndiyo inatibu kabisa.
Cha muhimu nikuelewa kama fangasi wanapenda kuota kwenye nafasi yenye joto na unyevunyevu.

Hakikisha kwanza unaosha miguu yako Na sabuni alafu kuisuza Na maji Na baada hapo kuipangusa Na kukausha na kitambaa au taulo.

Alafu atumie dawa hii:
- Terbinafine Tablets, Kunywa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa miezi moja.
- Terbinafine Cream, Pakaa dawa hii Kutwa mara mbili asubuhi Na usiku.
 
Asante sana Doctor kwa maelezo mazuri kuhusu dawa ya fangasi na nitalifanyia kazi mara moja.
 
Dokta mzuri sana huyu........mimi sina ugonjwa wa kuombea ushauri ila naomba nitumie fursa hii kukupa baraka zangu kama raia kwakua unajitoa kutoa ushauri nasaha kwa raia wenzangu ambao masikini ya MUNGU wanataabika kupata ushauri sahihi wa kiafya huko uraiani kwa maana madaktari waliosomeshwa kwa kodi zao wanageuza taaluma hii ya udaktari kuwa ni biashara na kuwalipisha hata pasipo stahili. Endelea na moyo huu na nakuhakikishia ndugu daktari MUNGU huyu huyu wa mbingu na ardhi atakubariki wewe na uzao wako na ukoo wako wote mtabarikiwa na uttafunguliwa njia zaidi ya moja ya mafanikio yako. Ubarikowe sana ndugu daktari mzalendo, MUNGU ibariki AFRIKA, MUNGU ibarikiTANZANIA YETU, MUNGU mbariki daktari Sajjad Fazel mwenye upendo wa dhati na binadamu wenzake....ila MUNGU wafilisi C.C.M maana tumewachoka wakose hata hela ya kuhonga kwenye kampeni zao.
 
Back
Top Bottom